Sensa: Kianalogia siku 1, kidigitali siku 7! Could there be something wrong somewhere?! Kesho mwisho! Je, ambao bado hawajafikiwa watahesabiwa?!

Kiukweli hakuna mwaka ambapo sensa ilifanyika siku 1 tu hapa TZ
Sensa ya 2012 ilifanyika week 2 kabisa

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Mwaka 2012 na miaka yote ya nyuma kuhesabiwa ilikuwa siku moja tu siku zingine zilikuwa ni maandalizi ya kutoa ripoti. Tena miaka ya nyuma watu waliendelea na kazi zao kama kawaida siyo kama mwaka huu ilitangazwa kabisa kuwa siku ya mapumziko. Tukubali tu kuna tatizo ili siku za mbele turekebishe.
 
Haha

Mkuu WAPIGAJI wakitaka kulifanya lao, SEBENE lake lazima watengeneze kitu au jambo fulani kama lina ugumu fulani, unafikiri 627 billion, usipotengeneza SEBENE la kununua VISHKWAMBI, WANASIASA KUTREND kwenye mitandao ya kijamii kama wapo serious wanahesabiwa tena wengine wameenda kuhesabiwa VIJIJINI kwenye MAJIMBO yao, wataiba vipi?

Cha kushangaza wamesahau WATANZANIA wa Leo sio kama wale wa miaka arobaini na saba.

Yaani WANASIASA wametuletea kaole(drama) za KISHAMBA, kama fundi MAKENIKA unampelekea gari GEREJI,tatizo anaweza kuliona rahisi, sasa ili akupige pesa nyingi ya MATENGENEZO lazima ataingia uvungu wa gari atatoka, mara atafungua BONETI, mara ataingia ndani kuangalia DASHBOARD, ndio walivyotufanya ili kuhidhinisha UPIGAJI wa zile pesa takribani 627 billion.
 
Wewe si ndio ulikuwa unasifia hili zoezi na mpaka unasema ulitumiwa message na Samia kuwa amehesabiwa ?

Nilikuambia kuwa ukiona kitu chochote nguvu kubwa inatumika kukipa umuhimu jua kabisa kitapuuzwa .

Mnapaswz kuelelewa serikali iko kwenye wiki ya mkwamo wa maswali kutoka kwa wananchi kuhusu tozo kila uchwao na serikali haitaki kutoa majibu na wananchi wameona serikali haina muda nao ipo wazi kuna watu wsmesusia zoezi hili kwa kutotoa ushirikiano kwa namna tofauti tofauti.

Suluhisho ni moja serikali ijitafakari wanannchi wanataka maelezo kuhusu gedha zao na pia wanahitaji waone matunda kutokana na wanachokatwa ila matokeo yake ni inaonekana makato yanakwenda kuwafaidisha watu wale kule wasiolipa kodi kwenye mshahara wao.
 
Mimi walifika kwangu wakakuta milango imefungwa wakaomba Namba Kwa jirani nikapigiwa simu nimeulizwa maswali matatu tu, jina, umri na kazi basii hayo 97 watakuwa wamejiongeza naona mambo mengi Muda mchache
 
Naunga mkono hoja, hili zoezi ni muhimu sana lilipaswa lisimamiwe na kada ya ualimu.

Shida tunawaonea nongwa sana walimu, lakin ndiyo kundi linaloweza fanya kazi kwa moyo na uaminifu.

Wangefanya kwa ufanisi mkubwa sana
Wala sio swala la WALIMU! Swala ni Manpower, Mtu mmoja Maswali yake kwenye kishikwambi ni 100, Akiwa mwanamke yanazidi zaidi ya hapo, imagine umekuta kaya Ina Watu 10 maana yake utawauliza Maswali 1000, kwahiyo hata ukiwa spidi Kiasi Gani huwez kutoboa Kaya zaidi ya 17 Kwa siku. Cha msingi wangepunguza Maswali, maana Kuna wengine ukimuhoji hadi anasinzia na kwenye Mafunzo unafundishwa kudodosa sio kuuliza maswali
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Leo ni Siku ya Sita ya Zoezi la Sensa, Ambao Hatujahesabiwa, Tutahesabiwa Kweli?.

