SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

SATIVA adhibitiwe kwa matusi ya nguoni anayotoa mitandaoni

Kwanza tujiulize hapo kabla ni kitu gani huyu Sativa alifanya mpaka kupelekea kutekwa?.

Je huko nyuma alikuwa akiishi vipi mitandaoni?.

Tusimtetee mtu au kumjaji kwa sababu za juu juu tuu pasipo kujua undani wa watu haoa, mtekwaji na watekaji, yatupasa kwanza hao wote tuwajue kinda ni.


Haiwezekani mtu aje tu pasipo sababu ya msingi aje akuteke ni wazi kuna jambo limejificha hapo panahitaji tafakari.

Tusiweke mihemko mbele kwa kila kitu cha mtandaoni, binafsi ngoja nifatilie kabla hajatekwa na maisha baada ya kutekwa halafu ndio nione upande up uko sawa.
Sababu ya kutekwa ni aliwatetea wafanya Biashara wa kariakoo ule mwezi wa Saba walipogoma kufungua maduka.

Ile ishu alitetea sana huko x na alikuwa against serikali.

Akatekwa kwa kuonekana analeta ujuaji. Wakampeleka Huko walikompeleka ili wamuue,ila Mungu hakupenda,Leo huyu hapa anawaadhibu watesi wake kwa njia ya maneno makali mnaita matusi ya nguoni.
 
Sativa jana kamtukana vibaya sana IGP kiasi kwamba hata baadhi ya supporters wake walishtuka. Mbowe na CHADEMA kwa ujumla watatafunwa na dhambi ya kuwaharibia maisha watoto wa maskini kama Sativa na Mdude. Huwezi sikia mtoto wa Mbowe, Lema, Kigaila na vigogo wengine wa CHADEMA wakitoa kauli chafu kwa mtu hasa serikali. Wamelelewa kwa adabu ya hali ya juu. Ila viongozi wa CHADEMA huhamasisha watoto wa maskini kupambana na dola kitu ambacho ni hatari.
 
Bc ukang'oe jino halafu tuseme umeng'olewa kichwa kwa sababu jino lipo kichwani.
Jino ni sehemu ya kichwa hakuna mahali utapang'oa na utasema umeong'oa kichwa kwa sababu ili sehemu iitwe kichwa ni mjumuisho wa vyote vilivyopo juu ya shingo yako😂😂😂
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiwango alichofikia huyu kijana ni kibaya sana,ni kiwango ambacho hakihitaji kuvumiliwa wala kuachwa hivi hivi pasipo kudhibitiwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa sasa anatukana matusi ya nguoni mpaka mtu mwenye hekima na akili timamu unabaki unaona aibu na fedheha kubwa.Ni matusi na lugha ambazo yeyote mwenye akili Timamu,mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na aliyepata malezi mazuri ya wazazi wake hawezi kutukana wala kutoa iwe hadharani au mafichoni.

Sielewi huyu kijana kama wazazi wake wapo hai au walishatangulia mbele za haki.sielewi ikiwa huyu kijana ana ndugu wa karibu au viongozi wa Dini . sielewi huyu kijana kama amewahi hata kujua kama Mungu yupo na kwamba kuna siku sisi wanadamu tutakufa na kwenda kutoa hesabu mbele za Mwenyezi Mungu.sielewi kama huyu Kijana amewahi kuishi na wazazi wake na kulelewa katika ukuaji wake.

Anatoa lugha na matusi makubwa na yenye kuibua hasira,chuki na ghadhabu kubwa sana . Ni matusi na lugha ambazo hazikubaliki mbele ya jamii iliyostaarabika. Ni matusi na lugha ambazo haziwezi na hazipaswi kufumbiwa macho na kuachwa zipite hivihivi.

Huyu kijana anapaswa kudhibitiwa haraka sana.hawezi kuachwa aendelee kutukana matusi ya Nguoni.ni lazima akamatwe na kuwajibishwa kisheria.ni lazima afundishwe adabu ,ni lazima aambiwe huo siyo utamaduni wetu na siyo maadili yetu ya kitanzania. Ni lazima aambiwe wazi kwa vitendo kuwa popote pale Duniani hakuna uhuru wa kutukana matusi kama kichaa au mwendawazimu mbele ya watu waliostaarabika na ukaachwa hivi hivi.

Kama kuna mtu anaweza kuunga mkono matusi ya huyu kijana basi atakuwa ni mtu wa ajabu sana,mwenye matatizo ya akili,mwenye kukosa hofu ya Mungu na aliyekosa malezi ya wazazi wake na mwenye matatizo kichwani na asiyejitambua.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mkuu muache ateme nyongo, Mwashambwa hujui maumivu ya kufumuliwa mdomo kwa risasi!!!
 
Perhaps he's in a state of a DEAD MAN WALKING..........
Which it might describe someone who is emotionally detached or going through the motions in life, feeling lifeless or without purpose.
 
Back
Top Bottom