Sasa hivi kuna pesa kama takataka, tangu tupate uhuru hakuna kipindi watu wanaogolea kwenye pesa kama sasa kipindi cha Samia

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Watu wana pesa jamani.
Kama za majini au za madili Mimi sijui ninachojua ni kwamba watu wana pesa sana.
Yawezekana mifumo ya sasa ni rafiki kwa watafutaji.
Tuombe Mungu asitokee tena mtu kama Magufuli aliyevurugavuruga uchumi wa wananchi na wananchi wakamshangilia.
Siko hapa kumsifia Rais Samia, Mimi sijawahi kumsifia binadamu mwenye pumzi kama Mimi.
 
Kichaa kimekupanda?Hebu tugawie hizo pesa.
 
Hela zipo kwa wenye connection na raia namba 1 iwe chawa au mteule.
 
Inaonekana hukuwahi kuishi katika enzi za Mwinyi wewe
 
Na Kuna Watu hawana pesa hadi wanashindia muhogo mbichi uliopakwa pilipili ya UNGA na chumvi! Kila kukicha afadhali ya jana😭
Sijui ww mwenzetu unazo na za kufurika?
Kama ndio tupe maokoto...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…