Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Kwenye crude piga kodi ya maana ili viwanda vyetu vikue
We ndiyo hazimo kabisa. Utakapotoza kodi kubwa wakati hatuna malighafi za kutosha, unadhani utakuwa unamkomoa mfanyabiashara au mtumiaji wa mafuta.

Hii ni kama mtu akuambie tuache kupanda mabasi yaliyotengenezwa China ili yaliyotengenezwa Tanzabia yawe na wateja wakati unajua hakuna mabasi yaliyotengenezwa Tanzania.

Alizeti za kupima kwa magunia na madebe, kwa akili yako unaamini zinaweza kulisha kiwanda japo kimoja tu kwa mwaka?
 
Jamaa anauliza swali....

Mzungu akianza kuongea na kutolea ufafanuzi yeye anainama chini... akiinuka ananyosha mikono juu... kwa ishara kanakwamba anasema yaishe bhanaa... anashika bega la huyu nashika bega la yule.... yaani !!! Hivi uliyaanza ya nini...

Mwangalie anavokuelezea sasa namna ya kutengeneza mafuta aiseee mda mwingine nikadhani ni Kinyamwanga ndo kinatumika..... aahaahaaaa

Kweli ilikuja na mtumbwi lugha hii

BACK TANGANYIKA
Tunachotaka sisis ni suluhu ipatikane.Habari ya Kingereza au Kijerumani hata vichaa wanaongea sio issue.Kingereza hakimalizi shida zetu mkuu
 
Kwenye Ofisi ya AG alikuwa na tabia ya kufanya amendment ya Muswada uliotoka bungeni. Yaani wabunge wanapitisha sheria, yeye anaeda kubadilisha na kuweka maneno anayoyataka yeye ndo anampa rais asaini. Ni tabia mbaya ilikuwa.
Hivi hili si nikosa la jinai...! Huyu mwanasheria anayesemwa hapa, hawezi kuchukuliwa hatua?
 
cheap public stunt.
create the problem, then come back in and offer the solution that the people demand.
Unaakili za 'kushangaza'...wewe kiumbe. Yaani serikali ndiyo ilikuwa inachanganya mafuta semi na crude oil baharini ? Yaani serikali ndiyo ilikuwa inadanganya kuwa tumeleta crude oil kiasi kadhaa kumbe uongo?
 
​

Mhe. Rais Magufuli afanya ziara ya ghafla bandari ya Dar es salaam muda huu. Anakagua matanki ya mafuta ya kula. Fuatilia matangazo TBC1 muda huu.

Atembelea kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam na kupewa maelezo kuhusu Mafuta kukwama bandarini.

Rais Magufuli amesema...

Baada ya kufanya uchunguzi imebainika kuwa kwenye matanki hayo kuna ambayo yalikuwa na 'crude oil', na mengine yalikuwa na 'refined oil' ambayo yalifichwa kwa makusudi.

Wafanyabiashara wanaotumia nafasi zao kulaghai watu, huwa mnawasikia kwenye vyombo vya habari wanasema mwaka huu mafuta yamepanda bei. Nawaomba tuwe wazalendo. 'Crude Oil' ichajiwe bei ya juu ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Haiwezekani 'crude oil' ukachaji sawa na 'semi refined', na hii sheria yetu inawezekana kulifanyika mchezo. Wabunge walipitisha kitu kingine, kilicholetwa huku ni kingine, kinachokuja kupitishwa kuwa sheria kimebadilishwa kuwa kingine.

Hii 'crude oil' ichajiwe bei ya juu ili watu wengi wajenge viwanda hapa, tujenge nchi yetu.

====

UPDATES:

Rais Magufuli anasema;


=> Nlituma wachunguzi wangu waje kufanya analysis ya haya mafuta. Wote wameleta majibu sawa. MAfuta yanafaa kwa matumizi ya binadamu. Nmesoma ripoti yote.

=> Ukitaka kutengeneza mafuta yoyote, kwanza mafuta yote yanatokea kwenye crude Oil, yakishatoka kwenye crude Oil..unafanya Neutralization na kwenda semi-refined oils au bridging kuchange colour of oil. Viwanda vingi vya tanzania ni semi refined Oil. Double refined.

=> Tatizo tulilonalo;

*Crude inachajiwa 10%

*Semi refined inachargiwa kwa 10%

Sasa unakuta vyote vinachajiwa sawa.

