Tunalo tatizo la elimu nchini, hatuna madawati ya kutosha, hatuna waalimu wa kutosha, hatuna vitendea kazi ikiwemo vitabu then yupo mtu amekaa wizarani huko amesoma sanaa na utamaduni anawaza kuidhinisha M420 kwa ajili ya sanamu kweli.
Hii imegeuka kuwa nchi ya sanamu Kama vipaumbele vyetu kweli? Kwamba tumeingia kwenye imani za sanamu kwa mabilioni ya Kodi za wananchi? We can't be serious. Kwamba tunakatwa pesa kwenye vocha na miamala mingine ili hizo fedha zikajenga sanamu?
Kwamba Mkapa 420 milion, sijui Nani mwingine akitutoka 420Milion, Mawaziri wakuu 220 milion, makawa wa Rais tuwajengee sanamu za milioni 300, Mawaziri milioni 150, wakuu wa Mikoa milioni 100, wakuu wa Wilaya 50milion? Ni hivi ndivyo tumejipanga kuiendesha nchi?
Lakini pia hizo fedha mbona hazipo kwenye bajeti ya serikali? Unaweza ukatamani kumpiga mtu rungu la kichwa atambae kwa mambo haya yakijinga unayoyasikia kutoka kwa watu wanaolipwa fedha za umma.
Hakuna anayewaza kuhusu maskini wote wanawaza matumbo yao na Sasa wameanza kuweka na utaratibu wakuhudumiwa hata wanapotwaliwa. Shame shame shame nchi masikini kutumia fedha za umma kwa mambo ya kijinga
Nchi hii kuna "Kakikundi ka watu" wachache sana; kwa ukwasi wa kupindukia walioupita kwa kupora mali za umma, sasa wanaona "Tanzania na vyote vilivyomo" ni mali yao. Huwaambii kitu. Wanaweza wakafanya lolote wanalotaka almradi kuzifurahisha nafsi zao.
Hali hii isiyofaa kwa afya ya Nchi ni lazima idhibitiwe mapema kwa faida ya vizazi vijavyo. Binafsi sioni mantiki ya kumshobokea JPM kiasi hicho ilhali alikuwa anatimiza wajibu wake kama Rais. Hata hivyo, JK wakati wa msiba wa BWM alituweka Watanzania wazi (kama mnakumbuka), bila shaka alikuwa anawajibu waliokuwa wakimpamba saana JPM kana kwamba watangulizi wake wanne, hususani BWM na JK hawakufanya lolote wakati wa awamu zao. JK alisema, Miradi inayoendelea ktk Awamu ya V ni utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa ulioandaliwa na Serikali ya Awamu ya III iliyokuwa chini ya uongozi wa hayati BWM kama Rais. Awamu ya IV chini ya JK ilianza kutekelezwa, Awamu ya V wakapokea kijiti. Sema hayati JPM ni kama alikuwa mtu wa tambo sana! Anyway, ni kuchukuliana kwani kila mtu na alivyozaliwa na haiba yake; wapo sanguine, fragmatic, choleric, etc.
Nchi hii imejipambanua kumtanguliza Mwenyezi Mungu mbele ktk masuala yote. Hii tuliishuhudia wakati wa kupamba moto vita ya UVIKO-19 mwaka 2020. Wakati mataifa mengine ulimwenguni yanahaha kwa kuhenyeshwa na ugonjwa huu hatari, Tanzania tulimtegemea Mwenyezi Mungu, akatuvusha salama. Sasa, chonde chonde tusimuudhi Mzee huyu wa Siku. Ni hatari.
Mwenyezi Mungu anachukia mno mno Sanamu. Sanamu ni chanzo cha Ibada za sanamu. Mwenyezi Mungu muda si mrefu ataanza kugawana utukufu Wake na hayati JPM. Hakubali. Yeye ni Mungu mwenye wivu. Tusimchokoze.
Kama ni kwa kumbukumbu, andikeni historia yake ktk vitabu. Vizazi vyetu vitakuja kuisoma. Tuna somo la Uraia mashuleni. Vijana wafundishwe. Sanamu tena? Tena la bei mbaya hiyo? Tena ktk kipindi hiki ambacho Mheshimiwa Rais SSH amesisitiza tumpatie muda na nafasi anataka kujenga uchumi wa Nchi? Are we serious kweli?
Aah, aah, ujenzi wa sanamu la hayati JPM usitishwe mara moja!