Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Sasa tunaweza kukubaliana kuwa; aina ya siasa anayoifanya Rais Samia ni ya kiwango cha juu sana ambapo ni nadra sana kuiona Afrika

Nguvu kubwaa Sana inatumika ila ukweli HAKUBALIKI HATA
Huwa kwa kawaida watu wema hawakubaliki mbele ya watu madhalimu, ndivyo ilivyo. Mfano mtu anataka kudhulumu halafu wewe utokee unataka kusimamia haki, unatarajia mtu huyo akukubali?
 
Hizo mbio unasema ziliishia ukingoni ni kwasababu ya huyo Kikwete ambae ndio anamshauri vibaya Samaia kuwa acheleweshe katiba mpaka baada ya 2025!!!
Mkuu, Mzee Kikwete ndiye aliyeanzisha mchakato wa Katiba mpya huku akisisitiza kuwa angetamani ipatikane kabla hajamaliza muda wake. Sasa hakuwa na sababu ya kuanzisha mchakato kisha aukwamishe mwenyewe , kwakuwa kufanya hivyo ni sawa na kujenga nyumba ili uibomoe wakati una uwezo wa kutoijenga kabisa.
 
Uhuru Kenyata kaiga uvumilivu huo toka kwa Jakaya Kikwete

Jakaya alivumilia Kashkash za kina Lowassa ikiwemo kuwavumulia kina Sofia Simba waliofikia hatua ya kutoka hadharan na kupinga Msimamo wa Mwenyekiti wake wa Taifa na Rais wa Jamhuri kwny mchakato wa uchaguzi 2015

Jakaya aliwavumilia kina Samweli Sitta kwny U Spika pamoja na vurugu zake zote alizima Jaribio la Mzee Yusuph Makamba la kumnyang'anya Kadi ya Chama 2009

pamoja na fitna zote na vijembe vya kina Warioba na Butiku aliwapa fursa ya kihistoria ya kuwa kwny Tume ya Kuandaa Rasimu ya Katiba akamuacha Prof Isaa Shivji aliekuwa pendekezo la mfumo wakati huo

pamoja na 'utoto wote' wa kina Chadema bado aliwavumilia

aliwavumilia Wahafidhina wa Kisiwandui waliopinga kwa nguvu zote CCM kuteua Rais kutokea Pemba (Dr Shein)

bado alivumilia vitimbi vya wahafidhina waliopinga kuundwa kwa Serikali ya mseto visiwani
Azizi Mussa ,

..mtoa mada umetudharau wasomaji wako.

..hivi kweli unaweza kulinganisha uvumilivu na ustaarabu wa Uhuru Kenyatta na ukasema amezidiwa na Samia Suluhu?

..umesahau jinsi Samia Suluhu alivyomshambulia na kumfukuza kazi Spika Job Ndugai kwasababu wametofautiana kimtizamo?

..Je, Samia Suluhu angeweza kumvumilia Makamu wa Rais kama William Ruto kama alivyofanya Uhuru Kenyatta.

..Juzi viongozi wa Bavicha wamekamatwa huko Manyara kwasababu ya kukusanyika ktk kijiwe cha kahawa halafu unasema Tanzania tunafanya siasa za usawa na ustaarabu?!
 
Nakubaliana na wewe mkuu. Umesema kweli tupu.
 
Siasa safi ni kuwafanya wananchi wapate mkate wao na maisha yanayotabirika

Siasa ya kuwafanya wananchi wawe na njaa, haijawahi kupendwa na mtu hata mmoja

Labda huko juu keki inakoanzia!
Mama anajitahidi sana ndugu. Ukitaka kujua mama anajitahidi nenda Uganda, Burundi na Rwanda utajua maisha yako juu kiasi gani. Rwanda Kagame kawazip watu wake midomo wooote kuanzia mtoto anayezaliwa mpaka mzee wa 90s. Pale hakuna mtu anayetaja jina la Kagame kama sio kusifia. Otherwise utajua hujui tena hujui sana. Hata bei pale hutakiwa kuuliza we ni kulipa na kutembea.
 
Mkuu, Mzee Kikwete ndiye aliyeanzisha mchakato wa Katiba mpya huku akisisitiza kuwa angetamani ipatikane kabla hajamaliza muda wake. Sasa hakuwa na sababu ya kuanzisha mchakato kisha aukwamishe mwenyewe , kwakuwa kufanya hivyo ni sawa na kujenga nyumba ili uibomoe wakati una uwezo wa kutoijenga kabisa.

Kikwete kwa hulka yake ni mvivu wa kusoma wala usiniulize nimejuaje; hivyo wakati ile rasimu inakamilishwa kulikuwa na vipengele mle ndani kuhusu GOOD GOVERNANCE alikuwa hajavisoma ambavyo kama vingepitishwa angeweza kuwajibishwa!!! Baada ya kushtushwa kuwa kuna vile vipengele ndio akaiweka rasimu kwapani na kutoa visingizio vingi visivyo na maana mpaka akamaliza muda wake!! Hana Sababu yoyote ya maana ya kuendelea kuikalia ile rasimu ya Warioba baada ya kupoteza mabillioni kuitayarisha.
 
