MASHANJARA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 379
- 500
Ukiacha kovu lake rais SSH (na wana ccm wote waliochaguliwa) lililotokana na wizi wa uchaguzi wa mwaka 2020 uliowaingiza madarakani, ameonyesha siasa nzuri bado inawezekana Tanzania. Anakwenda polepole na wapinzani, anawaachia wafungwa walioonewa, anafuta kesi zisizo maslahi kwa Taifa, kwenda ki international zaidi, kupenda haki kwa ujumla, ku act decisively ikibidi, kutoogopa kutenda akiamini ndio stahiki, kufutilia mbali ukanda na udini kwa kufanya teuzi zenye sura ya Taifa zaidi nk nk. Japo unaweza kusema ni mapema ku judge, binafsi namuona raisi na uraisi wake mzuri. Kasoro zinazotajwa ni za kibinadamu tu. Hatutapata rais malalaika hata hivyo. Ataacha legacy nzuri sana akiendelea hivi. Hongera mama.