Sapraiziiii: Yanga yamsajili Selemani Mwalimu siku mbili baada ya kunukuliwa akisema ataichezea Simba Msimu wa 2026/27

Sapraiziiii: Yanga yamsajili Selemani Mwalimu siku mbili baada ya kunukuliwa akisema ataichezea Simba Msimu wa 2026/27

Kosa la viongozi ni kumtangaza mchezaji bila kumiliki, Inaonekana kuna wafanya maamuzi pale Simba either siyo smart kabisa, yaani karai au kuna pandikizi moja lipo kwenye nafasi za juu sana za maamuzi.
 
View attachment 3648056

Klabu ya Yanga imetangaza kumsajili mshambiliaji Selemani Mwalimu ambaye msimu uliopita aliichezea Simba kwa mkopo, ikiwa ni siku chache tangu mchezaji huyo anukuliwe katika clip iliyopostiwa na Simba akisema ataendelea kuichezea timu hiyo katika msimu wa 2026/27.

Mwalimu alikuwa akiichezea Simba kwa mkopo akitokea Wydad Athletic Club ya Morocco, baada ya Simba kutangaza kuwa ataendelea kubaki kikosini hapo Wydad ilipinga taarifa hiyo na kumtaka arejee kikosini hapo, akafanya hivyo na sasa Wanasimba hawaamini macho yao imekuwaje kaibukia Yanga.

Yanga bado haijaweka wazi mkataba uliotumika kimsajili kama ni wa mkopo au moja kwa moja.
Mashabiki wenzangu wa simba hii picha ni AI. Msiiamini hata kidogo. Siku ile kwa macho yetu tulishuhudia ile clip. Selemani Mwalimu ni mchezaji wetu halali.

cocastic, Kalpana, Kipenzi Changu, na wengineo naombeni mniunge mkono kwenye jambo hili.
 
KiTanzania Tanzania hii ipo sana ujue. Hivyo wala hupaswi kuumia.

Mmeshasahau mlishatupokonya wachezaji kibao pale Airport. Yaani anakuja kwa lengo la kusajiliwa Yanga mwishowe anatambulishwa Simba.
Lakini hii ni tofauti kidogo. Simba ni kama walikuwa na uhakika wa kuwa na Sulemani. Bora hao ambao hawajulikani na wananyakuliwa airport.
 
Hii ni ishara kwamba simba bado kuna kirusi...

Kuna mtu alitoa taarifa kwa Yanga juu ya mienendo yetu kwa mchezaji(Mwalimu)

Yanga hawajakurupuka.
Usijaribu kumtaja Mwenyekiti Mangungu kama ndiyo kirusi. Huyu tunamlinda kwa wivu mkubwa. Taja akina Matola, Magori, Mo mwenyewe, nk. ndiyo utaeleweka.
 
Hii ni fedheha kwa wana Simba hii ni fedheha kwa mashabiki wote wa Simba.....sio kwa kusajiliwa kwa Mwalimu kwenda Yanga bali kwa kuonesha kuwa viongozi wa Simba wamewafanya mashabiki wa Simba kuwa ni Mazuzu, Mazezeta, MAJINGA MAJINGA yasiyo na akili......

Viongozi wa Simba wamewavua nguo mashabiki na wapenzi wa timu yao.......hii inaonyesha kuwa Simba wanafanya siasa kwenye mpira huku Yanga wakifanya kweli
 
Kosa la viongozi ni kumtangaza mchezaji bila kumiliki, Inaonekana kuna wafanya maamuzi pale Simba either siyo smart kabisa, yaani karai au kuna pandikizi moja lipo kwenye nafasi za juu sana za maamuzi.
Hapana
Haina haja ya kuuma uma maneno viongozi wa Simba wamewafanya mashabiki na wapenzi wao kuwa makatuni......wameongea huku wakijua kuwa sio kweli.....
 
Back
Top Bottom