Nonsense!Natamani niseme kwa jina la JMT, juu ya uhuru wa mitandaoni, sasa basi.
Wizi wa namna hii, UKEMEWE tena kwa nguvu. Ikimpendeza Raisat Samia afanye maamuzi magumu.
Hata kama ni kumwajibisha Bashungwa na Katibu Mkuu wake. Walaghai wanaibuka na kila uongo wa habari ili tusome uongo, lakini wako wameongoza dola mifukoni. Waziri wa shetia haoni hilo.
Umakonda una mapungufu yake, lakini una pia MAZURI YAKE. Unafikiri mateja Makonda asingethubutu, Leo vijana wangekuaje?
China hii Leo inayompiku mmarikani kwa kila hali, haikuwa na mchezo upande wa Malezi ya utu wa watu wao. Tambua kwamba Vyombo vya habari ndiyo SHULE ya WATU WAKO Samia Mama yetu Mpendwa kwa kuwajengea fikra, mtazamo, utambuzi, muelekeo, ilimu, uoni, ubunifu, marejeo, mabadiliko n.k.
Hili sio jambo LA kuchekeana, ikiwa tu wa kweli wa nia, maneno na matendo.
MATENDO, MATENDO Mama yetu Raisat Samia, ndiyo Mtangulizi wako hayati Magufuli alizamia. Hivi kweli, mtu ili auze habari, ana danganya kimtandaoni, je huyo si mwizi? Mh Bashungwa, unashindwa kuwalundika magereza wezi hawa ambao ushahidi uko live. Inahitaji kweli hadi Ikulu ijitetee! Naibu Spika mko wapi? Hii ni nchi yetu. Muda wakukaa kwenye nafasi za uongozi kama ajira, sasa basi. Tunautaka uzalendo. Tunataka nchi yetu taifa la USWAHILI linyanyuke kiutambuzi, TUJITAMBUE. Itawezekanaje tujitambue ikiwa Vyombo vya habari ni mamluki majambazi, maharamia mabaradhuli makuu?
Makamu wa Rais yupo anangojea kutumwa na Rais. No!
Tunataka tuwe kama Korea, japani, dubai, Singapore n.k; hii ni kazi yako mpendwa MAKAMU. UJASUSI MZURI, UIBE UTAALAMU, TEKELINALOKUJIA UIBE, TAIFA LA USWAHILI LIKWAMUKE. Unayo majeshi Tisa. Ya nini hayo kama sio miradi ya wazungu? JWTZ limekuwa jeshi LA ulinzi kwa miaka mingi tu. Makamu wa Rais! Tuambie linalinda nini, ili hali hata kijiti cha kuchokonolea nyama kwenye meno tunaagiza kutokana nje?
Enyi wateuliwa na Rais, huko kwenye majukwaa kulonga hili au kile waachieni makatibu tarafa na madiwani. Ofisi zenu ni kubwa, fanyeni makubwa. Mitandaoni, makonda makonda! Kulikoni? Hata mimi simpendi Makonda. Kwani mimi ni mkewe?
Ila enyi WATEULIWA, igeni UMAKONDA (matendo, acheni umbea [UTENDAJI]). Magufuli kama mtu, mimi simtaki, simtaki kabisa. Mimi sikuwa make wake, wala mwanaye. LAKINI "UMAGUFULI" UTAENDELEA KUWA PAMBO LA MOYO WANGU!
Raisat Samia, maneno haya siyasemi tu, ila kwa uchungu mkubwa. Katika kila taifa, ili JAMII itoke katika hali duni kufikia hali yenye nafuu katika huu ulimwengu wa manyang'au -UMAGHARIBI, inahitaji UMAGUFULI {UMAO TSE TUNG}, UMAKONDA [UTENG SHIO PING]. U u sote hizo, vichwa kukatwa ndio kawaida. Hii ni KWA sababu u u zote hizo ni msemeno. Ukiweka mkono wako kwenye njia ya msemeno, unatarajia nini kama sio kukatwa?
Huu ndio UMAGUFULI unataka sisi Waswahili tuwe na chetu. Ikiwa wewe kwenye mfumo huu ulitaka uendelee na umagharibi ghushi, vichwa vikaanguka; wakulaumiwa ni wewe, nyie au SISI.
