PreGE2025 Salma Kikwete: Mchinga Wamesema Ubunge Mpaka Nichoke Mwenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Jitu Zima kuwa muongo muongo ni hatari, wanatia aibu. Uongo kwa wanasiasa ni maisha yao..tuwapuuze
 
Huyu bungeni amekuja kupiga umbeya, hakuna analofanya....Elimu hana kama huyo mumewe. Eti hadi uchoke? Wananchi gani wamesema? Tupe ushahidi.......Kama ni kura halali utashindwa vibaya, lakini kwa vile mumeo yupo karibu na Samia, na kwamba yeye ndiye anayemuongoza Samia, yaani ni defacto President, ubunge utaupata bila shida.
 
Nasikia mwanamama mmoja anasema lindi inaongoza kwa nyumba za nyasi 🥺😭

Duuuh na katoka first lady humo ten yrs plus five years za ubunge kama sikosei duuh,

Huko mpk pm katoka
 
Huyu mama anatamaa kupita kiasi hafai kwenye jamii
1:Amezuia ajira kwa mtu mwingine, wakati yeye anaendelea kufaidi masurufu ya mume wake, na pia ya "MWENZA WA RAIS"
2:Amepunguza mzunguko wa fedha, ambazo zingetumiwa kutoka kwa m'bunge mwingine tofauti na yeye, kwani yeye karibia kila kitu analipiwa na Serikali!
 


Na wewe ndugu yangu unashabikia, mtu ambae ashakuwa first Lady miaka kumi anakuwa mbunge wa jimbo maskini

Hana nguvu tena ya mwili wala akili,

Ashakuwa mtu mzima,

Ndio maana majimbo ya kusini ni maskini sana
 
Na wewe ndugu yangu unashabikia, mtu ambae ashakuwa first Lady miaka kumi anakuwa mbunge wa jimbo maskini

Hana nguvu tena ya mwili wala akili,

Ashakuwa mtu mzima,

Ndio maana majimbo ya kusini ni maskini sana
Kuongoza na uongozi ni akili na siyo umri. Ni suala la hekima ,busara ,maono , uzalendo, uchapakazi na ubunifu.uongozi siyo kubeba nzege au kunyanyua vyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…