Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Kanuni hii haiwezi kuapply katika mjadala wa Mungu,kwa sababu Wanaomthibitisha Mungu wanamthibitisha kupitia matukio ama vitu ambavyo tunaviona na kuvikiri.

Hivyo wanaomthibitisha Mungu wao humthibitisha kwa yale mambo yaliyothibiti.

Kwa mantiki hiyo wanaokanusha uwepo Wa Mungu mbele ya wakubaliji uwepo wa Mungu basi hawa wakanushaji nao wanayo dhima ya kuthibitisha kutokuwepo kwake.

Hivyo kanuni hiyo haiwezi kuapply katika mjadala huu.

Ndio maana yule bwana mkubwa

Stephen Hawking's

Aliandika kitabu chake akakiita

There's 'No Possibility' of God in Our Universe.

Humo kaweka uthibitisho (kwa mjjibubwa yeye) wa kuthibitisha kwamba hakuna Mungu.

Hivyo hata wanaopinga Mungu hayupo nao wanatakiwa wathibitishe kwa hoja mbalimbali kama alivyofanya bwana stephen.
Dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mkamilifu, mwenye huruma na upendo kwenye dunia iliyo jaa uovu, ukatili, uasi na mabaya ya kila aina ni uthibitisho tosha kwamba Mungu huyo anaye daiwa kwamba ni mwema, mwenye upendo na huruma Hayupo.

Kama Mungu huyo yupo Basi ni mkatili na Muovu sana.
 
Unaweza kuthibitisha uwepo wa electron? Hivi unajua kwamba umeme hakuna mtu amewahi kuuona? Unachoona ni effects za uwepo wa umeme. Ukiweka taa utaona mwanga na kusema umeme upo japo hauuoni.
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika au kuhisika.

Hizo electrons unaweza kuthibitisha zipo kwa kuzihisi pindi umeme unapo safiri, ndio maana unahisi shoti ukiguswa na umeme.

Hapo electron zinatambulika zipo.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile haonekani, Hashikiki, Haisiki wala Hasikiki.

Mungu huyo ni mawazo ya kufikirika tu, Imaginations just an illusion.

Basi hata Mungu tunamuona kupitia matendo yake makuu hasa katika uumbaji wa ulimwengu na vyote vilivyo ndani yake.
Haya ni mawazo yako na imani ya kufikirika tu.

Haithibitishi Mungu huyo yupo.

Mungu huyo Hayupo katika uhalisia ila katika dhana ya kufikirika tu.
 
Eeeh naamini tutamfunga Wydad maana yake sina uhakika ndio maana naamini

Wydad namjua tumecheza naye mechi tatu kashinda 2 nimeshinda moja.

Mechi ya mwisho alipigiwa mpira mwingi na bao alipata kizari tu na ndio maana wametimua kocha

Kwasababu mpira ni namba basi matumaini yangu ya kumfunga Wydad nayaona ila ipo nafasi pia ya matokeo kuja tofauti.

Sasa Mungu sababu ya kuamini kwanza nitakuuliza katika maelfu ya Miungu, Mungu gani unayetaka mimi nimuamini?

Na kwanini wewe huamini Miungu hiyo mingine?
Kwahiyo kutokuwa na uhakika wa jambo ndio kuamini au wewe hauna uhakika na unachokiamini? Kwa sababu navyojua mimi hata kwa jambo ambalo utaona una uhakika bado ipo chance ya kutokea tofauti.

Sijasema Mungu nimesema muumbaji.
 
Dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mkamilifu, mwenye huruma na upendo kwenye dunia iliyo jaa uovu, ukatili, uasi na mabaya ya kila aina ni uthibitisho tosha kwamba Mungu huyo anaye daiwa kwamba ni mwema, mwenye upendo na huruma Hayupo.

Kama Mungu huyo yupo Basi ni mkatili na Muovu sana.
Unajadili upendo na wema wa Mungu au kuwepo kwa huyo Mungu? Kwani ili Mungu awepo lazima awe mwema na mwenye upendo?
 
Hivi kuna tofauti ya kutokuamini Mungu na kudai hakuna Mungu?
Tofauti ipo, unaweza kusema Mungu yupo lakini usiwe na utaratibu wowote wa kiibada kuhusiana naye.
 
Unajua unakosea hadi kuuliza swali

Nani kaweka ndani ya mwanadamu ndio swali gani?