=> Haya mafuta yaliyoleta hapa ukiuliza yametoka wapi hutopata document, haya ni yale mafuta yanayonunuliwa baharini, waliombwa na TRA leteni document zinazoonesha mafuta haya yametoa Malesia au wapi, Hawana. Baada ya kukosa document tukapata mashaka. ndo wakaanza kuzunguka wanasema kwenye tv na radio kwamba mafuta yameisha yamepanda bei, tukachukua wataalam wakakusanya sample hizi na kuangalia kama yamafaa kwa matumizi.

=> Wamechunguza yale yote yanatotakiwa kujua. Bahati nzuri tukakuta hayana tatizo. Tukaamua tujue kama ni cude au semi refined au double refined. Na wao karibu yote walisema ni Crude. Kwahiyo watapigwa faini ya kufanya udanganyifu. Yaliyobaki mtank manane wala sio mafuta, ni material ya kutengenezea sabuni. Hayafai kuliwa. tumeyawekea alama.

=> Nchi yetu tulifanya makosa ndani ya Serikali katika kutunga Sheria ya Mafuta ya kuliwa. Nawaagiza Wizara ya fedha na viwanda wakafanye marekebisho bungeni kuhusu hii sheria ya mafuta

Nmeagiza mafuta yaanze kutoka leo


Nlituma watu waje kufanya uchunguzi wa kitaalam. wakafanya analysis. Wameleta matokeo;

=> Vegetable oil, katika sample 13, matanki mawili (namba 4 na namba 12), haya yana double refined oil wanatakiwa kulipa 25 % ya charge

=> Kuna matenki 4 yana materials ya sabuni yalipiwe 10% na Mengine yote yalipiwe 10%

=> Tanzania liquid storage tank namba 3 ina double refined litalipiwa 25% Mengine yote yachagiwe 10%

=> Kuna mafuta East Coast Oils, imegundulika mafuta yote ni semi refined 10% na Matenki manne (ecb 1, 2, 9, na 3) yatalipiwa 25%

=> Katika Sample 13, matanki 7 yote yana content ya double refine, yanatakiwa yachagiwe 25%, na yaliyobaki yanachajiwa 10%

=> Natoa wito, kwenye mafuta hapa, haya nmeruhusu yatoke kutokana na condition. Lakini kama watadanganya tena wapigwe fine

=> Nawaagiza Mpeleke amendment bungeni ili mtu akileta crude semi refined au double refined chages zitolewe kutokana na mafuta aliyoyaleta.

=> Crude manaake haijafanyiziwa process yoyote. Hakuna mfanyabiashsara anayeweza kwenda ulaya kuleta crued

=> Hii sheria ya mafuta ni ya Hovyo, hili ni kosa letu kama Serikali. Hauwezi kuleta crude ukachaji 10%

=> Sitaki itumike advantage ya mwezi wa ramadhani kwa kudai mafuta yanahitajika halafu tuwape chakula hakifai. Ndo maana tukafanya uchunguzi kabla ya kurhusiwa.

=> Double refined ni pipa saba. watayatoa kwa 25% na kupigwa faini ya kudanganya.

=> Kafanyeni marekebisho ya Sheria ya Mafuta. Haiwezekani crued Oil ikachajiwa sawa sawa na Semi refined

=> Kwenye Ofisi ya AG alikuwa na tabia ya kufanya amendment ya Muswada uliotoka bungeni. Yaani wabunge wanapitisha sheria, yeye anaeda kubadilisha na kuweka maneno anayoyataka yeye ndo anampa rais asaini. Ni tabia mbaya ilikuwa.

=> Kaimu kamishina wampe ukamishina wa TRA kamili. (Rais Dkt. John Magufuli amempandisha cheo aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA, Ben Usaje na kuwa Kamishna kamili TRA bandarini hapo baada ya kusimamia vyema mchakato wa kukagua mafuta yaliyokuwa na utata bandarini)

=> Kaimu mkurugenzi wa TBS simamieni masirahi ya serikali bila kudanganya. Ongeeni ukweli kama mambo yalivyo.

=> Mkemia mkuu, nataka sample zote mtakazokuwa mnapewa fanyeni kwa utaratibu kwa kuzingatia maadili yenu. Mkiletewa madawa ya kulevya, kesho msiseme unga wa muhogo. Mkemia mkuu na TBS zingatia maadili yenu.

=> Hawa mliofanya analysisi nawashukuru sana mumesimama kidete.

