Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Ukiacha kovu lake rais SSH (na wana ccm wote waliochaguliwa) lililotokana na wizi wa uchaguzi wa mwaka 2020 uliowaingiza madarakani, ameonyesha siasa nzuri bado inawezekana Tanzania. Anakwenda polepole na wapinzani, anawaachia wafungwa walioonewa, anafuta kesi zisizo maslahi kwa Taifa, kwenda ki international zaidi, kupenda haki kwa ujumla, ku act decisively ikibidi, kutoogopa kutenda akiamini ndio stahiki, kufutilia mbali ukanda na udini kwa kufanya teuzi zenye sura ya Taifa zaidi nk nk. Japo unaweza kusema ni mapema ku judge, binafsi namuona raisi na uraisi wake mzuri. Kasoro zinazotajwa ni za kibinadamu tu. Hatutapata rais malalaika hata hivyo. Ataacha legacy nzuri sana akiendelea hivi. Hongera mama.
 
Hatutaki Utwana!

Ni kweli katika Karne hizi za karibuni kuona Utwana, ni "Nadra' sana kuona siasa zenye kujikita kwenye Utwana.

Asiturudishe huko.

Kwa mtazamo wangu, hatoweza kutoboa kama Mwanasiasa wa Aina yeyote Afrika.

Aluta Continua.
 
naunga mkono.
kazi kubwa na yenye akili ya hali ya juu sana
 
SIASA SAFI ASINGEENDELEA KUWAKUMBATIA WABUNGE 19 WALIOGUSHI KUINGIA BUNGENI HUKU AKIJUA KILICHOTENDEKA


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja.

# Samia mbele kwa mbele
 
Mama anaamini ushindi wa maana si kushinda tu ili mradi kushinda, bali ni kushinda kwenye chaguzi huru na haki.
Mbona alishawahi kunukuliwa na Media akisema kuwa hata Wapinzani wakishinda ni CCM ndio itakayotangazwa🤔 au kuna akina Samia wawili wanaituongoza?

Au mimi ndio sijaelewa? au ni Mirungi ndio imependa kichwani?
 
Ni Mtazamo wako tu
 
Mbona alishawahi kunukuliwa na Media akisema kuwa hata Wapinzani wakishinda ni CCM ndio itakayotangazwa🤔 au kuna akina Samia wawili wanaituongoza?

Au mimi ndio sijaelewa? au ni Mirungi ndio imependa kichwani?
Mkuu mleta mada baada ya kushiba urojo kaamua kuwa mchambuzi wa siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…