Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
Rais Mama Samia ni mtu anayeamini kwenye siasa za ushawishi badala ya kutumia maguvu ‘Unnecessarily’.

Ni mtu anayeamini kwenye utu na muadilifu kweli kweli. Falsafa yake hii, humfanya asiwe anaangalia tu matokeo ya mwisho ya michakato, bali pia uhalali wa michakato yenyewe na kutumia busara ya hali ya juu ili kupunguza madhara na kuongeza tija (Ikumbukwe kila kitu kina pros na cons zake, kwa hiyo kiongozi tunampima kwa kuangalia ana maximize upande upi).

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya amekuwa mfano bora wa siasa za namna hii kwa miaka ya hivi karibuni na kuwa role model wa EAC kama sio Afrika nzima.

Hata hivyo sasa rekodi yake inavunjwa na mama kwa kuonesha viwango vya juu sana vya siasa za kistaarabu na kisasa.

Inaendelea...
 
Kwa mfano, ukiangalia aina ya siasa aliyochugua kufanya pengine kutokana na uadilifu wake, Mama anaamini ushindi wa maana si kushinda tu ili mradi kushinda, bali ni kushinda kwenye chaguzi huru na haki.

Hili linajidhihirisha kwenye ‘reforms’ anazofanya sasa kwa kutengeneza mazingira Rafiki ya kila mtu kufanya sias na kuwa na mijadala ya hoja (constructive criticism). Ndio Maana tunasema anaamini kwenye siasa za kisayansi na sio siasa za kihuni ambazo wakati Fulani zimekuwa zikitetewa na baadhi ya watu wasiojielewa.

Inaendelea.....................
 
Ujue wakati wa chaguzi au kuelekea chaguzi; kuna saikolojia za aina mbili kuhusu ushindi kwenye siasa.

Saikolojia ya kwanza ni ya wale wanaoamini kwenye kushinda kwa namna yoyote ile. Yaani hawa wao, kwao la muhimu ni kushinda, uhalili wan jia zilizotumika, wahanga na hasara zilizo au zitakazojitokeza kutokana na na michakato n.k kwao sio muhimu. Mara nyingi hawa hawaoni shida kudhulumu au kufanya chochote kizuri au kibaya ili kushinda kisiasa. Kwa bahati mbaya wenye saikolojia hii, mara nyingi uwezekano wa kushinda ni mkubwa na wanashinda kwa 100%, lakini wanakuwa hawana furaha kwa sababu ya makandokando yanayoambatana na mchakato.

Aidha, Kundi la pili ni wale wanaoamini kuwa raha ya ushindi ni kushinda kwa njia za haki, halali , zinazokubalika na kila mtu aone kabisa haki ilivyotendeka huku ukipunguza au kuepuka kuumiza au kuzalisha wahanga bila ulazima wa kufanya hivyo.

Kwa uadilifu na matendo yake, kwa kujiamini tunweza kusema Rais mama Samia anaamini kwenye ushindi na mafanikio ya kisiasa yanayopatikana kwa njia za haki na ndio maana anafanya siasa za ushawishi na kufanya mambo ya maana yanayokubalika katika ulimwengu wa kistaarabu ili hata kama ukitokea/ukifika uchaguzi ashinde kwenye uchaguzi huru na haki na kila mtu awe shahidi kuwa haki imetendeka.

Inaendelea.........................
 
Ni Kwa nini sasa, wanasiasa wenye akili na waadilifu huchagua aina hii ya siasa ya kistaarabu ya kujenga ushawishi kwa hoja na matendo badala ya kuchagua ile siasa ya dhuluma, kulazimishia mambo, uongo uongo na ulaghai ambayo mara nyingi inapendelewa sana na watu madhalimu, wabnafsi na wenye ufinyu wa maarifa?

Zipo sababu nyingi za kitaalamu ila hapa tutaeleza tano tun a kuzioanisha na mazingira ya Tanzania.

1. Ushindi mzuri ni ule unaopatikana kwa haki, ukishinda kwa haki una feel ushindi wako na unakuwa na raha ya ndani. Kwa kuwa duniani tunatafuta raha, sasa ni nini tena Mungu akupe?.Aidha, kwa mazingira ya Tanzania, CCM inao uwezo wa kushinda vizuri tu kwenye uchaguzi huru na haki kwa kuwa bado ndio chama bora Zaidi ukilinganisha na vingine vilivyopo (Japo hawatashinda kwa 100% ambapo pia hawana sababu ya kushinda kwa 100%)

Inaendelea..............
 