Mama anajitahidi sana ndugu. Ukitaka kujua mama anajitahidi nenda Uganda, Burundi na Rwanda utajua maisha yako juu kiasi gani. Rwanda Kagame kawazip watu wake midomo wooote kuanzia mtoto anayezaliwa mpaka mzee wa 90s. Pale hakuna mtu anayetaja jina la Kagame kama sio kusifia. Otherwise utajua hujui tena hujui sana. Hata bei pale hutakiwa kuuliza we ni kulipa na kutembea.
Mkuu ni kweli vitu kupanda bei ni tatizo. Lakini tunachotakiwa kujiuliza ni kwa nini vinapanda, na nani ana uwezo wa kuzuia upandaji huo na kivipi? lakini kuna wenzangu na mie wazee wa kulaumu, basi wanalaumu yoyote kwa chochote, hapo wanajisikia ka 'raha' flani hivi moyoni hahahahah.
 
Kabisa ndugu, hii kupanda bei ya vitu waangalie kwanza chanzo ni nini? Na je ni Tanzania tu? Mafuta kwa Tanzania yako unafuu kulingana na wenzetu maana hata yanapatikana ila lawama ndo kila siku kwa mama. Pia bei ya mafuta ya kula ilianza kupanda sana kipindi cha Hayati Magufuli mpaka yakaadimika baada ya kuongeza kodi kwa waagizaji. Lakini kwasababu mama yupo wanamtupia lawama. Ila ndo hivyo ukubwa jalala.
 
Ufisadi Unashamiri
Utengano(ubaguzi) wa jamii Rich and Poor gap unaongezeka.
Mwananchi hawezi kujiamlia.
Badala ya kuunganisha nchi sasa Ukabila unanyemelea, Udini unarindima.n.k
Badala ya kuwezesha wananchi, mnawezesha wawekezaji uchwara.

Kuimba muimbe. Msimdanganye kuwa ustawi wa Jamii na Taifa utaletwa na wawekezaji kutoka nje.
Msimdanganye ustaarabu na demokrasia zenye mila na desturi za kiarabu na kizungu zitaleta afueni kwa mwananchi.

Awe anachagulika 2025 na sio kutusokomezea CCM na vibaraka wake wanaoshindwa kila siku
kupunguza makali ya maisha
na kutuongezea madeni.

Kura itaamua.
 
Ujue wakati wa chaguzi au kuelekea chaguzi; kuna saikolojia za aina mbili kuhusu ushindi kwenye siasa.

Saikolojia ya kwanza ni ya wale wanaoamini kwenye kushinda kwa namna yoyote ile. Yaani hawa wao, kwao la muhimu ni kushinda, uhalili wan jia zilizotumika, wahanga na hasara zilizo au zitakazojitokeza kutokana na na michakato n.k kwao sio muhimu. Mara nyingi hawa hawaoni shida kudhulumu au kufanya chochote kizuri au kibaya ili kushinda kisiasa. Kwa bahati mbaya wenye saikolojia hii, mara nyingi uwezekano wa kushinda ni mkubwa na wanashinda kwa 100%, lakini wanakuwa hawana furaha kwa sababu ya makandokando yanayoambatana na mchakato.

Aidha, Kundi la pili ni wale wanaoamini kuwa raha ya ushindi ni kushinda kwa njia za haki, halali , zinazokubalika na kila mtu aone kabisa haki ilivyotendeka huku ukipunguza au kuepuka kuumiza au kuzalisha wahanga bila ulazima wa kufanya hivyo.

Kwa uadilifu na matendo yake, kwa kujiamini tunweza kusema Rais mama Samia anaamini kwenye ushindi na mafanikio ya kisiasa yanayopatikana kwa njia za haki na ndio maana anafanya siasa za ushawishi na kufanya mambo ya maana yanayokubalika katika ulimwengu wa kistaarabu ili hata kama ukitokea/ukifika uchaguzi ashinde kwenye uchaguzi huru na haki na kila mtu awe shahidi kuwa haki imetendeka.

Inaendelea.........................

Kwa taarifa yako huyu mama unamuona mstaarabu maana hajakutana na ushindani wa kisiasa, wala uchaguzi wowote. Kama angekuwa na ustaarabu huo unaompamba nao, asingeendelea na katazo haramu la vyama vingine kufanya siasa kwa uhuru. Leo hii upinzani wakianza kufanya siasa na akaona kabisa anaingia kwenye ushindani halisi, lazima rangi yake halisi itaonekana. Kwa mtu asiyejua lolote ndio unaweza kumlisha hii Hadaa.
 
Azizi Mussa ,

..mtoa mada umetudharau wasomaji wako.

