Lend lease kwa Soviet Union ilikuwa ni msaada. Marekani ilitoa ndege za kivita zaidi ya 10,000 na vifaru zaidi ya 6,000 pamoja na mambo mengine kwa Urusi na haikuwa loan
Lend or lease. Marekani alikuwa anaweza kuchukua kitu chochote cha kutumia kwenye vita ile dhidi ya Nazi Germany ila sababu Urusi haikuwa na lolote la hadhi ya kuchukuliwa na Marekani, na Marekani ilijitosheleza ndio maana Urusi ikapokea tu kama Burundi inavyopokea misaada. Baadae mkataba ni wa kukodisha na kukodi, aya umekodisha ndege bure na umeziharibu au zimeharibiwa na adui, zilipe. Ndio hapo nchi zikailipa Marekani tena kwa riba ndogo sana, kwa msamaha wa deni na kwa kupewa miaka hata 40. Tabia za superpower hizo.
Taiwan ina privilege ya kuuziwa baadhi ya silaha za Marekani zisizowekwa open market. Sio kila mwenye hela anaenda US kumwaga mabilioni kununua silaha, kwa miaka kadhaa US iliblock Turkey kununua F-16 mpya mpaka mwaka huu, vilevile Turkey ilikataliwa kuuziwa Patriot ikaenda kununua S-400, Turkey hiyohiyo ilitolewa kwenye mradi wa F-35 ikarudishiwa hela. US hawauzi silaha kwa njaa.
Pia Taiwan inapewa misaada kama training ngumu ambazo sio kila nchi inapewa, na zina gharama kubwa. Inahesabika in monetary terms.