KWA NINI SOMO HATULIPATI:
1) Wairaqi walipo jaribu kujinafasi na kuwa na chao, wale wairaq wasioutaka USADAMU, wakatumiwa na maadui. Sadamu akanyongwa hadi kufanya.
Leo Iraq imechakaa.
2) Walibya, Gaddafi wakamuua wenyewe. Leo Walibya wanajuta. Gaddafi alitaka Bara letu "BARA LA WATU" tuwe na fedha yetu, mtandao wetu n.k. HAWAKUMUACHA. Je! Lumumba, Sankara, A. T Balewa wa Nigeria, sina nigeria wanasota hadi Leo. Je! Nyerere? Walianza kumuita Musa Nabii. Baada ya hapo walikuwa wamuite kichaa. Huku ya mbwa kichaa ni mini? Si kuawa? Basi walipopata mchepuko wa kwenda hispitali ulaya, basi ndio hivyo tena!
3) HAYATI MAGUFULI, miezi mitatu haijaisha. Yuko wapi? Magufuli yule ambaye sote kwa utashi wa kila mmoja, tulijitamba naye, KAONDOKA. A' Alituambia tuko vitani. Lakini ni nani alimsikia? Jemedari mkuu wa majeshi ya taifa letu USWAHILI kafa vitani, watu sote KIMYAAAA! Majeshi 9 -sungusungu, mgambo, magereza, JMT, polisi, ffu, jwtz, usalama wa taifa, sote ziiiiiiii. Mama Raisat Samia, watu namna hii ndio tuliokuzunguka. USIWE KAMA SISI!
TAIFA:
Taifa tunakuangalia wewe. Ukituangakia sisi, umekwisha.
1) Nyerere aliangalia juu, akitafuta MUELEKEO, akajenga barabara, mashule, mahosipitalu, vyuo, viwanda, majeshi n.k.
2) Mwinyi na mazuri aliyofanya, alimwangalia Nyerere, akaishia Mtanikumbuka, akasemwa, mkewe ndiye mshauri wake.
3) Mkapa na makubwa aliyofanya aliishia kuwauzia mamluki viwanda na mashirika bila kujipanga.
4) Kikwete na ukweli wake, wachache walinona; wakaishia kumuita dhaifu wale wale alio walinda
4) Magufuli na umagufuli AKAUKWAA MUELEKEO. MUNGU AWEKWE MBELE. Tukaona matunda kwa muda mfupi.
5) Samia, tayari mvua zimekuwa fupi. Ile kauli ya Mungu awe mbele imeachwa; njaa hiyo inakusogelea. Usiseme tu 'kwa jina LA JMT', LA. Bali sema KWA JINA LA "MOLA" WA JMT, KAZI IENDELEE.
Tambua Mama Malkia wa Uingereza ni mkuu wa dini ya taifa lao - uanglikani. Makel ni mkuu wa chama cha kikristo. Na wewe uwe mkuu wa dini ya taifa letu - UNYENYEKEVU:
Misingi hii mitatu ya maisha-
1) UAMIMIFU,
2) HESHIMA na
3) UTII,
Ndiyo dini yetu watu weusi, iliyoletwa na Manabii wa Mungu Nuhu, Ibrahimu, Musa, Yesu/Isa na Muhammad. Q42:13, ya kwamba ikulu isomamishwe bila Kufarakana. Ndio maana Uingereza sana vyama vingi. Lakini yeyote atalayeshinda, ataenda ikulu kusailiwa. Ikulu hatoki mtu pale.
HITIMISHO:
HUU UVHONGANISHI, SOJUI FULANI KAFA, AU KAVHOMWA NDANI, MIMI KAMA RAIA NAAGIZA VYOMBO HUSIKA, WAHALIFU HAO WAKAMATWE, NA KUTIWA HATIANI NA CHOMBO HUSIKA, SIO KUWAPELEKA MAHAKAMANI LA!
TAIFA LETU USWAHILI (ZANZIBAR, SHELISHELI, COMORO, KENYA, SUDANI KUSINI, UGANDA, RUANDA, BURUNDI, ZAIRE n.k) TUKO KWENYE TRANSITION. HAPA NO WAY, NI USAMIA TU -(kaanza na malezi).
Umetupigia kelele na utopolo wako mpaka masikio yameziba!