Sauli: Bilionea ambaye Wazungu/Wageni wanamtambua Waswahili hatujamfahamu kabisa

Sauli: Bilionea ambaye Wazungu/Wageni wanamtambua Waswahili hatujamfahamu kabisa

uwezo wa kufikiri kwa watanzania wengine ?????????. Unamuona mtu yupo mgodini na ana mabasi ya Ulaya say 10, you just conclude kuwa huyo mtu ni tajiri!
Utajiri unaongelewa kwa NAMBA. Nikiwa na maana mngeniambia:
1. net worthy ya Sauli ni kiasi gani,
2. hayo mabasi amenunua cash au ni mkopo na kama ni mkopo upo secured na mali zipi za Sauli?
3. Onyesha basi hata after tax profit ya kampuni za/yake kwa miaka hata 5 ili tuwe na uhakika kwamba huyu bwana ni tajiri.
Nasema hivyo kwa sababu unaweza kuta Sauli hana hata basi moja la kwake, kwamba ile fleet ni ya wapiga deal, wanatakatisha pesa. Wapiga deal kama:
1. Lugola na Ande - proceeds za mgao wa deal lao
2. Chenge na yule jaji aliyekuwa AG - proceeds za mgao wa escrow
3. Bashite Proceeds ya kodi aliyokwepa kwenye makontenna ya samani alizoingiza kutoka Marekani
4. Mzee wa mjengoni aliyelipwa Tshs. 12b/= kwa ajili ya matibabu India nk.
Simdharau au kukakataa kwamba Sauli hawezi kumiliki huo ukwasi, ila nataka uonyeshe ushahidi.
 
Mbona mimi nina pesa hamnitangazi jamani nikapata misifa.
 
Juzi kati tukiwa katika maongezi na my Salty Dawg..
mara tukabadili ukurasa wa maongezi, tukaingia kwenye usafirishaji...
Looh. ndo ikawa mara ya kwanza sikia ilo jina na ikawa ndo mara kwanza kujua kwamba Scania wanatengeneza mabasi...

kwa mara ya pili nimekutana na jina ili hapa jukwaani.


Sent using Jamii Forums mobile app
I see. Ina maana zile basi za Dar Express, Mtei na Kilimanjaro hukujua kwamba ni Scania? Itakuwa unaishi porini sana 🤣 🤣 🤣 👆 👆
 
Basi inawezekana watu walionipa hiyo story walichanganya.

Halafu stori ya raisi kupewa dhahabu imepindishwa

Kuna mkushi mmoja kajichimbia bush ndani ndani huko anaitwa mwembe ndio mwenye hiyo record ya kutoa dhahabu kama zawadi

Sauli sio tajiri kivile labda kwasababu bado kijana ndo maana wanam-bust lakini hata hivyo still yuko vizuri kipesa sema amekosa washauri wenye kumshauri namna gani nzuri ya kuwekeza pesa zake zikazaa
 
Mkuu umeelezea vizuri...endelea kutupa michapo.




Sauli ni kijana mdogo ambaye anapenda sana maujiko, nakumbuka alikua anapenda sana kucheza pool table.

Sa ikitokea anacheza pool table halafu ukawa mpambe wake kumpa sifa basi pesa atayopata hapo kama akimfunga mpinzani yote anakupa wewe.

Wahuni walipogundua huo udhaifu wakawa kila kona wako naye, hua anapenda kutembea na katoto kake basi hapo wahuni wakawa wamepata tiketi.


Sauli akianza kucheza wahuni wanambeba mtoto wanajidai wanacheza naye, na ukimbeba mtoto utakuta anakupa 20k anasema kamnunulie juice mtoto halafu chenchi inayosalia yako.

