Sasa imekuwa wazi, kanda ya ziwa ina watanzania asilimia 25 tu

Wewe ndiyo mtupu kabisa. Kasome historia tena. Mkoa wa Kagera haujawahi kuwa pamoja na Mwanza.

Mkoa wa Kagera, toka mwaka 1964 mpaka 1984 ulikuwa ukijulikana Jimbo la Ziwa Magharibi. Na makao makuu ya mkoa huu yalikuwa mjini Bukoba.

Mkoa wa Mwanza ulikuwa ukiitwa Jbo la Ziwani ambao ulikuwa ukijumuisha Shinyanga, Mara, Geita na Simiyu (kwa sasa).

Tabora ilijulikana kama jimbo la Magharibi.

Kujielemisha zaidi, soma hapa: Mikoa ya Tanzania - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Mi ndio nikufundishe labda jamii za kanda ya ziwa,usiangalie mipaka ya kijiografia,buseresere,bwanga,chato,muganza,buziku zote zilikuwa mkoa wa kagera,hayo maeneo yana makabila mchanganyuko,wahaya,wasubi,washubi,waangaza,waha,warundi,wasumbwa,warongo,wazinza,wasukuma ets,mzinza sio msukuma,mzinza ni jamii ya mkerewe,au msubi au mhayq,mipaka ya kijiografia isikuchanganye
 
Kwa hiyo muhaya na msukuma wanatamaduni sawa,acha siada dogo
Kwataarifa yako mtemi wa kwanza wa bujash,busumagui,nyashimo mpaka dutwa(simiyu na Mwanza) alikuwa muha kutoka kigoma na mpaka leo kizazi chake ndo kinatawala.
 
Ubabe kwenye nini sasa?
 
M Mpina 2025✅✅✅✅
 
Wewe unaongelea Kanda ya Zuwa kama vile ipo ahera. Naifahamu sana, na nimepita mpaka huko vijijini, pengine hata zaidi yako wewe. Kule Musoma, niulize kuanzia Majita mpaka kule Mrito mpaka Kibaso.

Shinyanga, niulize kuanzia kule Ushetu, Mega, Msalala, mpaka Masabi.

Simiyu, niulize kuanzia Gamboshi mpaka Kinamweri.

Kule Geita, niulize kuanzia Masumbwe m Nzera, mpaka Chato.

Kagera, niulize kuanzia kule Kabanga mpaka Kaitaba.

Tabora, niulize kuanzia kule Ulyankulu, Choma mpaka Bukene.

Nimetaja maeneo ya vijijini tu ili ufahamu kuwa nayaelewa hayo maeneo kuliko unavyodhania. Na kisukuma hunifichi neno.

Swali: Kiswahili unakifahamu
Msukumu: Ukuteleleja duhu
Ebu Elezea: Anakuja nanolaga duhu.
 
Halafu watu wa Kagera na hiyo mikoa mingine ni kulia na kushoto.
 
Tabora haipo Kanda ya kati ni magharibi lakini kwa muktadha wa Kura huwekwa Kanda ya ziwa kwa kuwa lugha,utamaduni,mentality na wasukuma havipishani sana

Tumeanza kuwaiga kenya? Kupiga kura kwa misingi ya ukabila?. Kanda ya ziwa huwa haipigi kura kwa pamoja. Ni mkoa wa Simiyu na Geita pekee ndio ngome za CCM kwa asilimia 100. Lakini Mwanza, Mara na kagera Ni 60 kwa CCM na 40 kwa upinzani. Hasa mkoa wa Mara huwa ni 50 kwa CCM na 50 kwa upinzani CHADEMA.
 
Ongezaea:-
1. Katavi
2. Simiyu
3. Kigoma
4. Tabora
 
Kigoma na Kagera zina tofauti kubwa sana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa.
 
Mwanza ni ngome ya CCM mzee acha maneno kisa Wenje kupata ubunge.
 

Acha kupotosha, Kanda ya ziwa Ni mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Simiyu na kagera. Shinyanga ipo kanda ya magharibi.
 
Msome vizuri mleta mada. Ameongelea kanda ya Ziwa. Tabora ipo Kanda ya Kati, Kigoma ipo Kanda ya Magharibi.
Hapana...

Tabora ni kanda ya Magharibi yenye mikoa mitatu tu; Tabora yenyewe, Kigoma & Katavi (kama sijakosea)

Kanda ya Kati ni Dodoma, Singida (na nafikiri) na Manyara..

Kanda ya Ziwa Victoria ofkoz ni mikoa yote inayozunguka ziwa Victoria ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Geita na miwili ya nje kidogo kwa maana ya Simiyu & Shinyanga

NB:
✓ Kanda hata hivyo, kila mtu hutumia vigezo vyake kuzigawa kwa namna aonavyo yeye....

✓ Mathalani CHADEMA, wana vigezo vyao walivyotumia kugawa kanda za kichama kwa chama chao na hawafuati geographical factors...
 
Acha kupotosha, Kanda ya ziwa Ni mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Simiyu na kagera. Shinyanga ipo kanda ya magharibi.
[emoji12][emoji12][emoji28][emoji28]we unachekesha aisee ..toka Lini shinyanga Iko Kanda ya magharibi...kwanza Kanda ya magharibi haipo official......tabora na kigoma wanapata huduma zao za kikanda mwanza ...nzega na igunga hiz wilaya ni Kanda ya ziwa 90 percent kutokana na sukuma culture na ukaribu wake na shinyanga....
Kigoma wanapata huduma zao za kiafya ,na kifedha Kanda ya ziwa . mwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…