Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Mpaka na mimba zilizoharibika..🀣
Wana mgomo au..?
 
Sijahesabiwa na hawatanihesabu.

Tozo zetu zimeliwa bure.

Tujiandae kupokea data za kukaangwa
 
Elezea kwa mapana,mi nakumbuka ilikua siku moja,makarani wakawa wamehitimisha,hizo wiki mbili labda kama walipigiwa simu baadhi ya makarani,kuendelea na zoezi.
 
Sensa ya nyuma makarani na Wasimamizi 100% walikuwa walimu ambao waliweza kujiongeza mfano unamuona mtu amesimama vizuri amekaa vizuri anasikia anaongea viungo unaona Kuna haja Gani ya kumuuliza ana ulemavu?
Sasa Kuna watu Wana bifu na walimu wanaona wakiwapa kazi watafaidi sana ndio ikawa hivi ilivyo
 
Mimi mpaka sasa sijahesabiwa mimi na watu wengine kama 10 niliokaa nao haa
 
Zoezi ni gumu na Kwa manpower waliyoiweka , ili likamilike Kwa usahihi inahtaji walau 2 weeks, sasa mtu tuu anaropoka kwenye media , kila karani afikie Kaya 100, Jana kuna karani kafika Kwa mganga wa kienyeji hyo ni Kaya moja , ina watu 50 na wengi ni wamama ambao maswali Yao yanaongezeka kaanza sa sita mchana kamaliza sa 11 jioni , kajikuta sku nzima kahoji Kaya 5 tuu,

Karani mwingine anafumania gap la wapangaji ambao ni Kaya ya mtu mmoja au wawili , unajikuta ndani ya masaa matatu kahoji Kaya 10 , .....hili zoezi linaenda pamoja na accuracy pamoja na efficiency , ukiwaforce Sana makarani wanakuwa wanaskip baadh ya maswali ili wakuridhishe kuwa zoez limekamilika ..

Hawa viongozi wengi wa NBS hasa hawa mama zero kabisa , zoezi nyeti wanaleta matamko ya kisiasa,.......
 
Kwani sensa haikupangiwa bajeti au pesa zimeishaliwa?
 
No Sense ni mfumo uliotumika ndo mbaya.
 
HApo hawataweza kupata takwimu za uhakika kamwe, kuna watakao kua hawajahesabiwa siku za nyuma wataamkia sehemu ambazo wameshahesabiwa, Data zitakazopatikana hazitakua sahihi
 
14 kulikuwa na kaya ngapi?
Inaonesha wewe si mwana mahesabu. Kaya za 2012 kwa vyovyote zilikuwa chache kuliko za 2022. Sensa inaweza kuchukua siku moja ila gharama yake itakuwa kubwa. Usisahau kama hii sensa inachukua siku 7 ungaliweza kuongeza wahesabuji 7 wakifuatana na guides 7 kwa siku moja. Ila kuna gharama za Vishkwambi vitaongezeka, gharama za mafunzo zitaongezeka etc.

Kwa ufahamu zaidi, Sensa huwa ni siku moja tu, ikizidi moja, matatizo yanajitokeza bwashee
 
Walikudharau
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Inawezekana karani alinidharau kwelii kwa maana ni mtu wa apa apa kitaa ananifaham la pili siku ya kuanza zoezi la sensa hakupita home alikuja siku ya pili ambapo pia home hapakuwa na mtu ikabidi anifuate kwenye mishe zangu ninapopigia kaz na pia akamfuata wife kwao ukweni walikua na harus akaenda kumalizia kuhesabia uko siku ya sensa tulilala watu 4 so wengine wote akawakuta uko uko nao haikuchukua ata dakik 10 akanambia amemaliza
 
Kuna ujinga mkubwa sana umefanyika katika hili zoezi na hapa ndio tunamkumbuka Magufuli kwani ufujaji wa pesa mkubwa sana umefanyika kwa kuandaa semina nyingi zisizo na tija zaidi kulipana posho tu ndio kilizingatiwa hakuna kingine mpango kazi ulibuniwa kwa ajiri watu wajilipe siyo ufanisi upatikane mpaka sasa zoezi la sensa limeharibika hakuna uhalisia vijana uko field wamechoka wanajaza tu dataπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Naimani mwamba angekuwa hai hapo NBS angetumbua wote kwa uzembe uliofanyika na watu wangeshangaa hao NBS wangekuwa ofisini wanapokea data tu uku mtaani tungehesabiwa na watendaji wa mitaa na wenyeviti wa nyumba kumi kusingekuwa na mfululizo wa semina zisizo na tija na kuandaa maswali mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…