Ikafika hatua wahuni wakawa wanagombea kumchukua mtoto, yani kila mtu anataka aonekane na sauli kamshika mtoto wake. Na jamaa alikua hana kwere haijalishi mmeshika wangapi alikua anahakikisha kila mmoja anamtembezea michuzi

Hata mpinzani wake kwenye pool alikua akikufunga na kukumaliza pesa zako hua anakurudishia na wale wadau waliokua pembeni yake wanamshangilia nao anawatembezea michuzi

Alikua anapenda sana mashindano ya piki piki sijui kwa saizi, kipindi kile nakumbuka alikua analipia kibali polisi kwa ajili ya kufanya battle ya pikipiki na jamaa mmoja alikua anaitwa konga

Analipiki piki lake hilo moja hatari yani umbali wa kilomita 75 ye alitumia dakika 6

Ana mengi ya kustaajabisha na mengi katika hayo ni ukijana sana halafu yuko social
 
Nakazia kwenye dhahabu pesa zao ndogo tu,wanaishia kujenga vilodge vidogo.
Pesa iko kwenye gemstone tu
 
Acha uongo mkuu....
Tuchukulie dhahabu hii ilipatikana jana ambayo ni sawa na gram 5000
Gram 1 kwa bei ya jana soko la dunia ilikua 127,990 Tsh.
Tuchukulie hii dhahabu ilikua na Purity ya 100% (swala ambalo ni gumu lazilma iwe pungufu)

So
5000*100%*127,990=636,950,000Tsh.
Je hii fedha unailisha chunya kwa miezi au mwaka??
hahahahahahahahahahaha.....Lita kufa jitu.
 
na km 75 ni sawa na kutoka mby to chny

wenzako walikua wabishi kam,a wewe likawekwa dau mezani
Ngoja tudanganyane kwa hisabati basi ndugu mleta hoja, ndipo tuaminishane ama tupotoshane.
Dakika 6 (alizotumia Sauli kuendesha pikipiki kilometa 75) ni sawa na sekunde 360.
Nikichukua sekunde 360, nikagawa kwa 75 (km) napata 4.8, ina maana kila baada ya sekunde 5 jamaa anakata kilometa moja, hii kwa kutumia pikipiki HAIWEZEKANI kwa njia ya Chunya. The same way, ukichukua kilometa 75 ukagawa kwa dakika 6 alizotumia (75/6=12.4). Ina maana Sauli anaendesha kilometa 12.5 kwa dakika moja, kitu ambacho SIO kweli. Huwezi kuendesha pikipiki kwa barabara ya Chunya kwa mwendo huo. Hata kutoka Uyole kwenda Sokomatola (paliponyooka) HUWEZI kuendesha kwa dakika moja.
Kiufupi HATUDANGAYIKI. Nimeandika kisayansi, lete hoja kisayansi pia.
 
Konga yuko Pale Makongolosi, kachoka ile mbaya, licha ya ujeuli aliokuwa nao enzi hizo.
Namkumbuka konga alikuwa akisema "kuishiwa Mimi pesa ni mpaka dunia yote iishiwe pesa". Saizi yuko hoi bin taabani.

Huyo mpumbafu wenu Konga na maneno yake ya nyodo mwambieni sasa aje kwangu Msoga nimpe kazi ya kufuga Tausi wangu kwani hana adabu kwa dunia
 
Ngoja tudanganyane kwa hisabati basi ndugu mleta hoja, ndipo tuaminishane ama tupotoshane.
Dakika 6 (alizotumia Sauli kuendesha pikipiki kilometa 75) ni sawa na sekunde 360.
Nikichukua sekunde 360, nikagawa kwa 75 (km) napata 4.8, ina maana kila baada ya sekunde 5 jamaa anakata kilometa moja, hii kwa kutumia pikipiki HAIWEZEKANI kwa njia ya Chunya. The same way, ukichukua kilometa 75 ukagawa kwa dakika 6 alizotumia (75/6=12.4). Ina maana Sauli anaendesha kilometa 12.5 kwa dakika moja, kitu ambacho SIO kweli. Huwezi kuendesha pikipiki kwa barabara ya Chunya kwa mwendo huo. Hata kutoka Uyole kwenda Sokomatola (paliponyooka) HUWEZI kuendesha kwa dakika moja.
Kiufuoi HATUDANGAYIKI. Nimeandika kisayansi, lete hoja kisayansi pia.
mjomba unatumia sayansi ya nadharia kutafuta jibu wakati ni swala la kwenda chunya na kuweka dau mezani ukajifunze kwa practical?

watu wanatumia sayansi ya theory kwenye magalaxy huko anga za juu kwa sababu sio rahisi kufika, sasa we hapa Chunya nako unahitaji theory?

kwa estimation zako na sayansi uliyoitumia inakuambia alitakiwa atumie dakika ngapi bwana sauli ngapi bila kuzidisha?
 
Back
Top Bottom