SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

Sasa kama matusi sio silaha hii mada umeileta hapa ya nini?
Au akili yako haielewi unachokijadili?

Maneno ni silaha. Matusi ni Maneno yenye sum. Ni silaha yenye sumu ndio maana umeandika hii mada.

Kumbe hujui hata ulichoandika
Matusi hayakubaliki na wala mtu hawezi kuvumiliwa au kuachwa aendelee kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu.ni lazima adhibitiwe na kufikishwa katika vyombo vyo sheria .ni lazima afundwe kisheria.
 
Sijui shuleni huwa mnaenda kusomea ujinga

Yaani Kuna wak Watati unaandika vitu mpaka wewe mwenyewe unaona aibu .

Tumia Elimu yako kuwakomboa Watanzania ,Uchawa ni utumwa wa fikira
 
Sijui kwanini Lukasi hamtakakagi kukubali kitu kimoja, mtu aliyechungulia kifo chake kwa sentimeta chache sana msitegemee kama atakuwa sawa kisaikolojia. Sijui kwanini mnaukwepa huu ukweli. Mtu aliyeponea milimita chache kuingia kuzimu kwa kupitia mkono wa binadamu mwenzake ambae bado anamuona msitegemee maisha yataendelea as normal business

Angalia Lissu angalia Sativa.

Nakuhakikishia hata wewe Lukasi au baba yako kesho mkitekwa mkafanyiwa aliyofanyiwa Sativa na watu mnaoamini wanatakiwa wawalinde badala ya kuwaangamiza hamtakuwa sawa. Trust me.
 
Wewe ni mwendawazimu kweli, hao wanaoshindwa kusimamia weledi kwa taifa zima hadi matukio ya kutekana yanaonekana kawaida tu na hawana habari mbona huwasemei?

Punguza uzwaza, tafuta chanzo cha tatizo sio unalalamikia matokeo.
 
Shida ya wanaharakati ndiyo hiyo. Dogo alianza tu vizuri baada ya kupata madhila na hata mimi nilimhurumia na kumuombea ila siku zinavyokwenda anaudhihirishia umma kwamba yeye ni liability kiasi gani kwa hili taifa la watu wastaarabu

Labda iwe ukurasa wake umedukuliwa ila kinyume na hivyo nalazimika kabisa kuviamini vyombo vya dola katika operations zao kwamba huenda kweli ni kwa maslahi mapana ya taifa na usalama wa watu wake
 

Huna ujualo kwenye mambo ya kutetea HAKI kwa sababu wewe sio mtu wa HAKI.

Kwenye vita za Ubaguzi wa rangi yapo matusi yalitumika kama silaha ikiwemo UKABURU.

Kwenye vita ya Uganda na Tanzania. Idi amini aliitwa Nduli.

Unaandika mambo usiyoyaelewa
 
Huna ujualo kwenye mambo ya kutetea HAKI kwa sababu wewe sio mtu wa HAKI.

Kwenye vita za Ubaguzi wa rangi yapo matusi yalitumika kama silaha ikiwemo UKABURU.

Kwenye vita ya Uganda na Tanzania. Idi amini aliitwa Nduli.

Unaandika mambo usiyoyaelewa
Endelea kumjaza ujinga wako juu ya ujinga wake
 
Matusi hayakubaliki na wala mtu hawezi kuvumiliwa au kuachwa aendelee kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu.ni lazima adhibitiwe na kufikishwa katika vyombo vyo sheria .ni lazima afundwe kisheria.

Lakini kutekwa na kutupwa kama panya Buku ndio kunakubalika.

Nakuambia siku zote utakuwa Liability tuu maisha yako yote.

Hata hao polisi unaowashauri wanakushangaa maana wanajua alichofanyiwa Sativa hakikuwa sahihi.
Sasa unataka Sativa aimbe mapambio kama wewe hapa
 
ATAINGIA KWENYE 18 TU MUDA SI M,MREFU NI SUALA LA MUDA TU AMUULIZE MDUDE SASAHIVI ANAYEA NDOO NA HACHOMOKI KIRAHISI SAFARI HII
 
Sijui shuleni huwa mnaenda kusomea ujinga

Yaani Kuna wak Watati unaandika vitu mpaka wewe mwenyewe unaona aibu .

Tumia Elimu yako kuwakomboa Watanzania ,Uchawa ni utumwa wa fikira
gentleman,
mimi hutoa mawaidha ya jumla jumla kwa wadau wote, ukipuuza kwa mihemko na makasiriko yako litakalokupata usilaumu kwamba mbona mbobevu hukushauri kabla..

kuporomosha matusi sio ujasiri gentleman ni ujinga πŸ’
 
Wewe unataka afanye nini ili aipate haki yake ikiwa vyombo vya kisheria vimekaa kimya?

Tupe solution yako maana malalamiko bila kuchukua Hatua ni upumbavu!!
 
Kwanza tujiulize hapo kabla ni kitu gani huyu Sativa alifanya mpaka kupelekea kutekwa?.

Je huko nyuma alikuwa akiishi vipi mitandaoni?.

Tusimtetee mtu au kumjaji kwa sababu za juu juu tuu pasipo kujua undani wa watu haoa, mtekwaji na watekaji, yatupasa kwanza hao wote tuwajue kinda ni.


Haiwezekani mtu aje tu pasipo sababu ya msingi aje akuteke ni wazi kuna jambo limejificha hapo panahitaji tafakari.

Tusiweke mihemko mbele kwa kila kitu cha mtandaoni, binafsi ngoja nifatilie kabla hajatekwa na maisha baada ya kutekwa halafu ndio nione upande up uko sawa.
 
ANALIWA TIMING TU ATANASA TU NI SUALAL LA MUDA TU MTAMSKIA ANALILIA MAHABUSU MPAKA AKOME ATAHENYA MWAKA HUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…