Zacht
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 1,026
- 2,266
JINSI MVUA INAVYO SABABISHA MMEA KUOTA KWA HATUA KATIKA QUR'AN
Kwa maelezo ya Qur-an na Sayansi
Allaah anasema katika Qurani
“... Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri.”(Quran 22:5)
Inafahamika kuwa hakuna uhai pasina maji na hewa. Lakini je imepata kupita kwenye akili ya yeyote kuwa udongo nao unayo sehemu yake kwenye hili? Quran hapa imetaja hatua tatu muhimu kwenye maisha ya udongo.
(1)Kutetema
(2) kuvimba (kututumka)
(3) kutoa mimea ya aina kwa aina (dume na jike)
Kwa kulinganisha maelezo ya wana sayansi na hatua zilizo tajwa kwenye Quran
Hatua ya kwanza mvua inapodondoka, chembe, chembe tofauti zinazo tengeneza chembe moja ya mchanga, zinaanza kutetema na kupokea au kupunguza chaji zake za kiumeme kutokana na matone ya mvua yanayo dondoka. Mwaka 1828, mtetemo huu wa udongo kutokana na matone ya mvua uliitwa ‘Brown Movement’ baada ya Robert Brown kufanya ‘uvumbuzi’ huo na kuieleza dunia kuwa matone ya mvua yanapo shuka vichembe, vichembe tudogo, tudogo, vinavyo tengeneza chembe moja ya mchanga vinatetema.
Hatua ya pili, Quran inazungumzia kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa chembe hizo za mchanga au mchanga kwa ujumla. Chembe ya mchanga hutengenezwa na tabaka mbili, baina ya tabaka hizo kuna nafasi ambayo inaruhusu maji na chaji zinazo tokana na matone ya mvua kupenya, kisha kutokana na athari hiyo udongo unatanuka au unavimba.
Hatua ya tatu, baada ya hapo ni udongo ulio kuwa umekufa, unapata uhai, na kutoa uhai kwa mimea ambayo nayo itasababisha kupatika uhai kwa viumbe wengine akiwemo binadamu.
Zama zote binadamu tumekuwa tukifahamu kuwa mvua ndiyo inayo sababisha mimea kuota, lakini hatukuwa hata kidogo, tukifikiria ni hatua gani au ni kitu gani kinacho tokea kabla ya mimea kuchomoza. Lakini ni vipi katika zama za Muhammadi binadamu angeweza kuzitambua hatua hizo zinazo pitiwa na udongo kabla ya kuanza kuotesha mimea yake?
Kama tulivyo ona, hatua hii ya muhimu sana, tunaikuta inavumbuliwa mwaka 1828, na kutokana na heshima na thamani uvumbuzi huo, tendo lenyewe linapewa jina la mvumbuaji, lakini Muhammad alishakisema karne zaidi ya kumi kabla, sasa inakuwaje? Vipi Muhammad aliweza kuliona hili, ni wapi alipatia taarifa hizi, ni vipi hazipingani hata kidogo na uvumbuzi wa zama zetu?