SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

Daah nimesoma tusi moja tu nimekimbia aisee wahuni sio watu daah...wacha niendelee kutojua katukana nini ila kwa mtu yeyote alietekwa harafu akapona salama kimakosa huyo mtu atatukana bila hata kujua nani anamtukana..
 
Ninyi ndio mnampoteza huyo kijana badala ya kumsaidia hata kwa ushauri wa kisaikolojia. Hivi hamuoni kuwa anaendelea kupotea kabisa.
Ungejitahidi kwanza kulaani kitendo cha kutekwa kwake na hata kumuombea kifo anayejaribu kutoa uhai wa wengine .Halafu kwa pamoja tumkemee kijana
 
Ungejitahidi kwanza kulaani kitendo cha kutekwa kwake na hata kumuombea kifo anayejaribu kutoa uhai wa wengine .Halafu kwa pamoja tumkemee kijana
Mimi namkemea vikali sana huyu kijana sativa kwa mwenendo wake mbovu na usiokubalika kwa jamii wa kuporomosha matusi ya nguoni na lugha chafu.
 
Mkuu unafikiri risasi ipenye nyuma ya kichwa itokee mbele ya mdomo ni jambo dogo ? Hata kama kachanganyikiwa walio mfanyanyia lile tukio nao wanahusika kwenye kuchanganyikiwa kwake🤔
Alikuwa na kauli tata hata kabla ya kupigwa risasi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiwango alichofikia huyu kijana ni kibaya sana,ni kiwango ambacho hakihitaji kuvumiliwa wala kuachwa hivi hivi pasipo kudhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa sasa anatukana matusi ya nguoni mpaka mtu mwenye hekima na akili timamu unabaki unaona aibu na fedheha kubwa.Ni matusi na lugha ambazo yeyote mwenye akili Timamu,mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na aliyepata malezi mazuri ya wazazi wake hawezi kutukana wala kutoa iwe hadharani au mafichoni.

Sielewi huyu kijana kama wazazi wake wapo hai au walishatangulia mbele za haki.sielewi ikiwa huyu kijana ana ndugu wa karibu au viongozi wa Dini . sielewi huyu kijana kama amewahi hata kujua kama Mungu yupo na kwamba kuna siku sisi wanadamu tutakufa na kwenda kutoa hesabu mbele za Mwenyezi Mungu.sielewi kama huyu Kijana amewahi kuishi na wazazi wake na kulelewa katika ukuaji wake.

Anatoa lugha na matusi makubwa na yenye kuibua hasira,chuki na ghadhabu kubwa sana . Ni matusi na lugha ambazo hazikubaliki mbele ya jamii iliyostaarabika. Ni matusi na lugha ambazo haziwezi na hazipaswi kufumbiwa macho na kuachwa zipite hivihivi.

Huyu kijana anapaswa kudhibitiwa haraka sana.hawezi kuachwa aendelee kutukana matusi ya Nguoni.ni lazima akamatwe na kuwajibishwa kisheria.ni lazima afundishwe adabu ,ni lazima aambiwe huo siyo utamaduni wetu na siyo maadili yetu ya kitanzania. Ni lazima aambiwe wazi kwa vitendo kuwa popote pale Duniani hakuna uhuru wa kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu mbele ya watu waliostaarabika na ukaachwa hivi hivi.

Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.


Hivi aliyemteka amepatikana?

Kuna wakati mtu akikata tamaa na ukosefu wa haki.....anajua ni suala la muda tu, atakuna na mambo magumu zaidi.
 
Nipo X muda mrefu,yule hana adabu........alichofanyiwa si kitu kizuri ila anavuka mipaka na sifa zitamponza,asidhani Kenya ni mbali sana kuna siku watamuuza anasahau kuwa huku ni Africa
 
Punda wewe..ambia wanao hayo maneno sababu unawalisha! achana na mambo ya watu..when the day comes God takes care not you! endelea kula hayo makombo unayotupiwa na hao unawatetea, no one will remain in this world!
Nyumbu huwa wanamshangaa mwenzao akitafunwa na Simba, na haijulikani hua wanajiskia huruma au vinginevyo.

Epuka tabia ya nyumbu, mihemko na ghadhabu hazijawahi kumsaidia nyumbu.

kuwa mstaarabu, kua na nidhamu kwa wate.

Mungu ni wa wote wamchao. Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa.🐒
 
Back
Top Bottom