Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Hii inathibitisha kuwa mfumo wa ukaguzi bandarini ni mbovu na hata uandaaji wa nyaraka na upitishaji mizigo mipaka ya nchi jirani ni questionable
Naunga mkono hoja?
Huu uzembe wa wazi au ombwe kubwa kupitisha mizigo kiholela
 
Makontena yote yana tracker. Na pia all transit Containers lazima pale Kibaha zihakikiwe kabla ya kuendelea na Safari- How comes hii itokeee mara nyingi kwa huyu mama kuwa ni mkwepa kodi?? Ina maana basi port, TRA yote ipo mfukoni kwake😁
Wewe ndugu hiyo tracker inahamishiwa kwenye bodaboda inaendeshwa mpaka mpakani, wanatoa documents zinagongwa
Waulize vijana wa mlandizi bodaboda wanapewaga dili za kupeleka tracker s mpaka mpakan
 
Aliwezaje kusurvive enzi za Magufuli huyo mama kibonge?
 
Shehena ya mzigo wa magendo uliokamatwa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mali ya Mfanyabiashara Salome Mgaya maarufu kama mama Bonge.

Vijana waaminifu wa TRA wakiwa katika majukumu yao ya kawaida wamefanya kazi nzuri ya kizalendo kwa kukamata makontena mawili ya magendo yakiyokuwa yamebeba shehena ya vitenge baada ya kuvamia moja ya store za mfanyabiashara mkwepa kodi.

Bi. Salome Mgaya ni nguli na sugu anayehusika katika mtandao wa utakatishaji Pesa, vipodozi feki pamoja na magendo mengine nchini.

Rada ya Vijana wa TRA hawakuona hata chembe ya aibu kwa kuogopa kwa kuhakikisha mzigo huo unakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kutimiza kiapo cha ukusanyaji kodi.

Mzigo huo wa magendo ulikamatwa baada ya watumishi wa mamlaka ya mapato kutilia shaka mzigo uliokuwa ndani ya Contena mbili uliokuwa unaelekea Chipata nchini Malawi.

Surveillance iliyofanywa kwa umakini na watumishi wa TRA kufuatilia ndipo walipogundua mzigo huu umechepushwa mitaa ya Tabata matumbi na kuelekea katika maghala ya bidhaa yanayomilikiwa na Bi Salome Mgaya.

Mara baada ya askari Polisi kuingia katika eneo la maghala hayo kwa ajili ya upekuzi walizuiwa na Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Mparuka Mtopela hata baada ya kutoa utambulisho Mtopela ndiye aliyetumwa pia kuzuia habari hii isisambae katika vyombo vya Habari.

Timu maalum ya ukusanyaji Kodi ilifanikiwa kufanya upekuzi baada ya Mtopela kutoweka katika eneo la tukio ambaye alikuwa anajaribu kuzuia maafisa wa mamlaka ya mapato wasifanye ukaguzi katika marobota hayo na kukuta kuwa mzigo huo uliokuwa umeandikwa ni mashuka kuwa ni vitenge.

Maafisa wa mamlaka ya kodi walipojaribu kumpigia simu Bi. Salome Mgaya kufahamu juu ya mzigo huo alikiri kuwa mzigo huo ni wake na kukatiwa simu. Taarifa zinasema kwa msaada wa Mnene mama bonge ametorokea Dubai.

Mtoto wa Mnene anayefahamika kwa jina Saad na Kennedy Mgaya Maarufu kama (Kenzo) mtoto wa mama Bonge walifika eneo la tukio lakini walitoweka kabla maafisa wa kikosi maalum hawajawatia nguvuni.

Zipo taarifa kwamba Saad katika kutaka kuzima soo aliamua kumpigia simu Waziri wa Fedha ili awasaidie kuzima ishu hii kubwa ya kashfa ya ukwepaji kodi ya mabilioni katika bandari ya Dar es salaam.

Kwa Muda mrefu kampuni ya Saad mtoto wa mnene ifahamikayo kama SK imekuwa ikihusika na Utoaji wa mizigo wa kampuni Gherisa Enterprises ambayo ni kampuni ya Bi. Salome Mgaya ambaye amekuwa akifanya Biashara pamoja na Bwana Mnene hadi kufika mtoto wa mnene kuwa rafiki wa karibu na mtoto wa Bi. Salome. ambao ndiyo waanzilishi wa kampuni ya SK yaaani (Saad&Kenzo).

Gazeti hili limepata mawasiliano binafsi kati ya Saad na kenzo haya hapa.


IMG_7820.jpg
 
Huyu mtendaji mkuu wa Serikali ndo PM siyo? Hii tatizo sana mama amtoe anaharibu kasi
 
Mfanyabiashara mwenye shehena hiyo alitorokea Dubai majuma matatu yaliyopita, huku TRA wakiweka doria na ulinzi mkali sana.
[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Heading inatofautiana na maudhui
 
Mfanyabiashara mwenye shehena hiyo alitorokea Dubai majuma matatu yaliyopita, huku TRA wakiweka doria na ulinzi mkali sana.
[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Heading inatofautiana na maudhui

Kifupi anetoroshwa….

Tafuta huu mzigo…..
 
Mama bonge...hajawah shindwa vita...na hii vita anapigwa na boss wa simba na mamluki kibao..kuna kaumafia fulan hivi kwenye hii biashara ya vitenge....kuna mmoja anataka kuwa supplyer na ni billionea na mzawa lakin kiwanda chake hakikidhi uhitaji wa bidhaa kwa hao wahitaji.,,na hapa ndio vita ilipoanzia tokea enz za Magu....

NB bil 5 kwa mama bonge...aah jaman mbona wanamchafua...pesa ya mandaz kabisa hyo...
Pesa ya maandazi kwake ?
 
Hii inathibitisha kuwa mfumo wa ukaguzi bandarini ni mbovu na hata uandaaji wa nyaraka na upitishaji mizigo mipaka ya nchi jirani ni questionable
Sijui yale malalamiko ya mbunge mmoja (KE) kwa waziri Mwigulu yamemuamsha huyu Waziri. Mbunge alisema: Acheni kunyanyasa watanzania walala hoi kwa hizi tozo zenu, badala yake wabaneni matajiri wanaokwepa kodi.

Kimsingi wakwepa kodi ni wengi, si huyu mama kibonge peke yake. Mchezo umeanza!!!!!!
 
Back
Top Bottom