Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Kwa mujibu wake anasema kontena moja kuliingiza pale bandari ni sh. 200m mpaka 300m wakati kenya na zambia wao wanaingiza kwa 45m tu. Sasa just imagine hapo jinsi ngoma inavyokuwa ngumu hapa ndani na wakati mizigo ya zambia inapitia pale pale bandari yetu.


Hii nchi ni ngumu sana kutoboa biashara kwa uhalali hata mimi simdai kwa kweli.
 
Kuna kitu hakipo sawa hasa katika maswala ya kodi nchini Tanzania na hapa anatafutwa mbuzi Wa kafara katika hii movie .Nilazima waliopewa dhamana ya kuongoza nchi kuzingatia viapo vyao na ningeomba mama awe mkali kwa wasaidizi wake maana walio wengi ni wapigaji they don't mean what they say ile style ya jpm panga pangua ili kuwa ni sababu ya haya maukakasi tunayo yaona nchini kwa sasa. Kama Dar usoni mwa nchi kuna utusi tusi mwingi wa namna hii habari gani huko mikoani kwenye halmashauri ,mipakani ?
 
Kashakula chaka kwenye tume hiyo. Huyo kama TRA wameshamuambia jana akachukue mzigo wake ina maana hapo kuna watu walikuwa wanatengeneza mazingira yakumpiga hela.
hujasikia vema akachukue na aende nan1/3 ya contena zake kwa maana 3bil unadhani anaenda tupu?
 
Kwa Jinsi wafanyabiashara walivyoeleza ,ni wazi watendaji wanaweka kodi zisizolipika ili mradi watu watoe rushwa na wao wapate chao,kuna mfanyabiashar alitoa wazo ambalo kama mwigulu angelitekeleza serikali ingepata kodi mara mbili ya waliotarget wao lakini hawakusikiliza mawazo yao zaidi ya kuongeza tozo kutoka laki 8 hadi 2.4m
 
Leo tarehe 13 Oktoba 2022, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata shehena ya mizigo ya vitenge ya marobota 290 katika kontena mbili yenye thamani zaidi ya tsh. Billioni 5 iliyopitishwa kwa magendo katika bandari zetu.

Mfanyabiashara mwenye shehena hiyo alitorokea Dubai majuma matatu yaliyopita, huku TRA wakiweka doria na ulinzi mkali sana.

Mfanyabiashara huyo wa Kariakoo, mtaa wa Aggrey, Bi. Salome Mgaya, maarufu kama 'Mama Kibonge' au 'Mkinga' amekuwa akifanya jambo lolote bila kuguswa na yoyote pindi anapoingiza mizigo yake nchini kwa njia za magendo. Muda mwingine amekuwa anawatishia watumishi wa Bandari au TRA kuhamishwa au kufukuzwa kazi.

TRA wameendesha Operesheni Maalum chini ya Waziri wa Fedha Mwigulu Madelu Nchemba na kuweza kumdhibiti Mama Kibonge.

Mama Kibonge amekuwa akidaiwa kutamba kwa zaidi ya miaka kadhaa bila kukamatwa na kuguswa na mamlaka nchini Tanzania.

Kwa wasiofahamu na wanaomtetea Mama Kibonge kukamatwa kwa Mizigo yake hawajui kuwa, wanamtetea mkwepaji kodi, fiisadi na haramia wa Mapato ya Nchi yetu.

View attachment 2386213
Hatimaye leo Waziri mkuu ameujuwa ukweli na mama Kibonge ameteuliwa kwenye tume ya serikali na wafanyabiashara.
 
Kashakula chaka kwenye tume hiyo. Huyo kama TRA wameshamuambia jana akachukue mzigo wake ina maana hapo kuna watu walikuwa wanatengeneza mazingira yakumpiga hela.
Na badala yake mama kibonge ndio anaenda kuwa wajibisha maafisa wa TRA waliokua wakimsumbua...🤣
Leo mende ameangusha kabati...😜
 
Back
Top Bottom