Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Anaandika kijana aliyetekwa na kunusrika kuliwa na mamba huko Katavi maarufu kama Sativa.
HUU NI MKOA WA MBEYA. NA MBUNGE WAKE NI SPIKA WA BUNGE.
Huyu spika yupo kwenye nafasi hiyo ya uspika na unaibu spika kwa zaidi ya miaka 7 sasa.
Hapa ndio jimboni kwake, yeye ndie anaesimamia vikao vya ujenzi wa barabara kwenda mikoa mingine na maendeleo mengine kwenye mikoa yote Tanzania.
Kuna muda kama wananchi wa mkoa wa Mbeya tunapata aibu sana kuunadi mkoa wetu. watu wengi sana hawajawahi kufika Mbeya na ni mkoa unaojiuza sana mitandaoni.
Mtu anakuja Mbeya na hamu zake za kuuona mkoa afu anakutana na MABWAWA kama haya. Ni mkoa ambao kipindi cha VUMBI inakuwa kasheshe.
Msimu wa matope inakuwa ni kasheshe. Wananchi wa Mbeya hatujawahi kupumzika miaka yote tangu tuzaliwe. Na ukimsikiliza MBUNGE yeye hoja zake ni kwamba yupo karibu na wananchi anahudhuria sana kwenye misiba.
Anamiliki kitega uchumi cha kukopesha wakina mama , analeta mashindano watu wakimbie kimbie kama wamewehuka vichwani. Hizo ndio hoja zake.
Nawaza tuanzishe mfuko kama wananchi tuchange hela tujenge barabara zetu wenyewe maana tunaoteseka ni sisi. Wao wanashinda DAR.
Mvua zikianza mbeya USIJE utajuta, jua likianza mbeya usije utajuta kwa vumbi. Hiyo ndio Mbeya hatutaki wageni tutaona aibu.
Inaumiza sana aisee.
SATIVA17🫡
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - CHADEMA Mbeya Mjini, Tafuteni Mgombea Mwingine
- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi adai mbunge Tulia Ackson ameshindwa kuendeleza mazuri Mbeya
- Kuelekea 2025 - Kinachoendelea Mbeya kamatakamata ya viongozi wa CHADEMA ni msiba kwa spika Tulia Akson na CCM