Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Hata kumtetea yule mama inabid akili iwe imefyatuka kidogo. Ona tu walivokuwa wanajifanyisha vya kizombi. Hakuna mtu mle. Mama tapeli ni muuaji wa nguvukaz ya Taifa. Nae atakuwa si mzma
 
Angekuwa anakashifu dini ya kislamu huyu angekuwa marehemu ila kwavile amekashifu ukristo mmegeuka kuwa watetez wake


Ukristo unakataza visasi na hukumu strictly.

Imeandikwa; visasi na hukumu viachwe mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Ukristo unaagiza kuwapenda hata maadui.

Na kwamba akupigae shavu moja mgeuzie na pili akupige , akinyang’anyae kanzu mpe na joho.

Mtu akisema ni dini ya amani kwa muktadha huo itaeleweka kwa vitendo.
 
nawaona makerubi mmeanza kujitokeza hadharani

kipindi hiki mnakuja kwa uso wa binadamu na siyo misukule tena😀😀
 
Nakubaliana nawe kwa maana ya ukiukwaji wa sheria ila mfalme wako anakashfu imani za watu wengine kitu ambacho kinaweza sababisha uvunjifu wa amani
amekashifu vp? wakati na yeye anahubiri kwan hakuna uhuru wa kuabudu. ana tofaut gan na kakobe, Nabii shila, mwamposa na wengineo
 
Comment iwekewe ulinzi hii na ichongewe kabati kabisa

Uhuru bila nidhamu nifujo
 
Kosa walilo utaarifu Umma kwamba anasafilisha BINADAMU 149, kosa hilo Linatia aibu nyingine!

Hivi tangu lini watu wanaokusanyika kusali pamoja imekuwa kosa la jinai?

Hapa naona upotoshaji wa makusudi ili kujenga hoja yako. Kosa ni anasafirisha binadamu wewe unasema kukusanyika
 
Yote KWA yote hivi waumini wa zumaridi sahiv sadaka wanampa nani [emoji849][emoji849]nami ngoja nikafungue kakanisa kangu huko niibe waumini wa zumaridi waje KWA babyfancy church [emoji39][emoji39]
 
PGO vp haikutumika?
 
Niliwahi ona clip moja ya huyu mama akiwa kwa ibada na watu wake aiseee ilikuwa ni kama zile muvi za mazombi sikutamani hata kulisikia jina lake.

Kwa hili kiukweli nawapongeza polisi.
 
amekashifu vp? wakati na yeye anahubiri kwan hakuna uhuru wa kuabudu. ana tofaut gan na kakobe, Nabii shila, mwamposa na wengineo

Tofauti Ni kubwa Kakobe anaamini kwenye Trinity lakini Mfalme Zumaridi haamini katika Trinity Yani utatu mtakatifu. Kuhusu nabii shila huyo sijui yupo kundi lipi maana aliwahi kumkashifu Yesu Kristo.
 
Nadhan miaka kadhaa nyuma (sikumbuki exactly ni lini) serikali ilitangaza kulifungia kanisa la huyu Zumarid. Na tokea wakat huo hatujawah kusikia km kanisa hilo limeidhinishwa kuendelea na huduma zake.

Kwangu mm binafsi naanzia kupata fikra kinzani kuhusu kukamatwa kwake Dianna Bundala. Kuwa ikiwa had hiyo juz alikuwa chini ya amri ya kufungiwa huduma na mamlaka za serikal,ujasiri wa kuanza kukusanya watu ktk misingi ya ibada ileile ambayo kazuiliwa atakuwa kautoa wapi?
Na endapo labda kimyakimya serikal ilishamruhusu aendeleze huduma zake,kosa lake litakuwa ni lipi hapo?

Lakin pia hatua ya kuwatuma vijana wake kujifanya vichaa (uzombi) ili tu kuwadhibit polisi wasitekeleze jukum lao,ni hatua inayotosha kisheria kukamatwa regadless ni matokeo yapi ya mbele.
Watu tusijisahaulishe ya Kabwetele Uganda lkn pia ya Bulldozer kule Moshi!
 

