Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Si kweli, Sensa ya 2012 nilipata kibarua NBS, ilikuwa wiki 2. Siku kadhaa (zaidi ya wiki) za kujaza madodoso field i.e mnaita kuhesabiwa, then baada ya kumaliza siku za field karani anakaa sehemu kama siku 3 kufunga hesabu zake, then msimamizi wa makarani (huyu alisimamia kama makarani 10) anatumia siku kadhaa ku-compile ripoti za makarani wake na kuziwasilisha Katani. Kwenye kata wanazituma jimboni, jimbo to H/shauri....

Hii ya sasa kila kitu kinakamilika kila jioni tena kwa dk 1 tu.
 
No Sense ni mfumo uliotumika ndo mbaya.
Na huo mfumo mzuri unakuwaje?! Au ndo huu πŸ‘‡ πŸ‘‡ πŸ‘‡ πŸ‘‡ πŸ‘‡
Mfumo waliyoitumia kwenye sensa ni mbovu.wangewatumia watendaji ambao ndo haswa wanawajua watu wao zoezi lingekuwa rahisi.
Hivi unawajua Maafisa Watendaji?! Hivi unafahamu kwamba Afisa Mtendaji ni Mwajiriwa na most likely wala sio mwenyeji wa eneo husika?! Sasa anawafahamu vp hao wakazi wake?! Au unazungumzia vijijini, tena vijiji vidogo?

Au unadhani Wakazi kumfahamu Afisa Mtendaji wao ni sawa na Afisa Mtendaji kuwafahamu wakazi wake?

Lakini hata kama akiwafahamu hao watu wake, zoezi linaanzaje kuwa rahisi?! Mtaa/kijiji kimoja kuna maafisa watendaji wangapi?!

Tuachane na mjini, na turudi vijijini kwenye population ndogo, na reference hapa ni kijijini kwetu walipo Maafisa Watendaji 4, na kwa mujibu wa sensa ya 2012, kijiji chetu kizima kilikuwa na roughly watu 10K... hapo sijataja kata mzima!

Sasa kama 2012 kulikuwa na Wakazi 10K, leo 2022 kutakuwa na Wakazi wangapi? Kwahiyo unataka kutuambia kwa Wakazi wote hao kazi ingekuwa rahisi endapo ingefanywa na Maafisa Watendaji ambao ni wa-4?
 
Kuna kitu kweli hakipo sawa huko juu, ila ukiachana na changamoto zote na wananchi nao sasa,niliona mahali mtu anapoulizwa hayo maswali hadi ajibu siyo muda huu,swali moja tu Tena dogo linachukua muda mrefu kujibika hasa vijijni,maswali mengine huitwa watu kutoka ndani Mara fulaaani weeee njoo apa unikumbushe, taaabu kweli kwa hao makarani na ukiongeza na uchovu wa kukosa baadhi ya malipo basi ni mwendo wa kuuliza maswali kumi yaliyobaki wanakadiria tu.
 
Nice idea:

Nafikiri wangeweka option ya collection of GPS mwanzoni kabisa kabla ya kufungua dodoso ni rahisi zaid kuliko kupiga picha.

I am not sure kama ipo au haipo.
 
Ni lini uliwahi kuona sensa ina maswali 100? Waziri mkuu alihojiwa Kwa dakika 35 he vipi Kwa mtu ngumbaru atahojiwa Kwa muda gani.

Kazi za takwimu zitenganishwe na sensa, ujinga uliofanywa na serikali ni kuchanganya kazi za takwimu kujumuisha na sensa ya watu vifanyike Kwa pamoja.

Hawa vijana wetu waliopata hizi nafasi za ukarani ilibidi waajiliwe au wawe na mkataba wa kuitwa kila baada ya muda Fulani kukusanya takwimu, hii siyo sensa ni uhuni serikali imefanya.
 
Sensa ya 2012 walimu waligoma ila baadae walilegea wakaja kwenye dodoso fupi.Ila lile dodoso refu walifanya form six leavers na wanachuo waliokua likizo wakati ule.

Lile zoezi lilikua interesting sana halafu kulikua na pressure kwa vijana kuzingua lakini tulifanya vizuri (speaking from my experience)

Not sure kama makarani wa mwaka huu wamefurahia hili zoezi.
 
Sensa kwa siku zaidi ya moja haijaanza leo mkuu. Hata miaka iliyopita ilifanyika zaidi ya siku moja.

Inasikitisha kuona watu wengi hawafahamu historia ya nchi.
2012 ilianza tarehe 26 Aug-1 sept
Vivyo hivyo 2002.

Tatizo ni kwamba kwa sasa imekuwa kisiasa zaidi.

Picha kwa hisani ya google!
 
Tulishasema hii sio sensa ni interogation...

Mtu unaulizwa masswali ambayo hayana msingi wowote, yani unaulizwa data ambazo ndani ya mwaka au miezi zitakuwa useless.
 
Inasikitisha sana hujui hata umeandika nini, halafu waweza kukuta huyu ni sehemu ya watu wa serikali hopelessness kabisa.
 
 
Kwanza ni km hawakujiandaa na mfumo wao wa kidigitali tukumbuke kn maeneo tanzania network ni shida karani wa sensa Hadi anapanda juu ya mti pili wingi wa maswali unaconsume muda tena ni unnecessary questions eti nyumba yako ni ya nyasi au bati wkt karani anaona kabisa tatu usafiri makarani wengi ni wavivu kutembea wengi wao jua likiwaka kidogo tu wanachili sehemu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ lingine speed and accuracy vishikwambi ni vigeni sasa kufeed data karani anakuwa slow balaa
 
Paka now sijahesabiwa. Labda kuna msamalia mwema kanijumuisha kwenye kaya yake
 
Dodoso lina maswali mengi mno, na miongoni mwa hayo maswali yanaleta maswali zaidi kutoka mlengwa kwenda kwa karani. Muda unaotumia karani kumuhoji mtu mmoja utakuta inachukua zaidi ya hata saa moja.
Mi mbona nilitumia dk 7 tu kujibu!!
 
Unakuta mtu anatoka hapo alipolala hiyo tarehe 23, anasafiri kwenda mji mwingine kwenye kaya ambayo walishahesabiwa. Nadhani kuna udhaifu mkubwa sana kwenye hili zoezi. Walipaswa kuwa na information chache ili zoezi lifanyike siku moja. Nina uhakika watu wengi hawatahesabiwa.
 
HApo hawataweza kupata takwimu za uhakika kamwe, kuna watakao kua hawajahesabiwa siku za nyuma wataamkia sehemu ambazo wameshahesabiwa, Data zitakazopatikana hazitakua sahihi
Wanauliza Hadi no ya simu babu,we ibukia popote lakini hutoongezwa Wala kupunguzwa...dizaini huna idea na takwimu
 
Hawahesabu watu tu..ndiyo maana wanauliza Hadi laptop na mashamba
 
Inasikitisha sana hujui hata umeandika nini, halafu waweza kukuta huyu ni sehemu ya watu wa serikali hopelessness kabisa.
Mie najua nilichoandika na ndio maana kabla hata ya sensa kuanza nilituma hii thread humu. Sema wengi hawakuelewa.

Na nilimtag PM kule twiter ili awafahamishe watu kuwa mapumziko hayana tija sana kwasababu sensa ni zaidi ya siku moja! Na nikasema siku great thinkers wakiamka usingizi watajua nini nilimaanisha!

Washauri wengi wa viongozi wa nchi hii hawana taarifa za kutosha na pengine hufanya mambo kwa mihemko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…