Ndugu vita ni intelligensia sio kurushiana mabomu na risasi. IDF kwa wakati mmoja kapigana na Hamas, Hezbollah na Houths kachakaza wote kaamua kwenda kulianzisha kwa baba yao kachakazwa naye. Bado ana uwezo wa kufanya kila anachojisikia kwenye anga ya adui huyo mtu unamchukuliaje?
Vita haikuanza Oct 07 ya Hamas, au usidhani ile siku IADF aliporusha drones kwenye kushambulia nyuklia sites za Iran ndio vita ilianza, kulikua mikakati na mbinu mbalimbali yawezekana miaka hata miwili nyuma. Kwahiyo nikisema huyu anapigana vita mwaka mzima unielewe
Mbona unadanganya sana we jamaa!?
Israel katika vita zote alizoanzisha AMEFELI na kupata hasara kubwa.
1.Vita na Hama,Israel lengo lake lilikua kurudisha mateka na kuwaangamiza Hamas.Mateka hawakurudi na Hamas bado wapo imara.Israel iliishia kupoteza Askari zaidi ya 10k na walemavu wa kudumu 120k katika jeshi.
2.Vita na Hizbollah ilisababisha kuteketezwa kambi ya Galilee nzima na kufa askari wasio na idadi isiyojulikana na raia takriban 300k kuwa internally displaced.Israel ikaanza kushambulia Central Lebanon na kuacha vita South Lebanon hali iliyopelekea Serikali kuu kumshurutisha Hizbollah akubali ceasefire kupitia US na France.
3.Houthi waliowashambulia ni USA sio Israel.
Tukija vita hii ya sasa na Iran ISRAEL IMEPIGIKA KULIKO KUWAHI KUUNDWA KWA HILO TAIFA.
millitary camps nyingi zimelipuliwa,vituo vya uwekezaji vingi vimelipuliwa na iron dome imefeli kufanya kazi yake.Malengo ya Israel yalikua kulipua uwezo wa makombora wa Iran unlucky Iran inahifadhi makombora kwenye mahandaki na ina missile launchers chini ya mahandaki HUWEZI kuyafikia.Lengo lingine lilikua kuvunja uwezo wa nuclear enrichment wa Iran ila umefeli na taarifa zinathibitisha wamerudishwa miezi michache nyuma tu kwenye kuendelea na urutubishaji.Lengo la mwisho ilikua kuubadili utawala ila nalo limeshindikanika.
Msitudangaye kuwa eti Israel ilitawala anga la Iran ilhali tulikua tunaona ADS za Iran zikifanya kazi licha ya kuwa kwa kiwango fulani zilizidiwa.
Tena hapo USA amekua akimsaidia Israel kwenye hii vita kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Mtake msitake Israel safari hii AMEFELI pakubwa,Kila mtu aliona,hata maafisa wa jeshi wastaafu walikiri kuwa Israel kwa mwenendo huu atafeli.
Mwisho aliyeomba amani ni Israel sio Iran.
Msitudangaye aisee tunajielewa.