Nini kinachokufanya ufikiri morality inapaswa kuwekwa na hicho kitu ukichokipa identity ya "nani"?
Unalikimbia swali, ngoja nikuulize hivi, kwanini ulimwengu una ulandano (uniformity)?
 
Kwahiyo kutokuwa na uhakika wa jambo ndio kuamini au wewe hauna uhakika na unachokiamini? Kwa sababu navyojua mimi hata kwa jambo ambalo utaona una uhakika bado ipo chance ya kutokea tofauti.

Sijasema Mungu nimesema muumbaji.
Penye uhakika, hakuna imani

Penye imani, hakuna uhakika
 
Dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mkamilifu, mwenye huruma na upendo kwenye dunia iliyo jaa uovu, ukatili, uasi na mabaya ya kila aina ni uthibitisho tosha kwamba Mungu huyo anaye daiwa kwamba ni mwema, mwenye upendo na huruma Hayupo.

Kama Mungu huyo yupo Basi ni mkatili na Muovu sana.
Uovu unaouona uliingia duniani baada ya mwanadamu kuasi maagizo ya Mungu.

Mungu, kwasababu ya upendo wake mkuu, aliamua kumpa mwanadamu uhuru wa kuchagua anachotaka.
 
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika au kuhisika.

Hizo electrons unaweza kuthibitisha zipo kwa kuzihisi pindi umeme unapo safiri, ndio maana unahisi shoti ukiguswa na umeme.

Hapo electron zinatambulika zipo.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile haonekani, Hashikiki, Haisiki wala Hasikiki.

Mungu huyo ni mawazo ya kufikirika tu, Imaginations just an illusion.
Moyo wako unapodunda na kusukuma damu ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu. Mpaka leo wanasayansi hawajui ni kitu gani kinasababisha heartbeats.

Kwahiyo uwepo wa Mungu upo kila mahali hata hewa unayovuta ni uthibitisho wa uwepo wake.
 
Unajadili upendo na wema wa Mungu au kuwepo kwa huyo Mungu?
Imani nyingi na dini nyingi humtafsiri na ku uelezea uwepo wa Mungu huyo kama mwema na mwenye Upendo.

Sasa kwenye dunia iliyo jaa uovu, ukatili, uasi na mabaya automatically Mungu huyo mwema na mwenye Upendo kwa mujibu imani hizi na dini hizi hayupo.

Otherwise Mungu huyo ni mkatili na muovu sana.
Kwani ili Mungu awepo lazima awe mwema na mwenye upendo?
Hakuna ulazima wa Mungu kuwepo.

Mungu huyo Hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Moyo wako unapodunda na kusukuma damu ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu. Mpaka leo wanasayansi hawajui ni kitu gani kinasababisha heartbeats.
Umejuaje moyo kudunda na kusukuma damu ni Mungu hufanya hivyo?

Thibitisha kwamba ni Mungu na si imani na mawazo yako ya kufikirika tu.

Au mwambie Mungu huyo aje hapa athibitishe kwamba ni yeye hufanya moyo kudunda.
Kwahiyo uwepo wa Mungu upo kila mahali hata hewa unayovuta ni uthibitisho wa uwepo wake.
Unathibitisha vipi kwamba hewa ninayo vuta ni ya Mungu?

Umejuaje kwamba hewa ni ya Mungu?

Niki kwambia kwamba hewa unayo vuta ni ya Aliens 👽bila uthibitisho uta amini?

Kusema tu hewa ninayo vuta ni ya Mungu bila uthibitisho, Hata mimi naweza kusema hewa unayo vuta ni ya Aliens 👽 bila uthibitisho.

Si kusema tu, kama wewe unavyo sema hewa ni ya Mungu ila huna uthibitisho wa ukisemacho.
 
Ulandano ndio nini? ebu fafanua
Ulimwengu una uniformity, angalia uumbaji wa species mbalimbali za wanyama na mimea. Gravitational force ipo consistent ulimwenguni.. nk
 
Ulimwengu una uniformity, angalia uumbaji wa species mbalimbali za wanyama na mimea. Gravitational force ipo consistent ulimwenguni.. nk
Unaposema angalia uumbaji, niangalie wapi?

Labda huko kwako ulipo ndio huo uumbaji unaonekana

Huko nilipo mimi siuoni labda unipe maana ya uumbaji ni nini
 
Back
Top Bottom