Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Wakinyimwa hongo ndio unasikia usanii huo eti wamekamata shehena , hapo kuna mtu tra au policcm kanyimwa mgao WA rushwa so kaamua kuwalipua wenzake
Da ila hawa jamaa TRA huwa nawaonea huruma sana maana kila jambo wakifanya ni kama vile ukisimama nchale ukikaa nchale hawana jema wafanyalo . sidhani kama kila jambo likiibuka inakuwa ni rushwa naamini wapo wazalendo wengi tu ambao wanataka taifa letu lifike mbele
 
Huoni mawaziri 8 wako mikoani kutatua kero/migogoro ya ardhi? Kumbuka huko mikoani kuna RC, RAS, DC, DED, DAS etc
Ni kukosa ubunifu na kazi za kufanya

Washauri wa huko juu sijui wanakosea wapi
 
Leo tarehe 13 Oktoba 2022, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata shehena ya mizigo ya vitenge ya marobota 290 katika kontena mbili yenye thamani zaidi ya tsh. Billioni 5 iliyopitishwa kwa magendo katika bandari zetu.

Mfanyabiashara mwenye shehena hiyo alitorokea Dubai majuma matatu yaliyopita, huku TRA wakiweka doria na ulinzi mkali sana.

Mfanyabiashara huyo wa Kariakoo, mtaa wa Aggrey, Bi. Salome Mgaya, maarufu kama 'Mama Kibonge' au 'Mkinga' amekuwa akifanya jambo lolote bila kuguswa na yoyote pindi anapoingiza mizigo yake nchini kwa njia za magendo. Muda mwingine amekuwa anawatishia watumishi wa Bandari au TRA kuhamishwa au kufukuzwa kazi.

TRA wameendesha Operesheni Maalum chini ya Waziri wa Fedha Mwigulu Madelu Nchemba na kuweza kumdhibiti Mama Kibonge.

Mama Kibonge amekuwa akidaiwa kutamba kwa zaidi ya miaka kadhaa bila kukamatwa na kuguswa na mamlaka nchini Tanzania.

Kwa wasiofahamu na wanaomtetea Mama Kibonge kukamatwa kwa Mizigo yake hawajui kuwa, wanamtetea mkwepaji kodi, fiisadi na haramia wa Mapato ya Nchi yetu.

View attachment 2386213
Ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
 
Inawezekana vipi mzigo upite bandarini bila kulipiwa kodi? Nafikiri ili haki itendeke, chain nzima inayohusika na ukwepaji wa kodi, isiachwe bila kuguswa.
Lazima kuna genge la wanaoshirikiana. Sio kikosi cha mtu mmoja
 
kwa hiyo miaka yote hawakumshtukia tu? isije ikawa kuna njemba ilienda kinyume na makubaliano ikaona bora imchome tu mmh! nawaza tu.

Mifumo yetu bado ya kizamani sana, pale bandarini ikiwezekana wasafishe wote tuanze upya na system mpya.

HUYO MAMA KIBONGE NI MFANO TOSHA KUWA SYSTEM YA BANDARINI BADO HAIKO SAWA, WAHUSIKA WAWAJIBISHWE!!!

Ingekua kwa mabeberu hapo bandarini kuna watu wangekua kazi hawana.

Hivi TRA hizo kodi mlizoziweka ni kwa ajili ya watanzania au wa zambia? Too much!
 
Mama bonge...hajawah shindwa vita...na hii vita anapigwa na boss wa simba na mamluki kibao..kuna kaumafia fulan hivi kwenye hii biashara ya vitenge....kuna mmoja anataka kuwa supplyer na ni billionea na mzawa lakin kiwanda chake hakikidhi uhitaji wa bidhaa kwa hao wahitaji.,,na hapa ndio vita ilipoanzia tokea enz za Magu....

NB bil 5 kwa mama bonge...aah jaman mbona wanamchafua...pesa ya mandaz kabisa hyo...
Alipe kodi tu kama wenzake hatutakuwa na shida naye.

Kama wenzake wanalipa kodi na yeye anakwepa hiyo inakuwa unfair competition.
 
Hii inathibitisha kuwa mfumo wa ukaguzi bandarini ni mbovu na hata uandaaji wa nyaraka na upitishaji mizigo mipaka ya nchi jirani ni questionable
Hapo huwa anakula na hao hao TRA na bandari sema labda walipandisha dau ama kuna mwenzao walimpiga hawakumpa posho yake akaamua kumwaga mboga....na ikishakuwa hivyo wote aliokuwa akifanya nao huo uharamia wanamruka futi 260 kulinda vibarua vyao
 
Jambo zuri ni kuwa TRA wameendesha Operesheni Maalum chini ya Kamanda na Jemedari Waziri wa Fedha Mwigulu Madelu Nchemba na amethubutu na kuweza kumdhibiti Mama Kibonge.[emoji23]
Nshumbi Madelu
 
Alipe kodi tu kama wenzake hatutakuwa na shida naye.

Kama wenzake wanalipa kodi na yeye anakwepa hiyo inakuwa unfair competition.
Na wanaomuwezesha ambao wamo kwenye mifumo wawajibishwe. Yeye peke yake hawezi kufanya hayo.
Nani wako naye?
 
Nasikia Ana chura tupieni picha yake basi

Ova
 
Nimecheka sana yaani TRA wanatoa mzigo wa Transit kwa gari ambayo hata Chalinze haiwezi kufika...ishu ya vitenge ni vita kama biashara ya unga wapo walikua wanauana hapo Kariakoo wengine hawasafiri wanategemea mizigo ya kuiba tuu na wana mitaji mikubwa usiku kwao ndio mchana kama mapopo utaona Ma vieti yanazunguka tuu wana siraha na cash za rushwa sio subiri utatumiwa...
 
Back
Top Bottom