Kwanza kabisa MUNGU alimuumba mwanadamu kwa mfano wake (yani Umungu) , akampa nafasi ya kuchagua kuishi katika mabaya ambao mshahara wake ni motoni na kuishi katika mema ambapo mshahara wake ni mbingu
Motoni haikutengenezwa kwa ajili ya binadamu , motoni ilikuwa ni kwa ajili ya shetani. Adam ndiye aliyesabisha wanadamu kuingia motoni baada ya kuchagua mabaya yaani pale alipodanganywa na shetani ale tunda na afanane na MUNGU , na ikumbukwe shetani (malaika walioasi) nao walifukuzwa mbinguni na kuhukumiwa kwenda motoni kwa sababu ya kutaka kuwa MUNGU na kuupinduwa utawala wa MUNGU
Pili swala la Biblia , Hakuna kitu kwenye Biblia kitafutika , yale yalioandikwa yatatimia .
Na nimeona pia hujui tofauti kati ya MUNGU na Yesu , Yesu ni mwana wa kwanza wa MUNGU , ndiye wa kwanza kuumbwa na MUNGU kabla hajaumba chochote kile kati ya mbingu na malaika . Na Yesu ndiye aliyefanya uumbaji , kwa kupitia nguvu ya MUNGU . Na yeye ndiye Masiha . Na kila goti litapigwa siku ya mwisho kwa sababu MUNGU amemfanya kuwa mfalme
Jina La Yesu , likitajwa Mapepo(Majini) yanapiga kelele za maumivu. Jina La Yesu likitajwa wenye imani wanapona UKIMWI , KISUKARI , KANSA na magonjwa yalioshindikana. HAKUNA JINA LENYE NGUVU KAMA JINA LA YESU