Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
- Thread starter
-
- #81
Kabisa mkuu wala haipingwi.....Yaani kushudia mtu katolewa ngeo ilikuwa sio ajabu kabisa huko masokoni/minadani ni ngumi tu yaani hakuna solution bila watu kuzichapa.Nakumbuka miaka Ile ya 1995 pale Coco beach kulikuwa na beach party watu walikuwa wanakesha lkn ikifika SAA 6 Tu unakuta watu wameshachomana visu.
Zamani kipindi tunakua ilikuwa lazima ujifunze ngumi kidogo ili uweze kuishi mtaani,siku kama za Christmas na mwaka mpya watu waliuana Sana kwenye kumbi za starehe
DJ alikuwa ana force wa aweke wimbo huo wimbo ukikosekana kama sio mbabe huyo DJ ndo mwisho wa disco atapigwa achakae au akimbie mazimaHii iliwahi kunikuta japo ni majuzi hapa 2013. Tupo kwenye disko la graduation, nimekunja kidogo suruali kwa chini, mhuni mmoja wa mtaani akaja anataka kunipiga kisa nimekunja tu suruali. Ilibini wanangu waje waniokoe kwenye ile dhahama. Kuna siku napita ubungo pale, nasikia mtu ananiita, kugeuka ni huyo jamaa. Kachoka vibaya mno, ananiomba hela ya fegi...
Dogo kama wewe niwa 2007 haya utayajulia wapi? haya yana watu wake tunajiuliza imekuwaje saivi vanga kama hizi hazipo tenaUnaweza kuta mtu amekaa mahali ametulia na simu ukadhani anafanya mambo ya maana kumbe anaandika mambo ya hovyo kama mleta mada.
Sahihi kabisa kuna muda ulikuwa unafika una siku kama tatu hujapigwa ama kupigana unajiona haupo sawa kabisa inabidi ukanunue ugomvi kwa namna yoyote ile.Kipindi hicho kila mtu alikuwa na mbio yaani akichomoka mbio huwezi mpata ndo basi tenaMtoa mada umeongea ukweli sikuhizi watu wameacha kugombana physically nadhani pia kuelimika kumechangia pia kuzingatia sheria za nchi... zamani ilikuwa shida unakuta mnacheza mpira ukipigwa rafu tu unaacha kucheza unamfuata unamwambia tutoke nje ya uwanja tukazichape kidogo tusiwaharibie wanaotaka kuendelea kucheza..mkienda huko mzichapa ee ukishindwa unanyoosha mikono juu halafu mnaludi kucheza mpira kesho mnakuwa marafiki wa kweli..wakati mwingine ugomvi unawapatanisha.
Sasa mkuu tungeishije unadhani? kwenda shule unatembea km7 ama zaidi kwenda na kurudi 14kila siku una muda mwingine njia za pori ubabe ulikuwa unasaidia pakubwa mnoNdo maana huwa nasema wazee wakae tu kimya bila kuwasema hovyo vijana wa nyakati hizi. Vijana wa zamani ndo wamerithisha kizazi hiki ujinga mwingi sana. Ingawa wanasemwa sana ila vijana wa leo wana akili nyingi kuliko wa zamani.
Mara ya kwanza kuona mwanaume anafanyiwa happh birthday nilikuwa na miaka 24 nilishangaa sana. Siku zote nilijua ni watoto wa kike tena wadogo wadogo wa mjini.unategemea huyu akitoka hapa ndo arushe ngumi huyu?
View attachment 3199829
wengi wa waalimu mbio zilikuwa zinawasaidia sana kipindi hicho.nimewahi shuhudia mwanafunzi akimshushia kipondo ticha siku ya assembly. kisa kilitokea baada ya mwanafunzi wa f.6 kukataa kuadhibiwa sasa yule ticha akawa amekomaa anataka amwadhibu jamaa. weee moto uliwaka sio wa hapa🔥🔥. ticha alikula mbata za kutosha za yule f.6. sasa madogo wa low classes kuona mwalimu anakula mambata wakaingia nao kumshushia kipondo cha maana yule ticha maana walikuwa hawampendi.