..hivi kweli unaweza kulinganisha uvumilivu na ustaarabu wa Uhuru Kenyatta na ukasema amezidiwa na Samia Suluhu?

..umesahau jinsi Samia Suluhu alivyomshambulia na kumfukuza kazi Spika Job Ndugai kwasababu wametofautiana kimtizamo?

..Je, Samia Suluhu angeweza kumvumilia Makamu wa Rais kama William Ruto kama alivyofanya Uhuru Kenyatta.

..Juzi viongozi wa Bavicha wamekamatwa huko Manyara kwasababu ya kukusanyika ktk kijiwe cha kahawa halafu unasema Tanzania tunafanya siasa za usawa na ustaarabu?!

Nakubaliana na wewe kuwa kumlinganisha Uhuru Kenyatta na Samia kuhusu uvumilivu is a tall order!! Samia uteuzi wa wasaidizi wake unaongozwa na jinsia , Dini na kama ni wa Bara au Visiwani!! Najua hili mtabisha sana lakini ukweli ni huo!! Uhuru Kenyatta is on record kuwa yeye uteuzi wa wasaidizi wake ungeongozwa na weledi na Sio ukabila dini wala jinsia ; akifuata nyayo za marehemu baba yake ambaye wasaidizi wake wore walikuwa Graduates na mchanganyiko wa makabila wakati huo!!
 
Kama hayo mnayosema ni kweli kwanini analeta janja janja na kuunda genge la kuhalalisha kuchelewasha katiba mpya mpaka baada ya yeye kuiba uchaguzi 2025? Kama kweli ana nia nzuri tupate Katiba mpya mapema ili ikifika 2025 kutakuwa na level playing field!!
Hayo mazungumzo na Chadema ni danganya Mbowe tu lakini hayana nia njema kwa nchi.

Kabisa, yale mazungumzo ya Mbowe ikulu ni kupotezeana muda na kutoa credit za bure kwa serikali iliyoko madarakani kwa shuruti.
 
Azizi Mussa ,

..mtoa mada umetudharau wasomaji wako.

..hivi kweli unaweza kulinganisha uvumilivu na ustaarabu wa Uhuru Kenyatta na ukasema amezidiwa na Samia Suluhu?

..umesahau jinsi Samia Suluhu alivyomshambulia na kumfukuza kazi Spika Job Ndugai kwasababu wametofautiana kimtizamo?

..Je, Samia Suluhu angeweza kumvumilia Makamu wa Rais kama William Ruto kama alivyofanya Uhuru Kenyatta.

..Juzi viongozi wa Bavicha wamekamatwa huko Manyara kwasababu ya kukusanyika ktk kijiwe cha kahawa halafu unasema Tanzania tunafanya siasa za usawa na ustaarabu?!
Bila kusahau aliyemuweka Mbowe ndani
 
Yaani tumekuwa na tabia ya kuwa Wazalendo kwa Watawala na si kwa Nchi...

Haka kaugonjwa ni mwanzo wa kutokuwa na fikra pevu na kuwa watazamaji na si wachezaji, washangiliaji na si wakosoaji...

The Future is Scary...
 
Kwa taarifa yako huyu mama unamuona mstaarabu maana hajakutana na ushindani wa kisiasa, wala uchaguzi wowote. Kama angekuwa na ustaarabu huo unaompamba nao, asingeendelea na katazo haramu la vyama vingine kufanya siasa kwa uhuru. Leo hii upinzani wakianza kufanya siasa na akaona kabisa anaingia kwenye ushindani halisi, lazima rangi yake halisi itaonekana. Kwa mtu asiyejua lolote ndio unaweza kumlisha hii Hadaa.
Mtu, kwa sasa upinzani hawana hoja yoyote ya maana zaidi ya katiba mpya ambayo iko wazi sana na tayari inafanyiwa kazi. Tunachotofautiana ni kuhusu utaratibu tu.

Kuhusu kwamba ni mstaarabu kwa sababu hajakabiliana na uchaguzi, hili au kweli. Ustaarabu ni tabia ya mtu. Vinginevyo kwa kupata madaraka tu, ingetosha kubadilika na kufanya vitu vya ajabu lakini uungwana au uhuni ni tabia ya mtu tu.

Kuhusu siasa za upinzani, unatakiwa ujue kuwa huko nako kuna wahuni wakutosha tu, kwa hiyo bila kuweka utaratibu mzuri ni tatizo lingine tena.
 
Yaani tumekuwa nabia ya kuwa Wazalendo kwa Watawala na si kwa Nchi...

Haka kaugonjwa ni mwanzo wa kutokuwa na fikra pevu na kuwa watazamani na si wachezaji, washangiliaji na si wakosoaji...

The Future is Scary...
So kwa uelewa wako uzalendo maana yake ni ukosoaji? Well ! ukosoaji wa kujenga unakaribishwa na ni jambo jema.
 
Back
Top Bottom