Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Kisheria watu wangapi wanaruhusiwa kuwa nyumbani kwenye makazi binafsi ya mtu?
 
Mtoa mada anatetea hata Mambo ya hivyo, huu Ni upotoshaji wa makusudi
 
Inatakiwa uelewe kwanza kuwa kanisani hakumaanishi wewe ni Mkristo, makanisa mengi ni makanisa ya shetani viongozi vyake uogopa kuwaudhi waumini Ili wasikimbie makanisa sadaka zikapungua.
Lakini wakafundisha ile kweli wengi awatoenda kanisani.
 
Usirudie Tena kumfananisha YESU na Uyo mfalme wenu.
Sio ajabu lakini,hata huyo Yesu alikataliwa na bado anakataliwa mpaka Leo hii na ndugu zake huko Uyahudi.... Ukienda huko Israeli na habari za Yesu wanakushangaa
 
Waanze na Mwamposa pale wanakula Hadi nauli in the name of sadaka ya kujimaliza,afuatwe Gwajima nae ndio muasisi wa kufufua misukule... kama vipi wampotezee tu huyu bibie
Mwamposa alisababisha hadi vifo Moshi kisa kugombania kukanyaga mafuta na sidhani kama alifunguliwa hata kesi ya manslaughter.
 
Pumzika sasa wacha mfalme Zumaridi apambane nayo yeye ndio mungu wenu. Kama wewe ni mkristo kweli usingemtetea sijali kuhusu mavazi yake kwanza libaya tu Ila ewe mkristo usikubali kumuita binadamu mwenzio au kumfananisha na Mungu.

Mie sijali anafanya mambo gani, anavaa nini, anaongea nini, anakaa na akina nani nk Ila kujiita Mungu aisee huyu hafai hata robo. Kwani angefanya hayo mazingaombwe yake bila kujiita hayo majina Kuna ubaya gani?

Kwani kuliita jina la Mungu kwa mizaha namna hii ni katazo kubwa kwenye biblia Kama wewe ni mkristo kweli basi kwako inatosha kuwa chukizo mbele yako kwakuwa hata mbele yake mwenye jina lipitayo majina yote ni chukizo na ubatili mkubwa kwa yite yanayofanyika pale.

Sijali anavaa nini Kama wengine wengi wanavyoisema in my view halitamanishi chochote libaya tu, Ila naudhika mtu kujiita Mungu.
 
Kitendo walichofanya polisi ni kuingilia uhuru wa kuabudu. Mbona wakatoliki wanafanya jumuia majumbani? Leo watamsakama Zumaridi sababu ni mdogo. Kesho watakuja kwenye dini kubwa zaidi.
Kosa sio kukusanyika, kosa ninkusafirisha watu 149.

Ndivyo hati ya mashtaka yake ilivyoandikwa.

Tusilete upotoshaji wa maksudi Hapa[emoji3525]
 
Sio ajabu lakini,hata huyo Yesu alikataliwa na bado anakataliwa mpaka Leo hii na ndugu zake huko Uyahudi.... Ukienda huko Israeli na habari za Yesu wanakushangaa
Leo umefeli sana
 
Inatakiwa uelewe kwanza kuwa kanisani hakumaanishi wewe ni Mkristo, makanisa mengi ni makanisa ya shetani viongozi vyake uogopa kuwaudhi waumini Ili wasikimbie makanisa sadaka zikapungua.
Lakini wakafundisha ile kweli wengi awatoenda kanisani.
Sasa tunaenda sawa,kwa kuwa umekiri kwa kinywa chako kwamba makanisa mengi ni makanisa ya shetani,sasa kwa nini anaonewa mmoja? kwa nini Zumaridi?si wakamatwe wote?
 
Dah... Hivi Ni Zumaridi au Zumalidi?....maana mnanichanganya😊🤭
 
Kosa sio kukusanyika, kosa ninkusafirisha watu 149.

Ndivyo hati ya mashtaka yake ilivyoandikwa.

Tusilete upotoshaji wa maksudi Hapa[emoji3525]
Kawasafirisha kutoka wapi kwenda wapi jamani?
 
Kuna watu wanaudhika pia wewe ukila Kitimoto. Lazima tujifunze kuishi kwa kuvumiliana imani na itikadi tofauti ilimradi watu hawavunji sheria wala kudhuru wengine.
 
Sasa tunaenda sawa,kwa kuwa umekiri kwa kinywa chako kwamba makanisa mengi ni makanisa ya shetani,sasa kwa nini anaonewa mmoja? kwa nini Zumaridi?si wakamatwe wote?
Simply fulani anafanya uasherati na hajakamatwa na mke au mume wake haimaanishi nawe hautakamatwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…