Wakat huo hadi nilijihis kama tupo china maana kila mmoja lazima ujue kupigana,nilkuwaga mwoga sana lakin kuna huyo mjomba wangu alikuwa anapenda sana kunitest kila nikikutana na wa rika langu mpaka uoga uliniisha
Nakumbuka wakat fulani tukiwa wadogo tukawa tumeenda ukerewe likizo ya mwez wa 12,siku ya sikukuu nilishangaa kuona sentani wababa wazima wamevua mashati wanapigana mpaka wanatoka midamu tena wengi wengi,hakika niliogopa sana nilikuwa sijawah ona kitu kama hicho
Kuna kabila moja la wazinza hawa ndo walikuwa wananichekesha,kwanza hawa jamaa ni wachache afu wakiwa sehemu moja karibia wote wanakuwa kama ndugu maana huwa wanaoana sana,ikitokea kuna mchezo wa mpira wa miguu enzi hzo mpira auishi tena kipindi hicho walikuwa wanacheza watu wazima tena wana familia,basi ghafla utaona wanashikana wachezaji kwa wachezaji mashabiki nao wanaingia mara unaona jamaa anamrukia shemeji yake au wakwe kwa wakwe wanakwidana yaan ni full valangati au mtu na mjomba wake wanazikunja
Haya mambo yameisha baada ya watu kupata mwanga na kuwa na tamaa ya pesa ya kutaka kulipwa unapompiga,ataanzisha kesi na utamlipa kwa kuuza mali zako