2. Raha ya ushindi uwe unashindana na watu ambao mna nguvu zenye uwiano (watu wazima wenzako). Kwa mfano simba ikifunga yanga kuna kuwa na raha kuliko ikifunga ka -timu dhoofu li- hali. Hata wewe ukikimbizana na mkimbiaji professional na ukamshinda ina raha tofauti na ukimshinda mlemavu wa miguu. Ukifanya interview na PhD na ukamshinda ina raha kuliko ukifanya interview na mtoto wa darasa la 4 na ukamshinda.

Kwa kuwa vyama vya upinzani Tanzania vimekuwa dhoofu li-hali kwa muda sasa kwa sababu mbalimbali, ndio maana anajaribu anagalau kuviwekea mazingira Rafiki ya kukua ili hata ataaposhindana ashindane na kuwashinda watu wazima wenzake.

Inaendelea.................
 
3. Mfumo wa siasa za Tanzania ni wa ‘simple majority’, kwa hiyo hakuna ulazima wowote wa CCM kushinda kwa 100% Ushindi wa 70% unaopatikana kwa njia huru, wazi na haki unatosha sana.Kumbuka unapaswa kuwa na kura 1 tu ya ziada kutangazwa mshindi.

Aidha, raha ya ushindi kwenye mechi, ni kushinda kwa bao chache tamu. Fikiria wewe unapiga bao 10, mwenzako ‘O’ inakuwa haina utamu, utamu 2 kwa 1 au 3-1.

Inaendelea.................
 
Siasa safi ni kuwafanya wananchi wapate mkate wao na maisha yanayotabirika

Siasa ya kuwafanya wananchi wawe na njaa, haijawahi kupendwa na mtu hata mmoja

Labda huko juu keki inakoanzia!

Kama hayo mnayosema ni kweli kwanini analeta janja janja na kuunda genge la kuhalalisha kuchelewasha katiba mpya mpaka baada ya yeye kuiba uchaguzi 2025? Kama kweli ana nia nzuri tupate Katiba mpya mapema ili ikifika 2025 kutakuwa na level playing field!!
Hayo mazungumzo na Chadema ni danganya Mbowe tu lakini hayana nia njema kwa nchi.
 
4. Kuwepo kwa vyama vya ushindani vinavyoweza kui challenge CCM ni faida kwa CCM wenyewe kwa kuwa huipa hamasa CCM yenyewe kufanya vizuri Zaidi. Kwa kawaida ukiwa na mtu anayekukimbiza nawe lazima uongeze spidi, ila kama kila ukigeuka nyuma hamna mtu anayekufuata, utaacha kukimbia na kuanza kutembea na hivyo kuchelea kufika.

CCM yenye spidi kubwa itapatikana kwa kuwa na watu wenye mbio wanaoikimbiza.

Inaendelea...............
 
Azizi Mussa ,

..mtoa mada umetudharau wasomaji wako.

..hivi kweli unaweza kulinganisha uvumilivu na ustaarabu wa Uhuru Kenyatta na ukasema amezidiwa na Samia Suluhu?

..umesahau jinsi Samia Suluhu alivyomshambulia na kumfukuza kazi Spika Job Ndugai kwasababu wametofautiana kimtizamo?

..Je, Samia Suluhu angeweza kumvumilia Makamu wa Rais kama William Ruto kama alivyofanya Uhuru Kenyatta.

..Juzi viongozi wa Bavicha wamekamatwa huko Manyara kwasababu ya kukusanyika ktk kijiwe cha kahawa halafu unasema Tanzania tunafanya siasa za usawa na ustaarabu?!
 
5. Nchi ni yetu sote, so pamoja na ukweli kuwa CCM itaendelea kuongoza kwa miaka mingine mingi; ni muhimu haki za wachache pia zilindwe maana nao ni watanzania wenzetu na wote tuna mchango Fulani kwa maendeleo ya nchi huku tukiwa na haki na wajibu.

Ndio maana tunaona Mama anakazana kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya shughuli za siasa kwa vyama vyote, anajitahidi kuimarisha mifumo ya haki na wakati huo huo anajitahidi kufanya mambo mengi mazuri kiuchumi, kisiasa na kijamii ambayo yanamsaidia kujenga ushawishi chanya siku hadi siku.

Kwa ujumla siasa inayofanyika sasa ni siasa ya kiwango cha hali ya juu sana ambayo ni nadra sana kuonekana kwenye nchi za kiafrika.
 
Azizi Mussa ,

..mtoa mada umetudharau wasomaji wako.

..hivi kweli unaweza kulinganisha uvumilivu na ustaarabu wa Uhuru Kenyatta na ukasema amezidiwa na Samia Suluhu?

..umesahau jinsi Samia Suluhu alivyomshambulia na kumfukuza kazi Spika Job Ndugai kwasababu wametofautiana kimtizamo?