Una shida kubwa Sana unahitaji msaada. Wewe unaichukulia dini Kama biashara kisa watu wachache wanafanya Mambo kinyume na mapenzi ya Mungu. Dini ya Kikristo misingi yake Ni amri kumi na kufuata Maisha ya Yesu Kristo ya utakatifu na utaua. Wewe macho yako yapo kwenye sadaka badala ya kuokoa roho za watu wasiangamie.

Naomba uelewe kidogo. Mimi Sina conflict na Zumaridi , ila nachosema tofautisha cult na ukristo. Haiwezekani mtu haamini kwenye misingi ya ukristo halafu unamwita mchungaji. Anauchafua ukristo wakati yeye sio mkristo, halafu lawama linapelekewa kanisa. Mtu yeyote asiyeamini kwamba Muhamad alikuwa mtume wa Allah huyo sio muislamu au kuamini nguzo tano za uislamu.

Shida yangu ni kwamba Zumaridi anajiita Mungu na anadai ya kwamba Yesu kwa Sasa Hana nguvu, yeye ndio ametumwa kuja kuukomboa ulimwengu. Sasa mtu anamkana Yesu Kristo na kujiita Mungu Chini ya jua utasemaje ni mkristo na kuanza kushutumu makanisa kwa ajili yake. Yeye aanzishe dini yake na imani yake ajitoe kwenye ukristo Hilo ndio nalo take, sio unajificha kwenye ukristo wakati humuamini Yesu Kristo.
 
Halafu siyo kila kitu lazima muingize siasa. Polisi waligonga, ila watuhumiwa wakagoma kufungua. Kwa mazingira kama hayo unataka waachwe? Hii chuki kwa Polisi itakuua usipokuwa makini.
Umejuaje Kama walisikia wakigongewa mlango pengine walikua wanalia.....mzuka umepanda
 
Cult ni nini?

Cult ni Imani ambayo ipo kinyume na dini husika. Kwa mfano wewe Ni muislamu Halafu ukaanzisha imani ya kutokutambua Mfungo wa Ramadhan kuhiji na Utume wa Muhhamad. Wewe ukadai ndio mtume wa Allah, tunasema huo sio uislamu ni cult. Zumaridi ana sifa zote za Cult, maana anajiita mungu Chini ya jua, wakati Mungu aliye hai kupitia Biblia anakataza mtu kuchukua utukufu wake hata tone.

Kiukweli mwisho wa cult zote huwa Ni mbaya Sana watu wengi hufa au kupoteza mwelekeo wa Maisha. Mfano mzuri ni Jim Jones wa Marekani aliyeua wafuasi wake 900 kwa sumu aliwadanganya Ni meza ya Bwana huko Guyana porini walipoenda kujificha. Au David Koreish aliyepambana pamoja na wafuasi wake dhidi ya FBI kwa siku 51 na baadae kuamua kujilipua wote wakafa. Msome mtu anaitwa Apple white alichokifanya mwishoni kwenye cult yake na kibwetere.
 
Mitume na manabii wanajiandikisha na kuwa na umoja wao?!

Ni ushauri wa serikali ili kudhibiti matapeli. Na Rais wao Ni Nabii Joshua na Mlezi mkuu Ni Askofu Dunstan Maboya. Huu umoja wao utasaidia mengi hasa kwenye suala la kutapeli waumini pesa zao na baadala yake washughulike na huduma za kiroho.
 
Hakuna limit kwenye uchaguzi wa maneno

haaaa! haaaa! Umenichekesha Sana. Kwamba hakuna limit ya kuchagua maneno, hivyo leo unaweza kumwita Baba yako Mama akaitika. Usifike huko kubadilisha jinsia za watu kisa Zumaridi.

Concept ya Mfalme Zumaridi Ni kwamba yeye ni baba kwenye mwili wa kike. Kwamba mwili wake Ni wa kike ila roho yake Ni ya kiume ndio maana anaitwa mfalme. Shida ya Cult ni kwamba Ina mfanya mtu haukatae ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…