Seba aliyeandika meseji kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho kwenye ghorofa ya Kariakoo lililoanguka, akutwa amefariki

Seba aliyeandika meseji kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho kwenye ghorofa ya Kariakoo lililoanguka, akutwa amefariki

Mungu hana ithibati ya kisayansi unayotaka wewe, unataka umuone kwa macho, unataka umguse au umhisi kwa milango yako ya fahamu, hilo haliwezekani bila imani.
Wapi nimesema nataka kumuona kwa macho?

Wapi nimesema nataka nimguse?

Wapi nimesema nataka nimhisi?

Unajua kusoma kwa ufahamu wewe?
 
Kwa imani yako ni sawa, but for me MUNGU yupo.
Kitu kuwepo au kutokuwepo si suala la imani.

Ni suala la uhalisia.

Ukiamini kuwa wewe ni Elon Musk tajiri wa kwanza wa dunia hii, wakati wewe si Elon Musk, imani hiyo haikufanyi uwe Elon Musk tajiri wa kwanza wa dunia hii.

Unaelewa hilo?
 
Its painful 😣

Hiv kam jengo moja ndio limeanguk tena ndan ya jiji kubwa na karbu krbu na fire (waokozi) lakn zoez la ukoaji watu halijakamilika itakuwaje siku magorofa 5/20 yakiangukia watu huko mikoa ya pembezon 😐😐
Kwa hiyo unataka kila gorofa kuajiriwe kikosi cha kuokoa au? Nyumba ikijengwa haitakiwi kuanguka suala ni kuziba mianya ya kipuuzi kujenga holela na vibali kununuliwa huko ndio kuna shida. Kuna magorofa yalijengwa enzi hakuna rushwa mpaka leo yapo imara.
 
Vifo vingi nchini ni uzembe wa siasa na mfumó wa uongozi Tanzania. Wakulaumiwa ni Nyerere (mnayemuita baba wa Taifa) alieruhusu janga hili ccm iendelee kwenye mfumo wa vyama vingi. Ilitakiwa ccm ife ipotee kwa sababu ni chama dola kilichokuea na matawi mpaka jeshini[ yaani majeshi yote na watu wote walikuwa ccm],
katiba mpya ingeanzishwe na vyama mbadala kukiwa na masharti laini kwa wanachama.
Sio eti viongozi wote lazima wawe ccm. Najua wachache sn watanielewa, machawa wata-dislike
Kabisa huyu ndio chanzo cha matatizo ya kutengeneza miungu watu! Untouchable
 
1 week before hili janga. Nilipita mitaa ya kariakoo kutafuta bidhaa kuna jengo lilikua katika ujenzi limepigwa zile wavu ila ghafla kuna kitu kilianguka - usalama wa ujenzi wa haya majengo ni wa kushika mkononi
 
Kitu kuwepo au kutokuwepo si suala la imani.

Ni suala la uhalisia.

Ukiamini kuwa wewe ni Elon Musk tajiri wa kwanza wa dunia hii, wakati wewe si Elon Musk, imani hiyo haikufanyi uwe Elon Musk tajiri wa kwanza wa dunia hii.

Unaelewa hilo?
Mkuu napokwambia mambo ya imani hayana ithibati ya kisayansi namaanisha si rahisi ama lah hayawezi kabisa kuthibitishwa moja kwa moja.

Binafsi naelewa unachomaanisha na kukiongelea humu jf mara nyingi ila sikubaliani na wewe kwa mambo mengi.
 
Wapi nimesema nataka kumuona kwa macho?

Wapi nimesema nataka nimguse?

Wapi nimesema nataka nimhisi?

Unajua kusoma kwa ufahamu wewe?
Sio mpaka useme ila ndivyo sayansi inavyotaka, au labda wewe unataka uthibitishe vipi nje ya hivyo ndgu??
 
Mkuu napokwambia mambo ya imani hayana ithibati ya kisayansi namaanisha si rahisi ama lah hayawezi kabisa kuthibitishwa moja kwa moja.

Binafsi naelewa unachomaanisha na kukiongelea humu jf mara nyingi ila sikubaliani na wewe kwa mambo mengi.
Hujanijibu swali langu.

Unajuaje hili ni jambo la imani la kweli ila halina ithibati ya kisayansi tu, na hili ni jambo lisilo na ithibati ya kisayansi kwa sababu ni uongo tu?

Kwa mfano, nikikuambia mimi Kiranga ndiye Mungu muumba wa vyote, niamini, hili ni jambo la kweli la kiimani ila halina ithibati ya kisayansi tu, utaamini?
 
Lazima, lazima ahukumiwe, kwani akiachwa hivi hivi ni kosa kubwa sana, sbb habari zilizoko Kkoo na mitaani ni kuwa alianza ujenzi ambao ni hatari sana kwa kufukua msingi wa ghorofa akitaka kuongeza underground floors ili apate vyumba vingine apate fedha zaidi na ikumbukwe, huwezi fanya ujenzi wa hivyo, ni hatari sana na hakuna kibali cha ujenzi wa aina hiyo, so alifanya ujenzi kiuhuni, kizembe na kusababisha janga kubwa na baya sana kwa Taifa letu, na janga kama hili lingeweza epukika, ni uhuni na upuuzi mkubwa kafanya, kaua watu na huzuni kubwa kwa watanzania wote, hivyo lazima sheria ichukue mkondo wake ili wengine wasidhubutu kamwe kufanya ujenzi wa aina hiyo..!!
Hii yote inatokana na watanzania wengi kupenda kuishi kwa ujanja ujanja.

Watanzania wengi wanapenda kuishi kwa janja janja, Bila kufuata utaratibu na sheria.

Ndio maana tunakufa sana kama kuku.

Kuishi kwa mazoea, siasa, ujinga uzembe na hizi janja janja zitaendelea kugharimu uhai wa watanzania mpaka pale akili zitakapo funguka.
 
Kwa akili km zako lzm waafrika tutawaliwe Tena , badala ya kuhimiza maboresho kwenye taasisi husika , ww ndo kwanza unawapa hamasa kuwa hakuna namn ya hv walivyoperfom kwenye hili jengo
Maafa hayana mbabe, sina wa kumtetea wala kumkingia kifua ila majanga ya namna hii hata nchi zilizoendelea zinasanda tu mkuu.

Tuhumize kweli wawekeze kwenye miundombinu imara ya uokoaji, ila amini hakuna mbabe katika hili.
 
Back
Top Bottom