=> Hakuna tatizo la mafuta, na taratibu zikikamilika mafuta yataingizwa sokoni

Wafanyakazi wa bandarini wameulizwa kama wana chochote cha kumuuliza rais wakasema hamna mwenye swali wala maoni

Nlitamani niende kuchwa chai kwa mama lishe, ana nini? ngoja nikanywe chai. Anaenda kunywa chai kwa mama Lishe.

Amenunua matunda ya Elfu 30.

Paralyzed system!!
Hivi mheshimiwa Rais asingekwenda ingekuwaje?
Hivi PM alipotoa siku tatu alikuwa na habari zipi za uhakika?
Hivi aliyekamatwa Songea for hoarding na haya tunayoyaona,nani ni mkosaji?
System iamke sasa
 
Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,hujui kwa nini rais anataka kodi halisi,endelea kupiga domokaya
Kilichofanyika ndiyo kilitakiwa kufanyika siku nyingi zilizopita. kutoa ripoti ya ukaguzi kutoka chombo kinachoaminika na wote kwamba ukweli ni huu na kodi stahili ni hii. Hiyo ingefanywa tu na waziri na mambo yakaenda. Kama TBS na Mkemia walikuwa wazembe, waadhibiwe kwa mujibu wa taratibu. finish. kama alivyosema Ndugai, hiyo siyo ROCKET SICENCE. lakini kwa kuchelewesha muda wote huu, hizo gharama atalipa mwananchi one way or the other. taifa limepata hasara.
 
Unaakili za 'kushangaza'...wewe kiumbe. Yaani serikali ndiyo ilikuwa inachanganya mafuta semi na crude oil baharini ? Yaani serikali ndiyo ilikuwa inadanganya kuwa tumeleta crude oil kiasi kadhaa kumbe uongo?
mkuu mbona unanishambulia kwa maneno makali sana?. [emoji23]

mbona unaniuliza swali gumu sana?.[emoji23]
 
Tatizo langu kubwa ni moja. Hata ukiwa nyumbani kwako unaweza kupima mafuta na kujua haya ni crude au refined kwa kigezo cha Free Fatty Acid. Unahitaji Sodium Hydroxide, Ethanol na Indicator(hivi unaunua kwenye maabara ya mtaani tu) na gram 10 za mafuta kufanya neturalization process ambayo kama itachukua muda mrefu sana ni robo saa. Hata mwanafunzi wa darasa la saba akielekezwa anafanya kwa ufanisi mkubwa tu hii kazi. Sasa hiki kilichokuwa kinaendelea kati ya TBS mara TFADA mara mkemia mkuu kwenye maPHD mara waziri yaani naona kizunguzungu.Siku zote hizo wameshindwa kujua kuwa haya mafuta ni crude au refined hadi mgogoro umefika bungeni hadi kwa rais. Kweli mtu akisema yupo frustrated ana haki. Labda niamini kuwa kulitegeshwa upigaji mkubwa. Unless kuna kitu sjaelewa vizuri
Huna unalolijua
 
Wala hujamwelewa na inaelekea hutakaa umuelewe.
Sasa kama huyu anashindwa kueleweka kwangu, tena mimi kachala niliyekulia kijijini "Handalie" kwa umri wangu wote wa 'Kijana maji ya moto'...ataeleweka kwa nani sasa, uh !?
 
Jinsi ya kutawala wajinga kiakili:
1. Create a problem
2. Create a solution to the problem you created in (1) above.
3. Repeat.
 
cheap public stunt.
create the problem, then come back in and offer the solution that the people demand.
Hakuna unachokijua zaidi ya kuongea utumbo mkuu. Pole sana. Sisi tunasonga mbele
 
Kwenye crude piga kodi ya maana ili viwanda vyetu vikue
Anadhani watu wanaagiza semi na double refined na kudanganya kuwa ni crude oil. Sasa badala ya ku deal na hilo kisheria yeye anapiga kodi mara dufu eti watu waache kuagiza crude oil. Tusubiri muda kidogo tu watu wataanza kulia bei ghali ya mafuta. Hiyo ni raw material ya kuchakata mafuta. Tanzania hata madawa ya binadamu tunaagiza tu nje kisha tunachanganya. Sasa na hizo porojo zake tusubiri maumivu.
 
Siku ya mwisho ya awamu ya kwanza ya miaka 5 natabiri atatokea kwenye ziara ya kushtukiza na kuanza kampeni.
 
jamaa anapenda kweli live covarage. yupo live anaelezea process za kutengeneza/ kuchuja mafuta. crude, semi refine double refine na maprof sijui nini? ina kera kweli
Pasuka sasa
 
Back
Top Bottom