Shehena ya mzigo wa magendo uliokamatwa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mali ya Mfanyabiashara Salome Mgaya maarufu kama mama Bonge.
Vijana waaminifu wa TRA wakiwa katika majukumu yao ya kawaida wamefanya kazi nzuri ya kizalendo kwa kukamata makontena mawili ya magendo yakiyokuwa yamebeba shehena ya vitenge baada ya kuvamia moja ya store za mfanyabiashara mkwepa kodi.
Bi. Salome Mgaya ni nguli na sugu anayehusika katika mtandao wa utakatishaji Pesa, vipodozi feki pamoja na magendo mengine nchini.
Rada ya Vijana wa TRA hawakuona hata chembe ya aibu kwa kuogopa kwa kuhakikisha mzigo huo unakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kutimiza kiapo cha ukusanyaji kodi.
Mzigo huo wa magendo ulikamatwa baada ya watumishi wa mamlaka ya mapato kutilia shaka mzigo uliokuwa ndani ya Contena mbili uliokuwa unaelekea Chipata nchini Malawi.
Surveillance iliyofanywa kwa umakini na watumishi wa TRA kufuatilia ndipo walipogundua mzigo huu umechepushwa mitaa ya Tabata matumbi na kuelekea katika maghala ya bidhaa yanayomilikiwa na Bi Salome Mgaya.
Mara baada ya askari Polisi kuingia katika eneo la maghala hayo kwa ajili ya upekuzi walizuiwa na Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Mparuka Mtopela hata baada ya kutoa utambulisho Mtopela ndiye aliyetumwa pia kuzuia habari hii isisambae katika vyombo vya Habari.
Timu maalum ya ukusanyaji Kodi ilifanikiwa kufanya upekuzi baada ya Mtopela kutoweka katika eneo la tukio ambaye alikuwa anajaribu kuzuia maafisa wa mamlaka ya mapato wasifanye ukaguzi katika marobota hayo na kukuta kuwa mzigo huo uliokuwa umeandikwa ni mashuka kuwa ni vitenge.
Maafisa wa mamlaka ya kodi walipojaribu kumpigia simu Bi. Salome Mgaya kufahamu juu ya mzigo huo alikiri kuwa mzigo huo ni wake na kukatiwa simu. Taarifa zinasema kwa msaada wa Mnene mama bonge ametorokea Dubai.
Mtoto wa Mnene anayefahamika kwa jina Saad na Kennedy Mgaya Maarufu kama (Kenzo) mtoto wa mama Bonge walifika eneo la tukio lakini walitoweka kabla maafisa wa kikosi maalum hawajawatia nguvuni.
Zipo taarifa kwamba Saad katika kutaka kuzima soo aliamua kumpigia simu Waziri wa Fedha ili awasaidie kuzima ishu hii kubwa ya kashfa ya ukwepaji kodi ya mabilioni katika bandari ya Dar es salaam.
Kwa Muda mrefu kampuni ya Saad mtoto wa mnene ifahamikayo kama SK imekuwa ikihusika na Utoaji wa mizigo wa kampuni Gherisa Enterprises ambayo ni kampuni ya Bi. Salome Mgaya ambaye amekuwa akifanya Biashara pamoja na Bwana Mnene hadi kufika mtoto wa mnene kuwa rafiki wa karibu na mtoto wa Bi. Salome. ambao ndiyo waanzilishi wa kampuni ya SK yaaani (Saad&Kenzo).
Gazeti hili limepata mawasiliano binafsi kati ya Saad na kenzo haya hapa.