Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Sidhani kama kweli dhamira yao SENSA, maswali ni mengi sana na yasiyo na mlengo wa Sensa ya watu, na ndio maana wanatumia muda mrefu sana kwenye kaya moja,
Baadhi ya maswali yanafikirisha na kukera,
-mimba zilizoharibika!!!! Ngapi!!
-Umewahi kuolewa!!! Mara ngapi!!
Hapo tukajikuta tumeanzisha mjadala mwingine wa yeye kuulizwa badala ya yeye kuuliza.
Wapewe mwezi mzima ndio watawafikia kaya zote kwa hilo zoezi wanalofanya.
Mpaka na mimba zilizoharibika..🤣
Wana mgomo au..?
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Paskali
Sijahesabiwa na hawatanihesabu.

Tozo zetu zimeliwa bure.

Tujiandae kupokea data za kukaangwa
 
Elezea kwa mapana,mi nakumbuka ilikua siku moja,makarani wakawa wamehitimisha,hizo wiki mbili labda kama walipigiwa simu baadhi ya makarani,kuendelea na zoezi.
 
Sensa ya nyuma makarani na Wasimamizi 100% walikuwa walimu ambao waliweza kujiongeza mfano unamuona mtu amesimama vizuri amekaa vizuri anasikia anaongea viungo unaona Kuna haja Gani ya kumuuliza ana ulemavu?
Sasa Kuna watu Wana bifu na walimu wanaona wakiwapa kazi watafaidi sana ndio ikawa hivi ilivyo
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Paskali
Mimi mpaka sasa sijahesabiwa mimi na watu wengine kama 10 niliokaa nao haa
 
Zoezi ni gumu na Kwa manpower waliyoiweka , ili likamilike Kwa usahihi inahtaji walau 2 weeks, sasa mtu tuu anaropoka kwenye media , kila karani afikie Kaya 100, Jana kuna karani kafika Kwa mganga wa kienyeji hyo ni Kaya moja , ina watu 50 na wengi ni wamama ambao maswali Yao yanaongezeka kaanza sa sita mchana kamaliza sa 11 jioni , kajikuta sku nzima kahoji Kaya 5 tuu,

Karani mwingine anafumania gap la wapangaji ambao ni Kaya ya mtu mmoja au wawili , unajikuta ndani ya masaa matatu kahoji Kaya 10 , .....hili zoezi linaenda pamoja na accuracy pamoja na efficiency , ukiwaforce Sana makarani wanakuwa wanaskip baadh ya maswali ili wakuridhishe kuwa zoez limekamilika ..

Hawa viongozi wengi wa NBS hasa hawa mama zero kabisa , zoezi nyeti wanaleta matamko ya kisiasa,.......
 
Twende pole pole jamani. Hivi mnajua hawa makarani wanalipwa kimafungu mara hawa wamelipwa hivi mara hawa wamelipwa vile na yamkini wapo kata moja na wametofautiana AE na wanajaza dodoso la aina moja. Tusiwalaumu makarani kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo.
Kwani sensa haikupangiwa bajeti au pesa zimeishaliwa?
 
Honestly, kwa nchi kama Tanzania huwezi kufanya sensa kwa siku moja unless kama unakusudia kufanya survey na sio sensa!!

Assume una Makarani 200K wanaotakiwa kuwafikia watu 50M... hapo ina maana kila karani anatakiwa kuwafikia watu 50M/200K = 250

Again, assume unatumia dakika 10 kwa kila mtu... yaani una-include muda wa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Hiyo maana yake kila karani atatumia Dakika 2500 kuwafikia hao watu 250.

Dakika 2500 ni sawa na saa 41... NONE STOP ambazo ni almost 4 days for 10 hours per day!!

That being said, kama siku za nyuma sensa zilikuwa zinachukua siku moja, basi tulikuwa tunapigwa manake hata hizo dakika 10 nilizotaja, ni impractical.
No Sense ni mfumo uliotumika ndo mbaya.
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Paskali
HApo hawataweza kupata takwimu za uhakika kamwe, kuna watakao kua hawajahesabiwa siku za nyuma wataamkia sehemu ambazo wameshahesabiwa, Data zitakazopatikana hazitakua sahihi
 
14 kulikuwa na kaya ngapi?
Inaonesha wewe si mwana mahesabu. Kaya za 2012 kwa vyovyote zilikuwa chache kuliko za 2022. Sensa inaweza kuchukua siku moja ila gharama yake itakuwa kubwa. Usisahau kama hii sensa inachukua siku 7 ungaliweza kuongeza wahesabuji 7 wakifuatana na guides 7 kwa siku moja. Ila kuna gharama za Vishkwambi vitaongezeka, gharama za mafunzo zitaongezeka etc.

Kwa ufahamu zaidi, Sensa huwa ni siku moja tu, ikizidi moja, matatizo yanajitokeza bwashee
 
Walikudharau
😂😂😂 Inawezekana karani alinidharau kwelii kwa maana ni mtu wa apa apa kitaa ananifaham la pili siku ya kuanza zoezi la sensa hakupita home alikuja siku ya pili ambapo pia home hapakuwa na mtu ikabidi anifuate kwenye mishe zangu ninapopigia kaz na pia akamfuata wife kwao ukweni walikua na harus akaenda kumalizia kuhesabia uko siku ya sensa tulilala watu 4 so wengine wote akawakuta uko uko nao haikuchukua ata dakik 10 akanambia amemaliza
 
Kuna ujinga mkubwa sana umefanyika katika hili zoezi na hapa ndio tunamkumbuka Magufuli kwani ufujaji wa pesa mkubwa sana umefanyika kwa kuandaa semina nyingi zisizo na tija zaidi kulipana posho tu ndio kilizingatiwa hakuna kingine mpango kazi ulibuniwa kwa ajiri watu wajilipe siyo ufanisi upatikane mpaka sasa zoezi la sensa limeharibika hakuna uhalisia vijana uko field wamechoka wanajaza tu data😂😂😂

Naimani mwamba angekuwa hai hapo NBS angetumbua wote kwa uzembe uliofanyika na watu wangeshangaa hao NBS wangekuwa ofisini wanapokea data tu uku mtaani tungehesabiwa na watendaji wa mitaa na wenyeviti wa nyumba kumi kusingekuwa na mfululizo wa semina zisizo na tija na kuandaa maswali mengi
 
Back
Top Bottom