..Je, Samia Suluhu angeweza kumvumilia Makamu wa Rais kama William Ruto kama alivyofanya Uhuru Kenyatta.

..Juzi viongozi wa Bavicha wamekamatwa huko Manyara kwasababu ya kukusanyika ktk kijiwe cha kahawa halafu unasema Tanzania tunafanya siasa za usawa na ustaarabu?!
Mkuu JokaKuu , Mama hakufukuza mtu kwa kutofautiana mitizamo. Na yeye alieleza mtizamo wake kuhusu mikopo na hayo ndio mapambano ya hoja. Aliyekuwa spika akajikuta anajichanganya na kushindwa kusimamia hoja yake. Mwisho baada ya kuyumba yumba akaona ajiuzulu. Ukisema alifukuzwa sio kweli.

Kuhusu watu kukamatwa, jamani sio kila kitendo kinachofanyika wafanyaji wanakuwa wametumwa na Rais, au Rais anakuwa anakifurahia. mambo mengine ni mitizamo, uelewa na tabia binafsi za mfanyaji. Kumlaumu rais ni kumuonea bure. Kama angeagiza au kutoka hadharani na kuunga mkono vitu vizivyo vya kawaida, hilo lingekuwa jambo jingine.
 
Siasa safi ni kuwafanya wananchi wapate mkate wao na maisha yanayotabirika

Siasa ya kuwafanya wananchi wawe na njaa, haijawahi kupendwa na mtu hata mmoja

Labda huko juu keki inakoanzia!
Mkuu, Kwa hiyo wewe ungekuwa ndio rais, ungezungukia kila mtu ukimpa mkate na chai, ikibidi na kuwalisha?

Kazi ya kiongozi/serikali ni kutengeneza mazingira rafiki ya kila mtu kufanikiwa na ni jukumu la kila mtu sasa kutumia fursa zilizopo kutafuta mkate wake. Kufikiri serikali inatakiwa kukuletea mkate ni kukosa uelewa sahihi.
 
Kama hayo mnayosema ni kweli kwanini analeta janja janja na kuunda genge la kuhalalisha kuchelewasha katiba mpya mpaka baada ya yeye kuiba uchaguzi 2025? Kama kweli ana nia nzuri tupate Katiba mpya mapema ili ikifika 2025 kutakuwa na level playing field!!
Hayo mazungumzo na Chadema ni danganya Mbowe tu lakini hayana nia njema kwa nchi.
Kwenye suala la katiba, ishu sio ku kimbia spidi kubwa, bali quality na proper process. Tulisha jaribu kukimbia mwaka 2014 na mbio za sakafuni zikaishia ukingoni.
 
Rais Mama Samia ni mtu anayeamini kwenye siasa za ushawishi badala ya kutumia maguvu ‘Unnecessarily’.

Ni mtu anayeamini kwenye utu na muadilifu kweli kweli. Falsafa yake hii, humfanya asiwe anaangalia tu matokeo ya mwisho ya michakato, bali pia uhalali wa michakato yenyewe na kutumia busara ya hali ya juu ili kupunguza madhara na kuongeza tija (Ikumbukwe kila kitu kina pros na cons zake, kwa hiyo kiongozi tunampima kwa kuangalia ana maximize upande upi).

Rais Uhuru Kenyetta wa Kenya amekuwa mfano bora wa siasa za namna hii kwa miaka ya hivi karibuni na kuwa role model wa EAC kama sio Afrika nzima.

Hata hivyo sasa rekodi yake inavunjwa na mama kwa kuonesha viwango vya juu sana vya siasa za kistaarabu na kisasa.

Inaendelea...
Nenda Malawi kwa Polepole ukajionee mwenyewe.
 
Kwenye suala la katiba, ishu sio ku kimbia spidi kubwa, bali quality na proper process. Tulisha jaribu kukimbia mwaka 2014 na mbio za sakafuni zikaishia ukingoni.

Hizo mbio unasema ziliishia ukingoni ni kwasababu ya huyo Kikwete ambae ndio anamshauri vibaya Samaia kuwa acheleweshe katiba mpaka baada ya 2025!!! Kikwete alihujumu ile rasimu ya Warioba kwavile it was against his personal interests and that of his gang as against the interests of the rest of the population!! Hivyo hiyo hoja kuwa Katiba iligonga ukuta si kweli; hizo ni porojo za Kikwete na genge lake la mafisadi wenzie!! Samia jukumu lake kubwa kuliko yote ni kuwapa wananchi katiba period ; hayo mambo ya kufungua uchumi yatakuwa rahisi zaidi iwapo yatapata baraka na kukubalika na wananchi wengi!!
 
Back
Top Bottom