KERO Sehemu ya Kuabudia Airport izingatie Dini zote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Uliwahi kua mkristo?Nani anakupa mamlaka ya kuona wengine wana mahitaji makubwa kuliko wengine?Au kwa sababu huwa wananyamaza tu?Ligi itoke wapi wakati mnatolewa tongotongo?
 
Utaachwa na ndege ndugu yangu! Kuna misa ya dakika 5 kwani?
Umewahi kwenda makanisa ya RC kwenye zile sala za asubuhi siku za kati za juma na saa sita mchana?Acha kupotosha.Tutaandika na mengine mchukie.Tofautisha kati ya sala na maadhimisho ya misa.
 
Ukitaka kuabudu kaabudie nyumbani kwako, msituletee ujinga.

Taifa lolote likiendekeza sana watu wa dini mnakuwa kama wote ni wapumbavu. Ndio maana Kagame anafunga makanisa.

Kuna watu wao wanachotaka ni dini tu na kuabudu, watataka hadi kwny treni watengenezewe misikiti na makanisa.

Mkiwachekea hao watu mnavuna mabua!
 
Uliwahi kua mkristo?Nani anakupa mamlaka ya kuona wengine wana mahitaji makubwa kuliko wengine?Au kwa sababu huwa wananyamaza tu?Ligi itoke wapi wakati mnatolewa tongotongo?
Katika huo ukatoliki mtu akiacha hizo sala anapata dhambi? Nijibu kwa mujibu wa ukatoliki.
 
Katika huo ukatoliki mtu akiacha hizo sala anapata dhambi? Nijibu kwa mujibu wa ukatoliki.
Kama kuna hadi slogan ..."Sala na kazi"...wewe kwa tafsiri yako unadhani ni kitu kidogo kwao?Si hivyo tu.Sheria mojawapo za kanisa RC inalazimisha waamini wake wahudhurie maadhimisho ya misa(sala)unadhani kwa nini?
 
Umewahi kwenda makanisa ya RC kwenye zile sala za asubuhi siku za kati za juma na saa sita mchana?Acha kupotosha.Tutaandika na mengine mchukie.Tofautisha kati ya sala na maadhimisho ya misa.
Hizo sala ni lazima kwa wakatoliki? Yaani katika mafundisho yao wanaambiwa ni lazima wazisali na anayeziacha anapata dhambi?
 
Kama kuna hadi slogan ..."Sala na kazi"...wewe kwa tafsiri yako unadhani ni kitu kidogo kwao?Si hivyo tu.Sheria mojawapo za kanisa RC inalazimisha waamini wake wahudhurie maadhimisho ya misa(sala)unadhani kwa nini?
Narudia tena. Hizo sala ni lazima kwa mujibu wa ukatoliki na anayeziacha anapata dhambi?
 
Ndiyo maana serikali inapaswa kujiweka kando na imani za watu. Halafu hai akina Mwamposa kwanza siyo Churches bali ni Ministries, pili ni state made churches/ministries. Serikali kupitia mikakati na mikino yake inajenga baadhi ya dini huku ikibomoa nyingine
 
Utajenga makanisa mangapi kwenye airport?
TAG, KKKT, RC, PENTECOSTE, AIC, EAGT,FBF, Kila mmoja atataka sehemu yake ya kuabudia. Si itakuwa fujo
Kwani kwenye hiyo airport pia kumejengwa misikiti miwili(2) ya Sunni na Shiya ?
 
Msikiti upi?
Sunni au shia?
Nani aliyekudanganya kubwa waislamu wana dhehebu moja?
 
Nani aliyeweka hayo mapumziko? Mkiamua kufanya kazi pasipo kupumzika hiyo ni nyie. Mkiamua kubadili siku hiyo ni nyie. Msingi wa mapumziko Jumamosi na Jumapili ni sababu babu ni weekend siyo kwa sababu ni Church days.
Wakristo wana Misa za kila siku asubuhi (siyo ibada, naongelea misa), hilo najua itakuwa ni mara yako ya kwanza kulisikia tangu uzaliwe. Wakatoliki wanapaswa kusali sala hizi katika utarayibu wao;
  • Matins (Office of Readings)
  • Lauds (Morning Prayer)
  • Terce, Sext, None (Midmorning, Midday, Midafternoon Prayers)
  • Vespers (Evening Prayer)
  • Compline (Night Prayer)
Hizi ni sala ambazo wanapaswa kusali kila muda unapowadia.

Halafu kuna The Angelus Prayer “Angelus Domini." Hii husaliwa 6 AM, noon, na 6 PM, na muda wote wa sala hii huwa inasindikizwa na mlio wa kengele, nadhani umewahi kusikia Kengele zikilia asubuhi, mcjana na jioni. Kila usikiapo kengele za Kanisa muda huo basi ujue ni muda wa kusali
 
sasa mkuu wakisema wajenge kanisa watajenga la wakatoliki? pentekoste? africa inland church? kiboko ya wachawi? at least wenzetu wanawza sali msikiti wowote na inajulikana wana swala kadhaa kwa siku.
Mambo mengine ya kuacha yapite tu ni jamii kukubaliana tu
 
Kutumia Hela ya wananchi kujenga nyumba za ibada za watu Fulani ni ujinga
 
Uliwahi kua mkristo?Nani anakupa mamlaka ya kuona wengine wana mahitaji makubwa kuliko wengine?Au kwa sababu huwa wananyamaza tu?Ligi itoke wapi wakati mnatolewa tongotongo?
Wewe ni mdini na una roho ya kwanini. Safisha nafsi yako utakuwa na amani.
 
Huo ni ujinga , airport sio sehemu ya ibada hakuna haja ya kuweka sehemu ya kuabudia kwa dini yeyote ile , wakianza huo upuuzi basi na wale wengine nao watadai maana ni haki yao pia , maana kwa style hii watajenga kila mahali penye mradi wa serikali na hapo sasa ndipo serikali inapo geuka kuwa wakala wa dini fulani serikali iachane na hizo mambo zitaamsha migongano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…