Kwa taarifa yako ni kwamba polisi huwa hawakamati waharifu huwa wanawakamata watuhumiwa wa uharifu,ambao bado uharifu wao haujathibitishwa kwa kuwa kazi ya kuthibitisha uharifu wa mtuhumiwa ni mahakama.
Kazi ya polisi ni kumkamata mtuhumiwa kulingana na tuhuma zilizopatikana kutoka kwa raia wema au kwa askari wenyewe,na kukusanya ushahidi utakao tumika kuthibitisha tuhuma za mtuhumiwa mahakamani kutoka vyanzo mbalimbali.
Katika suala la ukamataji, mtuhumiwa ndiye anayemshawishi askari polisi atumie nguvu ya namna gani katika ukamataji wake, ndio maana kuna usemi unaosema tii sheria bila shuruti, ukionyesha utii kwa askari aliyekuja kukukamata kutokana na tuhuma zako hakuna askari atakayetumia nguvu kukusurutisha kwa sababu tayari umeshafuta kipengera cha askari kukushurutisha kwa kuwa umechagua kutii pasipo kushurutishwa,mtuhumiwa ndiye anayechaguwa atendeweje na polisi.
Mtuhumiwa ndiye anayemjengea askari polisi mazingira ya kumkamata, ni nguvu ya kiasi gani itumike katika ukamataji mataji wake.
Mtuhumiwa akitaka akamatwe na askari polisi kama watu wanaokwenda pamoja kanisani kusali ni juu ya mtuhumiwa mwenyewe,jinsi atakavyoonyesha mwitikio wake wa kutii sheria pasipo shuruti kwa askari.
Matumizi ya nguvu/kuruka ukuta kwa askari polisi vinakuja pale ambapo mtuhumiwa anapokataa kuonyesha ushirikiano wa kutii sheria bila shuruti na njia zote hizi za mtuhumiwa kutii sheria,pasipokushurutishwa na kutii sheria kwa kushurutishwa zote ni njia za kisheria.
Ndio maana polisi kapewa rungu ili alitumie kwa mtuhumiwa ambaye amegoma kutii sheria bila kushurutishwa, kapewa silaha za moto, kapewa mabomu ya machozi, kapewa mabomu ya kubomoa kuta na kuvunja milango kwa lengo hilohilo la kutumia kumlazimisha mtuhumiwa atii sheria,na hakuna sheria inayomtaka askari polisi katika ukamataji wake akamchukue kiongozi wa mtaa au akamchukue jirani aje athibitishe ukamataji unavyofanyika.
Na hakuna hati ya kumpekulia mtuhumiwa anapokamatwa isipokuwa kuna hati ya kufanya upekuzi kwa ajili ya kutafuta mali zilizoibiwa au zimefichwa kwa nia ovu na hapo ndipo anapotakiwa kuhusika kiongozi yeyote wa mtaa au jirani kuja kuthibitisha upekuzi huo.