Pre GE2025 Samia ndio kiongozi pekee wa awamu ya 5 aliyeenda kumjulia hali Tundu Lissu hospitalini lakini shukrani anayopata ni matusi na kumbagua

Pre GE2025 Samia ndio kiongozi pekee wa awamu ya 5 aliyeenda kumjulia hali Tundu Lissu hospitalini lakini shukrani anayopata ni matusi na kumbagua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Samia suluhu Hassan ndio alikuwa Kiongozi pekee wa awamu ya 5 ambae alijitoa muhanga kwenda kumjulia Hali Tundu Lisu hospital Nairobi wakati wengine wakisubiria breaking news.

Lakini Cha ajabu Sasa Shukrani ya bwana Lisu Kwa Samia ni kumtukana,kumsinhizia anauza Mali za Watanganyika na kumfanyia ubaguzi wa kikabila na kimaeneo.

Lisu amejivika kilemba na kuwa champion wa kueneza chuki na ubaguzi Kwa Samia kana kwamba Kuna baya amelifanya.

Ikumbukwe kwamba, Ubinafsishaji wa Bandari sio kuuza na unalenga kudhibiti waliogeuza Bandari ya Dar shamba la bibi.

Ieleweke wazi kwamba Masai hawajafukuzwa Bali wamehamishiwa Kwa staha na fidia kupisha uhifadhi ya Ngorongo ambayo ilishaanza kuharibiwa na Wingi wa watu kinyume na sheria za kuanzishwa kwake.

Ikumbukwe Muungano haukusainiwa na Samia yeye kazi yake ni kuulinda ila Lisu anataka Samia auvunje, haiwezekani.

Ieleweke kwamba Asili za Watu wa Tanzania ni kutoka sehemu tofauti za Dunia ila Lisu anataka Samia ajigeuze abadili historia yake au?

Ieleweke Lisu alikimbia Nchi na Samia huyu huyu anaemtukana ndio amerenesha mazingira sawia ya uhuru wa kujieleza ila Lisu anamtusi.

View: https://twitter.com/PMadeleka/status/1792878597406855471?t=3j4TQ1NiLX56_gebKNSJFg&s=19

My Take
Ni wazi huyu bwana asiye na jema hakupaswa kuhurumiwa,waliojitosa kumsaidia wengine walifutwa kazi na wengine walidharirishwa na kusutwa ila Shukrani yake ni dhihaka.

Bora mfadhili mbuzi utakunywa mchuzi, binadamu hapana.

Pole sana Samia,pole sana Tanzania.

Lisu na chama chake tuwakatae , Mwalimu alionya huu ubaguzi Toka kitambo.

Huwa Ninacheka sana nikiona ccm wanasema kuhusu kueneza chuki, halafu fuatilia wanavyongia madarakani kwa njia za kihayawani, yaani ni chuki za kudumu wanajenga. Kwa maneno marahisi kama umejitoa ufahamu kwa kuona ccm ni sahihi, msamiati wa kueneza chuki uepuke maana haukubebi.
 
Ni beyond that, anadhihaki hata pose ya mama Samia kwenye mabango,
ile kumuita "mama Abduli" repeatedly ni unnecessary, ni kuingiza ishu za familia kwenye siasa
Mbona wanasema pochi la mama husemi wanaingiza ishu za familia na Makonda juzi alisema yeye ndiyo mtoto pekee wa mama huku lalamika, acheni upuuzi, Lisu hajui siasa za kinafisi za kumsema mtu pembeni yeye hupasuka live ili kama una akili timamu ujirekebishe, mfano nipe faida 5 za muungano kwa mtanganyika/bara
 
Huwa Ninacheka sana nikiona ccm wanasema kuhusu kueneza chuki, halafu fuatilia wanavyongia madarakani kwa njia za kihayawani, yaani ni chuki za kudumu wanajenga. Kwa maneno marahisi kama umejitoa ufahamu kwa kuona ccm ni sahihi, msamiati wa kueneza chuki uepuke maana haukubebi.
Zipi hizo? Huwa wanaeneza chuki na ubaguzi?
 
Nyerere hakuwa Mungu.... Tafakari
Ni ujinga kumtukuza marehemu ni kukosa akili, utadhani Nyerere ndiyo anawaza kwa niaba ya watanzania wote, alifanya mazuri kwa wakati wake sasa hayupo lazima tusonge mbele na turekebishe makosa yake.
 
Narukia wapi? Hoja ipi imekosa majibu?

Unadhani pesa ambazo Serikali inaingiza kutoka Zanzibar sio faida ni hasara ya Muungano au?
Kama TRA ipo Zanzibar kwanini kuna ZRA? kwanini ukinunua hata TV kwa matumizi yako toka Zanzibar lazima bandarini ulipe tena?
 
Kama TRA ipo Zanzibar kwanini kuna ZRA? kwanini ukinunua hata TV kwa matumizi yako toka Zanzibar lazima bandarini ulipe tena?
Kama TRA Iko Kila Halmashauri Kwa nini Kuna makusanyo ya ndani ya Halmashauri?

Ukipata zero Civics na huyo Lisu wako si ndio? 😁😁
 
Unauliza au unapigia jibu mstari? Ama umesahau habari za chama Cha wachaga? Upore uchaguzi, ubambikie wapinzani wako kesi, uue hiyo sio chuki bali ni upendo?
Chadema ni absolutely chama Cha kidini Cha Wakristo,angalia hata huko kwenye Uongozi wenu
 
Back
Top Bottom