SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

Kwanza tujiulize hapo kabla ni kitu gani huyu Sativa alifanya mpaka kupelekea kutekwa?.

Je huko nyuma alikuwa akiishi vipi mitandaoni?.

Tusimtetee mtu au kumjaji kwa sababu za juu juu tuu pasipo kujua undani wa watu haoa, mtekwaji na watekaji, yatupasa kwanza hao wote tuwajue kinda ni.

Haiwezekani mtu aje tu pasipo sababu ya msingi aje akuteke ni wazi kuna jambo limejificha hapo panahitaji tafakari.

Tusiweke mihemko mbele kwa kila kitu cha mtandaoni, binafsi ngoja nifatilie kabla hajatekwa na maisha baada ya kutekwa halafu ndio nione upande up uko sawa.
Hata kabla hajatekwa alikuwa anaitukana serikali ila kwa sasa ndo amezidisha, fuatilia utajua.
 
Mna bahati sana huko majimboni mnaongoza watu mnaowamudu gentleman 🐒
sio bahati gentleman, ni Neema na Baraka za Mungu tu, ukisema neno moja tu na roho za wananchi zinatulia, zinapona, nanakuamini na kukufuata wewe tu...

kwa kuporomosha matusi nani atakuelewa gentleman? Hata Baraka zinakaa mbali nawe 🐒
 
nchi yetu matus n luksa ila si luksa kuikosoa selikali.. wacha atukane tu mana kam upo mahali ambapo huwez kupata haki yako kila mtu huwa na namna flani akifanya anapunguz machungu moyn mwake..
 
Matusi yanamsaidia vipi kupata haki anayoona hajapewa au kutendewa? Ni vipi matusi yakawa utetezi?ni vipi matusi yakakupa msaada wa njia ya kufikia ushindi wa kupata haki? Ni wapi na nani aliwa kupata ushindi kwakuporomosha matusi ya nguoni. Wewe unaweza kutukana matusi atukanayo SATIVA na ukawapa na wazazi wako waone na kusoma? Ndivyo unavyoweza kuwafundisha wanao kuwa wawe wanatukana sana matusi katika kupigania haki zao au kufikisha ujumbe fulani?Ndivyo unavyoweza kuwapa ushauri huo watu na jamii iwe ya kutukanana matusi katika kupigania haki?
Wewe BWABWAH
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiwango alichofikia huyu kijana ni kibaya sana,ni kiwango ambacho hakihitaji kuvumiliwa wala kuachwa hivi hivi pasipo kudhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa sasa anatukana matusi ya nguoni mpaka mtu mwenye hekima na akili timamu unabaki unaona aibu na fedheha kubwa.Ni matusi na lugha ambazo yeyote mwenye akili Timamu,mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na aliyepata malezi mazuri ya wazazi wake hawezi kutukana wala kutoa iwe hadharani au mafichoni.

Sielewi huyu kijana kama wazazi wake wapo hai au walishatangulia mbele za haki.sielewi ikiwa huyu kijana ana ndugu wa karibu au viongozi wa Dini . sielewi huyu kijana kama amewahi hata kujua kama Mungu yupo na kwamba kuna siku sisi wanadamu tutakufa na kwenda kutoa hesabu mbele za Mwenyezi Mungu.sielewi kama huyu Kijana amewahi kuishi na wazazi wake na kulelewa katika ukuaji wake.

Anatoa lugha na matusi makubwa na yenye kuibua hasira,chuki na ghadhabu kubwa sana . Ni matusi na lugha ambazo hazikubaliki mbele ya jamii iliyostaarabika. Ni matusi na lugha ambazo haziwezi na hazipaswi kufumbiwa macho na kuachwa zipite hivihivi.

Huyu kijana anapaswa kudhibitiwa haraka sana.hawezi kuachwa aendelee kutukana matusi ya Nguoni.ni lazima akamatwe na kuwajibishwa kisheria.ni lazima afundishwe adabu ,ni lazima aambiwe huo siyo utamaduni wetu na siyo maadili yetu ya kitanzania. Ni lazima aambiwe wazi kwa vitendo kuwa popote pale Duniani hakuna uhuru wa kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu mbele ya watu waliostaarabika na ukaachwa hivi hivi.

Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Sijasoma uzi wako ila nimesoma heading tu nikaelewa.
Nikuulize tu mleta mada hivi siku ukitekwa wewe au mwanao akapitia aliyoyapitia huyo bwana mdogo Sativa utakuja hapa kuandika hiki ulichoandika?!
Matukio haya yana matokeo mabaya sana huko mbeleni maana hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kufurahia mwanaye apotezwe au kuachwa na kilema cha maisha halafu unataka asifu na kuabudu!
Dogo alieleza kila kitu lakini ameishia kupuuzwa kama mwendawazimu!
Haya angalia tukio la mzee Kibao Unaambiwa muuaji hajulikani na hili tukio la juzi mpaka clipp na picha na sura za wahusika zimeonekana kabisa lakini mpaka leo ishu imepita kimya kimya
Watu wana maumivu wanaogopa kusema ukweli kwa kuhofia yatawakuta lakini ipo siku roho ya kinyama itawavaa wananchi wengi na kitakachotokea ni balaa
 
sio bahati gentleman, ni Neema na Baraka za Mungu tu, ukisema neno moja tu na roho za wananchi zinatulia, zinapona, nanakuamini na kukufuata wewe tu...

kwa kuporomosha matusi nani atakuelewa gentleman? Hata Baraka zinakaa mbali nawe 🐒
Huyo Mungu ni danganya toto kwanza hauwezi thibitisha uwepo wake .

Kuporomosha matusi pande zote tu, huwa mnafanya hivyo, hasa hasa kwa wale wanaoona ugali wao unaguswa kwa upande wenu gentleman 🐒
 
Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ona tusi hili kww IGP Camillius Wambura:-
Screenshot_20241123_103505_X.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiwango alichofikia huyu kijana ni kibaya sana,ni kiwango ambacho hakihitaji kuvumiliwa wala kuachwa hivi hivi pasipo kudhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa sasa anatukana matusi ya nguoni mpaka mtu mwenye hekima na akili timamu unabaki unaona aibu na fedheha kubwa.Ni matusi na lugha ambazo yeyote mwenye akili Timamu,mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na aliyepata malezi mazuri ya wazazi wake hawezi kutukana wala kutoa iwe hadharani au mafichoni.

Sielewi huyu kijana kama wazazi wake wapo hai au walishatangulia mbele za haki.sielewi ikiwa huyu kijana ana ndugu wa karibu au viongozi wa Dini . sielewi huyu kijana kama amewahi hata kujua kama Mungu yupo na kwamba kuna siku sisi wanadamu tutakufa na kwenda kutoa hesabu mbele za Mwenyezi Mungu.sielewi kama huyu Kijana amewahi kuishi na wazazi wake na kulelewa katika ukuaji wake.

Anatoa lugha na matusi makubwa na yenye kuibua hasira,chuki na ghadhabu kubwa sana . Ni matusi na lugha ambazo hazikubaliki mbele ya jamii iliyostaarabika. Ni matusi na lugha ambazo haziwezi na hazipaswi kufumbiwa macho na kuachwa zipite hivihivi.

Huyu kijana anapaswa kudhibitiwa haraka sana.hawezi kuachwa aendelee kutukana matusi ya Nguoni.ni lazima akamatwe na kuwajibishwa kisheria.ni lazima afundishwe adabu ,ni lazima aambiwe huo siyo utamaduni wetu na siyo maadili yetu ya kitanzania. Ni lazima aambiwe wazi kwa vitendo kuwa popote pale Duniani hakuna uhuru wa kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu mbele ya watu waliostaarabika na ukaachwa hivi hivi.

Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hakuna watu wanatukana kama majeshini...huku sio ualimu wako wewe chawa wa kijani..kiufupi lugha anayotumia Sativa ndio Lugha wanayoelewa PT wale ni mashetani kamili...
 
Kitendo cha kumzuia mtu anayeona njia anayoitumia kutetea HAKI zake na kujiponya nafasi yake ni kuonyesha unasapoti waliomfanyia ubaya huo.

Ni kama watu wanaolaumu Hammas dhidi ya wayahudi

Iko hivyo logically
Bro, naomba hii comment iwe ya mwisho kwako mana naona hatuelewani.

Mm nampinga yeye kutumia matusi kupata haki yake na sio kwamba nasapoti alichofanyiwa.
Em angalia hiyo screenshot hapo juu.

Uwe na siku njema mkuu.
 
Back
Top Bottom