Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

sijapitia contributions zote kwenye thread hii lakini kuna maneno ya rais yameniacha kinywa wazi (nimeyanukuu hapa chini). amekuwa misquoted, au mimi ndiyo sielewi mtu anielimishe kidogo?

Nanukuu..
Rais Magufuli amesema...

Baada ya kufanya uchunguzi imebainika kuwa kwenye matanki hayo kuna ambayo yalikuwa na 'crude oil', na mengine yalikuwa na 'refined oil' ambayo yalifichwa kwa makusudi.

Wafanyabiashara wanaotumia nafasi zao kulaghai watu, huwa mnawasikia kwenye vyombo vya habari wanasema mwaka huu mafuta yamepanda bei. Nawaomba tuwe wazalendo. 'Crude Oil' ichajiwe bei ya juu ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Haiwezekani 'crude oil' ukachaji sawa na 'semi refined', na hii sheria yetu inawezekana kulifanyika mchezo. Wabunge walipitisha kitu kingine, kilicholetwa huku ni kingine, kinachokuja kupitishwa kuwa sheria kimebadilishwa kuwa kingine.

Hii 'crude oil' ichajiwe bei ya juu ili watu wengi wajenge viwanda hapa, tujenge nchi yetu.

Mwisho wa kunukuu
 
We ndiyo hazimo kabisa. Utakapotoza kodi kubwa wakati hatuna malighafi za kutosha, unadhani utakuwa unamkomoa mfanyabiashara au mtumiaji wa mafuta.

Hii ni kama mtu akuambie tuache kupanda mabasi yaliyotengenezwa China ili yaliyotengenezwa Tanzabia yawe na wateja wakati unajua hakuna mabasi yaliyotengenezwa Tanzania.

Alizeti za kupima kwa magunia na madebe, kwa akili yako unaamini zinaweza kulisha kiwanda japo kimoja tu kwa mwaka?
Malighafi za mafuta ni zipi?
 
Anadhani watu wanaagiza semi na double refined na kudanganya kuwa ni crude oil. Sasa badala ya ku deal na hilo kisheria yeye anapiga kodi mara dufu eti watu waache kuagiza crude oil. Tusubiri muda kidogo tu watu wataanza kulia bei ghali ya mafuta. Hiyo ni raw material ya kuchakata mafuta. Tanzania hata madawa ya binadamu tunaagiza tu nje kisha tunachanganya. Sasa na hizo porojo zake tusubiri maumivu.
Hebu niambie hapa TZ ni kiwanda gani kinatoa mafuta double refined?? Najua hakuna kiwanda cha kutoa double refined bali kuna viwanda vinavyotoa semi refined. Sasa jiulize kwa nini mafuta ya semi refined kutoka nje yanatozwa kodi ya 10% kama crude oil?? Huoni huo ni mchezo ambayo mafisadi walikuwa wanautumia kukwepa kodi ?? Ndiyo maana magonjwa ya moyo yameongezeka sana kwa sababu ya kuchanganya mafuta hayo na kuuzwa mitaani.
 
Director wa movie alikosea kuidirect.....

Kijana akapindisha script.

Safi sana kijana...umewakilisha wengi....

Hali ngumu mtaani. Amekuambia ukalime...ungemwambia sina mtaji.
 
Huyo kijana alimfuata magufuli kuomba hiyo nauli? Shilingi ngapi? Nauli ya kwenda wapi?
 
jamaa anapenda kweli live covarage. yupo live anaelezea process za kutengeneza/ kuchuja mafuta. crude, semi refine double refine na maprof sijui nini? ina kera kweli
Ukiona hivyo usiku hakulala alikuwa akipiga msuli.....

Semi refined/ Double refined [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom