Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Kukamatwa ni hoja? Ngoja waende mahakamani ndiyo utajua kwamba wanatumia rasilimali za taifa efficiently? Ndiyo yale ya TAKUKURU unakamata na kufungua kesi Mia moja mwisho wa siku unashinda tano. Kumbuka hizo 95 ni fedha ya umma imeketekea hapo.
NDIYO maana nikasema SHERIA IKIFUATWA Hata DPP wanampunguzia Mzigo! Huko mahakamani Upande wa utetezi unaelezaga ushahidi wa kuchekesha! Mfano hapo shahidi akiombwa aieleze jamhuri ushahid wa kusafirisha binadamu atajibu nini?
Hao watoto wanaosemwa walitakiwa kuwa shule je anafaham wazazi wao wamewaleta hapo kuombea nini, je kama wanakifafa cha mapepo?

Siyo kila sehemu zinatatuliwa na polisi pengine ni wangetumia USITAWI WA JAMII INGETOSHA KUTOA ELIMU!

Ningewaelewa sana kama MASHITAKA YANGEFUNGULIWA NA NEMC na siyo polisi!
NEMC wangetumia sheria ya Air pollution na polisi wangekuja mwishoni ku-enforce law ya mazingira!

Lakini kusema anasafilisha binadamu ni makida makida
 
Sijaona kosa kwa polisi kwa maana Kama ingekuwa sehemu ya tukio ndio ungethibisha hayo uyasemauo acha polisi wafanye kazi yao
 
Sijaona kosa kwa polisi kwa maana Kama ingekuwa sehemu ya tukio ndio ungethibisha hayo uyasemauo acha polisi wafanye kazi yao
Haya subiri kama watampeleka mahakamani kwa hilo kosa la usafirishaji wa binadamu
 
Mharifu hawi mharifu hadi pale itakapothibitika!

Sakata la mfalme Zumaridi (Kiongozi wa kanisa la Zumaridi huko Mwanza) Linaacha midomo wazi kwa wapenda haki na utii wa sheria!

Sipo hapa kumtetea Mfalme Zumaridi, Bali nashangaa namna ya uharamu wa ukamtaji!

Taratibu za ukamataji kwa mujibu wa sheria ziko wazi kabisa lakini mamlaka zimekuwa zikionesha kufeli Mara kwa Mara kutekeleza sheria hiyo jambo ambalo limekuwa likitweza utu wa watu wasio na hatia.

MFANO! mambo kama haya yalitokea huko mtwara hadi kufedhehesha uongozi wa polisi ambayo yalianza hihivi kwa kufumbafumba mambo,

Mfano 2. Ni huko ARUSHA Kuna taarifa ya askali mzalendo kulalamika kutaka kuuwawa na polisi wenzake kwa mambo Yale Yale kama ya mtwara na serikali iko kimya.

SASA NI HILI SAKATA LA TATU LINALOTIA KICHEFCHEFU

Ni TUKIO LA zumalidi Siku ya kwanza inaripotiwa kwamba polisi waliruka ukuta/geti ili kuingia kwa Zumalidi! Kitendo hiki kilitakiwa kulaaniwa na kila mtu! (Waliruka kwa Zumalidi kesho wataruka kwako)

Kama kulikuwa na ulazima wa kufika pale kwanini hawakufuata utaratibu wa upekuzi unavyotaka? Kwanini hawa kumshirikisha mwenyekiti wa mtaa/mjumbe? Kwanini waliruka ukuta kama jambazi! (VIPI KAMA ZUMARIDI ANGEJIBU MASHAMBULIZI KWA KUFYATUA RISASI KWA POLISI ALIYEVAA KIRAIA ALIPORUKA UKUTA?) Ina maana wangejibu kwamba walikuwa kwenye mapambano na majambazi au?

Kwa utaratibu walio utumia polisi hauna tofauti na utarabu wa kijambazi! Na hili linachangia sana siku hizi RAIA kutokutofautisha kati ya jambazi na polisi.

Tukiachana na mbinu ya ukamataji!

Riport ya polisi ina ukakasi mkubwa juu ya mtuhumiwa Zumaridi!

Kosa walilo utaarifu Umma kwamba anasafilisha BINADAMU 149, kosa hilo Linatia aibu nyingine!

Hivi tangu lini watu wanaokusanyika kusali pamoja imekuwa kosa la jinai?

Mbona jumuiya na taasisi kibao tunawaona wanakusanyika na kukesha na haijawahi kutajwa kuwa ni kosa?

Zumalidi kasafilisha binadamu kutoka wapi kwenda wapi kwa lengo gani? Kuna jinai gani pale?

Hapo taifa juzi wakatoliki walikusanyika mbona haikutamkwa kuwa ni usafirishaji wa binadamu?

Kina mwingira na wachungaji kibao Tanzania kila kutwa wanakusanya watu na haisemwi ni usafirishaji,

INAKUWAJE JAMBO LILE LILE LIWE HALALI KWA MWAMPOSA LAKINI LIWE HARAMU KWA ZUMARIDI?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Nawashauri TAKUKURU WAINGILIE KATI!
Haiwezekani sheria zipo wazi, kwanini zisingefuatwa kama kweli ZUMALIDI anamakosa makubwa hivyo!

Mimi kwa utashi wangu nahisi sakata la Zumaridi lina maslahi binafisi!

TUKIRUHUSU HAYA YA UKIUKWAJI WA SHERIA HAKUNA ATAKAYEBAKI SALAMA!