uko sawa kengele ya saa4 mapumziko hiyo nusu saa haiwezi isha bila ngumi ni kila siku iendayo kwa mungu lazima ngumi kupelekana kwa mwalimu hadi umpige mtoto wa mwalimuMambo yalikuwa [emoji91] [emoji91]
Kwa kweli hata sisi mambo ya kupigana tumeyakuta yakiwa bado moto, yameeanza kupungua miaka ya 2005 kwenda juu, now no ngumi just peace and love[emoji1][emoji1]
Siku hizi boys are becoming girlish.Wakat huo hadi nilijihis kama tupo china maana kila mmoja lazima ujue kupigana,nilkuwaga mwoga sana lakin kuna huyo mjomba wangu alikuwa anapenda sana kunitest kila nikikutana na wa rika langu mpaka uoga uliniisha
Nakumbuka wakat fulani tukiwa wadogo tukawa tumeenda ukerewe likizo ya mwez wa 12,siku ya sikukuu nilishangaa kuona sentani wababa wazima wamevua mashati wanapigana mpaka wanatoka midamu tena wengi wengi,hakika niliogopa sana nilikuwa sijawah ona kitu kama hicho
Kuna kabila moja la wazinza hawa ndo walikuwa wananichekesha,kwanza hawa jamaa ni wachache afu wakiwa sehemu moja karibia wote wanakuwa kama ndugu maana huwa wanaoana sana,ikitokea kuna mchezo wa mpira wa miguu enzi hzo mpira auishi tena kipindi hicho walikuwa wanacheza watu wazima tena wana familia,basi ghafla utaona wanashikana wachezaji kwa wachezaji mashabiki nao wanaingia mara unaona jamaa anamrukia shemeji yake au wakwe kwa wakwe wanakwidana yaan ni full valangati au mtu na mjomba wake wanazikunja
Haya mambo yameisha baada ya watu kupata mwanga na kuwa na tamaa ya pesa ya kutaka kulipwa unapompiga,ataanzisha kesi na utamlipa kwa kuuza mali zako
Ajabu sana.....ZAMANI ILE ASUBHI ASUBUHI WAKATI WA MCHAKA MCHAKA LAZIMA KIRANJA HATA MMOJA APIGWE. Halafu ili uwe kiranja ubabe ilikuwa sifa ya kwanzaVIJANA WA KILEO HOVYO KABISA UNAKUTA KIJANA KAJAZIAJAZIA MWENYEWE MTANASHATI ANA BONGE LA KIFUA NA MUSTACHI WA NGUVU LAKINI AKITOKEA NYOKA TU HAPO AU PAKA ALIYEPAGAWA ANAKULA KONA.
HUWA NASHANGAA SANA HATA MAJESHI YETU SIJUI WANAPATA WAPI NGUVUKAZI KWA SASA MAANA VIJANA HAWANA UJASIRI KABISA. NDIO MAANA SI AJABU KUSIKIA KIJANA SHABABI WA KIUME AMELAMBWA MAKOFI YA USO NA BINTI KIGORI MKUNANAZI ALIYEMTOLEA MAHALI.
Zamani kulikuwa na ubabe wa hovyo sana. Ili uishi kwa amani ni lazima uwe mtemi au uwe na washkaji ambao ni watemi...DJ alikuwa ana force wa aweke wimbo huo wimbo ukikosekana kama sio mbabe huyo DJ ndo mwisho wa disco atapigwa achakae au akimbie mazima
Kabisa hadi wanatia huruma sasa hivi hata vujana wa kurina asali hawapo kabisa hadi wavae ppe zake ajabuSiku hizi boys are becoming girlish.
Wavulana wanalelewa kikikekike sana. Homones za kiume zinaishia kabisa!!vitoto vya kiume vinaitwa Junior
Umenikumbusha tulikuwa kwenye mkesha wa mwaka mpya mara hali ya hewa ikabadirika ghafla tulivumilia lakini tukashindwa paroko akaagiza aliye rusha hilo yai akamatwe tumpelekee...mayai visa kumbe yalikuwa mengi bana tulipondwa na hatukurudi kanisani tenaKipindi cha mwaka mpya bila kumpiga mtu na yai viza au kugonga mageti ya watu kama ngoma roho inakosa raha kabisa
Sahihi huwezi ukatoka mtaa huu kwenda mtaa mwingine mwenyeweZamani kulikuwa na ubabe wa hovyo sana. Ili uishi kwa amani ni lazima uwe mtemi au uwe na washkaji ambao ni watemi...
Kipindo hicho kila mtu alikuwa mwanariadha ukibahatika kuchomoka ni kama upepo watakuwa wanao shati tu unatokomeaNakumbuka nikiwa mdogo kuna sehemu nilienda kucheza,sasa jamaa wakanichonganisha na jamaa flani
Aisee nilimchapa,baada ya washkaji kuona nimemchapa mwenzao c wakaniungia tela,mda huo sina kampani nipo peke yangu
Na mda huo kufika home ni kama km 3 aisee niliokolewa na miguu yangu
HahhahahahahahaaaaaaaVIJANA WA KILEO HOVYO KABISA UNAKUTA KIJANA KAJAZIAJAZIA MWENYEWE MTANASHATI ANA BONGE LA KIFUA NA MUSTACHI WA NGUVU LAKINI AKITOKEA NYOKA TU HAPO AU PAKA ALIYEPAGAWA ANAKULA KONA.
HUWA NASHANGAA SANA HATA MAJESHI YETU SIJUI WANAPATA WAPI NGUVUKAZI KWA SASA MAANA VIJANA HAWANA UJASIRI KABISA. NDIO MAANA SI AJABU KUSIKIA KIJANA SHABABI WA KIUME AMELAMBWA MAKOFI YA USO NA BINTI KIGORI MKUNANAZI ALIYEMTOLEA MAHALI.