Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Sakata mafuta ya kula: Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta

Serekali ya awamu ya 5 inapigwa vita sana na wafanya biashara, na wabaya zaidi ni wale wakizalendo wsiopenda kulipa kodi.

Na zaidi ya wafanyi biashara ni wapiga domo wa humu JF, amabo kazi yao kubwa waliyotumwa ni kupinga na kukosowa lolote zuri linalofanywa.

Haya mafuta yalikwama kuingia mitaani kwa sababu muingizaji alidanganya ili alipe kodi ndogo na apate faida mara 10. Kigogo wa TRA akagoma na kusisitiza walipe kodi ipaswavyo. Raisi katumia power yake kuwapa nguvu TRA ya kutimiza kazi yao.

Nawauliza wote wanaiponda ziara ya raisi ambayo ni kazi yake, jee ni kosa kutetea wananchi kwenye hili?
 
Ni wendawazimu kusababisha tatizo halafu ujifanye unatatua halafu utegemee kushangiliwa. Lazima uwe mjinga hasa kushangilia mambo kama haya.

Ni miaka mingapi hatujawahi kuwa na tatizo la mafuta wala sukari? Nani aliyesababisha upungufu wa sukari na mafuta?

Aliyeumbwa na uso wa haya, angejitahidi kwenda kimya kimya.
Kasababishaje tatizo, au ulipenda hao wafanya biashara wangeachiwa wafanye walotakalo.

Hebu piga hesabu nchi ingekosa kodi kiasi gani, na kukwamisha kuyaingiza mafuta madukani, bei imempanda wananchi wanatizwa bei ya ziada, imagine kiasi gani kinapotea kwa wanamchi pamoja na nyumbani kwenu.
 
Tushazoea kushtukiziwa na hamna litakalofanyika. Moja ya kiki zake.
 
Kwahiyo crude oil kodi 25% na semi refined ni 10%, kumbe unaweza kuexport raw material? Mnatulisha makinikia ya mafuta ya kula, nyambafu shenzi zenu,
Sasa mimi nashindwa kuelewa! Crude oil si ndiyo mwekezaji anatakiwa ajenge kiwanda cha kuyachakata hayo mafuta ili yaende kwenye semi refined na baadaye double refined? Sasa unatozaje kodi kubwa kweye malighafi ya kiwanda? Ila nilivyomsikia anazungumza nikabaki mdomo wazi eti yatozwe kodi kubwa ili kulinda viwanda vyetu. Sasa mfanyabiashara akileta semi refined au double refined si ataua viwanda vyetu pia? Jamani anayeelewa haya mambo hebu atusaidie tumechoka kulishwa matango pori na huyu jamaa!!
 
Ikiwa umefuatilia hili saga tokea mwanzo utaona TBS walikua upande wa wafanyabiashara kwa kusema hayo mafuta ni ghafi ila TRA wao wakakomaa na kusema na safi so walipe 25% badala ya 10% ya ghafi. Cha kushangaza hapa ni je, wao TRA wana mamlaka gani kuingilia kazi ya TBS ilhali hawana utaalam wa kupima ubora wa bidhaa?
Tra ni kikwazo cha ukuaji wa wafanyabiashara wengi,cha msingi inabidi waachiwe wafanye Kazi ya uajenti wa kuagiza vitu au bidhaa,wao waagize kisha sisi tununue kwao Maana kila bei wakiletewa wanakataa wanakupa bei watakayo wao utadhani wao ndo manufacturer,
 
=> Kwenye Ofisi ya AG alikuwa na tabia ya kufanya amendment ya Muswada uliotoka bungeni. Yaani wabunge wanapitisha sheria, yeye anaeda kubadilisha na kuweka maneno anayoyataka yeye ndo anampa rais asaini. Ni tabia mbaya ilikuwa.

😳🙁😱 Aiseeeeeeeeeeee... Kumbe AG ulikuwa mchezo wake huu. Mh. Rais kaweka waziiiiii leo.. Eeeeeehh..!!! 😱😱😱😱😱😳😳🙁🙁
 
Kusema kweli mshua yupo sawa kwani ninyi mnaobeza mlitaka afanyeje?
 
Sasa crude oil si ndo inatakiwa ichajiwe chini maana refine zifanyike hapa tz ila magu chemistry ulisoma kweli au
Hata mm ndio nilielewa hivyo,ghafi au crude ndio inabidi itozwe kdg semi na refined zitozwe juu maana hata gharama za manunuzi kati yao ni tofauti. Lakini kwa upande mwingine ni sahihi ili kulinda viwanda na malighafi zinazozalishwa nchini ,ushuru ya Crude oil ukiongezwa itawalazimu kuagiza semi refined ambazo bei ya manunuzi ni kubwa au kulazimika kuanza kutumia malighafi kutoka nchini. Madhara yanayoweza kujitokeza ni kupungua kwa utendaji wa viwanda vya Ku process mafuta endapo wafanyabiashara wataamua kununua refined na kupack tu au kutopatikana kwa malighafi ya kutosha kwa msimu wote wa mwaka kutoka kwa wazalishaji wa ndani ,hii itapelekea baadhi ya watu kukosa ajira .
 
Ziara za kushtukiza zimerudi tena? Bandari watakuwa wanaomba jamaa ahamie Dodoma haraka. Hata hivyo sina imani na ziara zake za kushtukiza kwani hazijawahi kuleta nafuu yoyote. Suala la suukari alichokoza mpaka leo ameshindwa kurudisha bei ya zamani ya 1800/= Suala la makinikia mpaka sasa hatima yake haijulikani. Kishika uchumba hatujui kilikoishia na hatujui mpaka sasa mchumba ni nani
 
CCM bana walipitisha sheria wao leo wanaruka as if hawakujua chochote kile kwamba karibu 60% ya sheria zetu tulipigwa na tunaendelea kupigwa, nani alizipitisha?.

I will always Trust & Believe in Lissu.
 
Magu anapiga kazi hata mkisema ni cheap stunt au cheap publicity lakini mbona marais wengine hawakufanya zaidi ya kutuma watu huku wao wakiwa kwa malikia wanapiga white wine
 
Picha za akiwa anakunywa chai kwa mamantilie feki
 
Back
Top Bottom