Itakuwa mtu akikosana na polisi wanakuja kuluka ukuta! Na majambazi nao watatumia mwanya huohuo kufanya uharifu!
Ww ni miongoni mwa ile mijinga iliyokuwa inaigiza kuwa ni mazombi? Maana unachokitetea ni kitu cha kipumbavu na hakina maana.. sasa huo ushenzi wa zumaridi ni wakutetea
 
Mbona wasabato huwa wanahubiri dhidi ya Papa na wako huru?
Nakubaliana nawe kwa maana ya ukiukwaji wa sheria ila mfalme wako anakashfu imani za watu wengine kitu ambacho kinaweza sababisha uvunjifu wa amani
 
NDIYO maana nikasema SHERIA IKIFUATWA Hata DPP wanampunguzia Mzigo! Huko mahakamani Upande wa utetezi unaelezaga ushahidi wa kuchekesha! Mfano hapo shahidi akiombwa aieleze jamhuri ushahid wa kusafirisha binadamu atajibu nini?
Hao watoto wanaosemwa walitakiwa kuwa shule je anafaham wazazi wao wamewaleta hapo kuombea nini, je kama wanakifafa cha mapepo?

Siyo kila sehemu zinatatuliwa na polisi pengine ni wangetumia USITAWI WA JAMII INGETOSHA KUTOA ELIMU!

Ningewaelewa sana kama MASHITAKA YANGEFUNGULIWA NA NEMC na siyo polisi!
NEMC wangetumia sheria ya Air pollution na polisi wangekuja mwishoni ku-enforce law ya mazingira!

Lakini kusema anasafilisha binadamu ni makida makida
Imeisha hiyo...wewe ni kerubi.
 
Mleta uzi anazungumzia namna ya ukamataji sio makosa anayosemwa nayo huyo Zumaridi
Kama mimi na wewe hatufahamu huyo Zumaridi anasafirisha kina nani toka wapi kwenda wapi tuwaachie polisi wafanye kazi yao, unaonekana umekuja kulalamika bila kuwa na uthibitisho wa malalamiko yako
 
Tofautisha cult na kanisa ninvitu viwili tofauti. Kuna kitu serikali inataka kufanya ili kuzuia Mambo Kama ya Jim Jones na David Koreish kutokea Tanzania. Ila watu hawajaielewa Sana.

Cult nyingi huanza kwa kuwa na makambi na kukusanya watu sehemu moja baadae ndio hutokea.

Kasome historia ya cult ya Jim Jones na David Koreish ndio utaelewa. Walianza hivi hivi lakini mwishowe maafa yalikuwa mabaya.
Cult ni nini?
 
Kwa jangiri kama hilo Police nawatetea kabisa,kama nawewe ni muumini basi jua Police wanajaribu kukufumbua macho kuwa huyo SI kiongozi wakanisa Bali ni jambazi linalotumia dini
Kwa nini unamuita jangiLi na jambazi?
 
Mbona unalazimisha Mambo ya uongo. Kuna mchungaji gani anauza maji na mafuta. Tofautisha manabii na mitume na wachungaji usiwachanganye kapu moja.

Wanaouza mafuta Ni mitume na manabii. Na serikali imeingia Kati na Sasa mitume na manabii kujiandikisha na kuwa na umoja wao.
Mitume na manabii wanajiandikisha na kuwa na umoja wao?!
 
Umejitahidi kueleza ingawa umeeleza kana kwamba wewe ni Mfuasi wa Zumaridi.
Anyway haki itendeke!
 
Kwa jangiri kama hilo Police nawatetea kabisa,kama nawewe ni muumini basi jua Police wanajaribu kukufumbua macho kuwa huyo SI kiongozi wakanisa Bali ni jambazi linalotumia dini
Kwani kiongozi mzuri wa dini ni mpaka atoke kwenye haya makanisa ya wazungu..au wewe kiongozi wa dini unampima kwa vigezo gani..je huko unakoamini kuna viongozi sahihi wa dini mbona kila siku wamejaa maovu na mazambi mengi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kudanganya
Ukweli katika Imani ni subjective
Kwa kukusanya watoto wa wenyewe akawafuga kama mbuzi
kwahio anafanya child molestation, abuse au kidnapping ?
Kuhubiri upumbavu
Upumbavu kwako kwa mwingine ni neema unless otherwise anakashifu wengine
Kujipatia kipato kinyume na sheria
Sheria ipi ? Kama nilivyosema Imani ni subjective tukikazia hapa huenda sadaka zote zikapigwa marufuku
Kuwatumikisha watu na kuwafanya mabwege
Subjective mwingine anaweza kusema vilevile kwa imani zote
Kujifananisha na Mungu
Mungu yupi ? Wa Waisraeli, wa Rastafarians, wa Hindus, wa Mababu zetu au wa Wafuasi wa Zumaridi...,.
Soma Katiba utajifunza mengi
Nadhani nawe wahitaji kufanya hivyo...
Usisahau kusoma Vitabu Vitakatifu pia
Vitakatifu kwa nani ?, Nadhani Huyu pia ana vitabu vyake vinavyomuongoza kufanya afanyavyo...

To each his/her Own

Kwa kuishi kistaarabu nadhani tuvumiliane kwa kila mmoja na Imani Yake..., so long as Imani yako / yao isiwe Kero kwa Wengine...

Kuna Mengi wanayoweza kushitakiwa hawa watu wa Imani (Public Nuisance n.k.) ila sidhani uliyoorodhesha hapo juu yana angukia kwenye hio category.... (ukizingatia kama wote ambao wanarubuniwa ni of legal age)
 
Back
Top Bottom