Mkuu so sasa hivi unaamini nyomi ndiyo wapiga kura? Maana wenzio waan mawazo tofauti na wewe . Ila ije mvua liwake jua Jiwe hashindi uchaguzi huuUwanja wa Samora umefurika na kutapika na hii haijawahi kutokea tangu uwanja huu umejengwa 1976.
Ni kampeni za kihistoria, karibu.
==========
Updates;
MIGORI, IRINGA
LUKUVI: Tunaomba kawilaya, utawala ni mgumu sana. Wasiwe wanawafata wakuugenzi, wakuu wa wilaya kilomita 125. Namuombea kura mheshimiwa Magufuli, mtampa? Namuombea kura diwani, mtampa? Mzee Mungu akubariki sana, sisi tunajua unatupenda sana jimbo la Ismani, tunakukaribisha sana.
MAGUFULI: Nileteeni mheshimiwa Lukuvi ili tufanye nae kazi, angalau kama mnanipenda na mimi imebaki miaka yangu mitano, nimalize na Lukuvi. Amefanya kazi zake vizuri sana katika kipindi kilichopita na nimeshangaa kwanini hakupita bila kupingwa kwa sababu siku za nyuma alikuwa anapita bila kupingwa na mimi kule jimboni kwangu nimewahi kupita bila kupingwa. Mtamleta Lukuvi?
Amenisaidia sana katika kazi, amefanya kazi katika wizara ya Ardhi ambayo mimi mwenyewe nimewahi kuwa waziri wa Ardhi. Tukawezesha vijiji 920 katika nchi hii kuvirudisha katika matumizi ya wananchi badala ya kuwa hifadhi za taifa.
Ingawaje nafahamu, shujaa huwa hapendwi kwao. Hata mti wenye matunda ndio unapigwa mawe lakini umuhimu wa Lukuvi mimi nausema kwa wazi, nileteeni Lukuvi, nileteeni na diwani wa CCM. Matunda yake mtayaona, na mimi naomba kura.
SAMORA, IRINGA
POLEPOLE: Leo hapa Iringa tumekuja na injini mbili za ziada kwa ajili tu ya kuweka mambo sawa. Tuna wana CCM waandamizi, makada waandamizi nitawatambulisha baadae. Sasa wameanza kuweweseka, mahala fulani wanasema, Kassim Majaliwa ni waziri mkuu, kwanini anazunguka?
Nikasema humu tayari, dozi imeingia maana kila anapoenda kuharibu, Rais anamtuma Majaliwa anasafisha. Ndugu Kassim majaliwa ni sehemu ya viongozi wa kitaifa wa chama cha mapinduzi na leo tunayo heshma, tunao wajumbe wengine wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa ambao wamepewa majukumu mahsusi ya kuzunguka kitaifa kupiga kazi njema ya kutafuta kura.
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app