SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Mbona bado vivyo hivyo.

Jaribu kupitia tena kama unataka nijibu hoja zako.

Hii mada unayong'ang'ana nayo imekaa vibaya kwani kile kilichosemwa na huyo kaimu wa PAC na hilo tangazo la bunge ni kama kutuona watanzania wote ni wapuuzi kwamba hatuwezi kusikia na kuelewa mpaka hilo bunge linalonuka rushwa litutafsirie. Nikusaidie tu, usilazimishe kutetea mambo ya ajabu hata kama Magufuli yeye kama yeye anajitahidi kurekebisha mambo. Kimsingi mpaka sasa serekali inaonekana inaanza kuzidiwa kete na wahuni wa ccm kwani tabia hizi za kihuni za ccm ni kama samaki ndani ya maji na kitendo cha kujaribu kumtoa ni kutaka kukatisha maisha yake.
 
Kwanza nimekata andiko lako lote kwa sababu ninadhani hoja zinazotakiwa kujibiwa ni hizi nilizobakiza. Hoja zilizozikata nadhani ni hisia zako ambazo tayari umeziwekea hitimisho badala ya kuacha uwanja utakaoruhusu majadiliano.

Pili, Sijawahi kusema hakuna tatizo tatizo katika mkataba wa Lugumi na polisi. Nilisema kwa sasa vilimbi ni nyingi kiasi kwamba kwa mtu mwenye fikra pana hawezi kufahamu ukweli ni upi. Kutokufahamu ukweli hakuna maana kuwa hakuna tatizo.

Rekodi yangu ni kusubiri ukweli kamili ili niweze kujenga hoja zenye msingi wa ukweli badala ya hisia. Ninachokiona kwa upande wako ni kujenga hoja kwa kutumia hisia.

Nimeishapata fundisho kwenye suala la Hati ya Muungano kwenye Bunge la Katiba kuwa kujenga hoja kwa kutumia msingi wa hisia ni kutoka nje ya hekima na busara.

Tuliaminiswa hakuna Hati ya Muungano baada ya Ikulu kusua sua kuitoa kwa umma kumbe kelele zote tulizokuwa tunazipiga hatukuwa kwenye ukweli.

Wahenga husema, subira huvuta heri.
 
HOJA INAYOTAWALA SASA HIVI NI JUU YA KAMPUNI ZILIZOINGIA MKATABA NA POLICE: KINA NANI WAMILIKI! HII NDIYO HOJA. WAO WAUPELEKE HATA KAMATI YA AFYA AU MICHEZO. TUNACHOTAKA HUO MKATABA UWEKWE HADHARANI.
 
Ni aibu taasisi kama Bunge letu tukufu kuelekea kutumika kuficha uchafu! Nani tumuamini, kama Mheshimiwa Hilary Aeshy ametamka hadharani kuitaka Wizara na Polisi kuwapatia Mkataba halafu taarifa ya ofisi ya bunge inasema sio kweli?
 
Huu ni mtego mkubwa sana kwa serikali ya Rais tunaendelea kumuombea!Kweli ndio maana huwa anasema tumuombee kwa nguvu zote

Si ajabu alimwambia Cardinal Pengo kuwa "Urais ni kazi ngumu sana,angelijuwa basi asingegombea"
 
Inaniuma sana kuona hawa watu wanaanza kutetewa na kupindisha maelezo... Trump Yuko sahihi kabisa sijui lini wananchi tutaibuka na kupinga haya yanayotokea leo hii.... Ebu angalia Brazil wananchi wanapiga kula kumuondoa raisi wao... South Africa pia rais kabugi pia wanamtikisa sisi tunachekacheka ivi tutakua lini!!????? Ebu tuamke basi
 
Ugumu wa kutumbua Wanene kama Lugumu & followers .Mkuu bhana
 
Mbona tupo pamoja mkuu, kuanzia mwanzo hoja yangu ni kuwa kificho cha nini? Ninashangaa unasubiri ukweli, utaupata wapi ikiwa ilichukua 7 kutafuta faili na sasa yanazuka mengine kama haya ya bunge? Ukweli upi unaousubiri ikiwa mwenyekiti PAC aliomba mkatab, Mwenyekiti ulinzi na usalama akakiri kuupata, Bunge linasema kinachotakiwa ni maelezo ya kina. Ukweli upi tena na utaupata wapi?

Hakuna mahali nimeweka hitimisho la suala hili, hata hivyo ubabaishaji umezua hisia kwa jamii na ni haki ukizingatia serikali inasema hili, bunge linasema kile kamati hazijulikani zinafanya kazi gani, bunge halijui kamati zimeomba nini

Hoja hapa ni kuwa wanaficha ukweli, ndio maana tunawaangalia kupitia mboni za macho na kujiuliza, ndio hawa wanaosema wanapambana kweli?

Ukweli utapatikana wapi katika ubabaishaji uliopo?

Rekodi zinaonyesha ukibadili mwelekeo kila taarifa inapokuja! katika hali hiyo unaupta wapi ukweli? Ni upi unaoufuata!
 
Toeni taarifa kamili mseme kama hata hicho mlichoomba mlipewa au la????
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…