Ama kweli, mkamia maji, hayanywi!, Waswahili walisema, jambo ukilipania saana, haliwi!, inawezekana hii sense, mimi niliipania sana!. Kwa wiki tatu mfulululizo kabla ya sensa, safu yangu hii ya kwa Maslahi ya Taifa, ilijikita kwenye kuhamasisha zoezi la sensa, sasa siku ya sense yenyewe imefika, mimi siku hesabiwa!, leo ni siku ya 6 ya zoezi la sense, bado sijahesabiwa!, kuuliza kama tutahesabiwa kweli ni genuine concern!.

Kuna ka mtindo kamezuka, ukihoji jambo lolote ambalo wewe kwa mtazamo wako unaona haliendi vizuri au haliendeshwi vema, utanyoonyeshewa kidole kuhusu uzalendo wako!. Hii sensa, hatukuanza nayo leo, tena tumeihamasisha kikamilifu.

Sensa nilianza nayo hapa Sensa: Je, kuna ubaya kuwauliza watanzania their hopes & expectations of their government? Niko tayari kuhesabiwa, wewe je? kisha nikaja hapa Agost 23, tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa ili kuiwezesha Serikali kujipanga kimipango mkakati ya SMART, kutuletea maendeleo. halafu hapa Natoa wito Agosti 23 tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa na hapa Sensa: Leo ni leo, Kazi ni Moja tu!, Kuhesabiwa! na hapa Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Nimeshiriki sensa 4, ya mwaka 1978, ya mwaka 1988, ya mwaka 2002 na ya mwaka 2012, sense ya mwaka huu, 2022, ndio sensa yangu ya kwanza, kutohesabiwa siku ya kwanza ya sensa yenyewe!, na mpaka leo naandika hapa, leo ni siku ya 6 tangu zoezi la sensa lianze na bado kaya yangu, au mtaa wangu, haujafikiwa!.

Siku ya sensa niliianza vizuri kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais wa JMT, amenitumia ujumbe mfupi wa maandishi, SMS kuhusu Sensa!, na nikapandisha bandiko humu Just Imagine Umepokea SMS hii "Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha ...."- Ungemjibu nini?
"Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha kushiriki Sensa tarehe 23 Agosti,2022. Nakusihi utoe taarifa sahihi".

Mimi niliupata ujumbe huu, vipi wewe mwenzagu, pia uliupata?. Umejisikiaje kupokea SMS ya Rais wa JMT kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu?.

Nani mwenye kumbukumbu yoyote ya Rais wa JMT kuwahi kutuma SMS yoyote kuhusu jambo lolote at person level "
Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha..."

Si lengo la makala hii kuingilia kazi ya makarani wa sensa, lakini kwa vile sense zote zilizopita, ulikuwa unahesabiwa siku ya kwanza, hivyo ile siku ya kwanza ya sensa, unakuwa umeipania sana, kila ukisikia mlango kugongwa, siku siku zote ni kumtuma dada kufugua geti, lakini siku hiyo ni baba mwenyewe unakwenda kufungua geti ili uwapokee mwenyewe makarani wa sensa, hivyo kusikia tuu geti linagongwa, lao baba mbio kwenda kufugua geti kukaribisha makarani wa sense!.

Kufika getini na kufungua geti… la haula!, kumbe ni mama wa mboga!, nusu ubamize mlango na kutaka kumfurusha mama wa watu kuwa leo hatununui mboga!, mama wa mboga, anamuulizia dada kama leo tunachukua!, kumbe dada kamsikia na kuja getini, tunachukua, pesa utapitia baadae!, dada wa mboga nae kasema, leo nimepita mapema zaidi, ili nimalize mapema na mimi niende kwangu kusubiri kuhesabiwa, hivyo naomba pesa kabisa, maana leo nikipita nimepita sirudi tena njia hii!. Uzuri wa waleta bidhaa wa nyumbani siku huna wataacha na kesho yake watapitia. Hivyo dada akamwambia tunachukua utapitia kesho!, na siku hiyo ndio baba unashuhudia mboga zikinunuliwa, kisa ni kuwasubiri makarani wa sense!.

Kwa vile sensa zote za nyuma, umezoea kuhesabiwa siku ya kwanza ya sensa, sijui kama ilikuwa ni bahati tuu, lakini kaya nyingine zilikuwa zinahesabiwa kwa siku 7, sijui!, lakini sensa hii leo siku ya 6, nina haki ya kujiuliza kama leo au kesho nitafikiwa kweli?.

Hivyo nikaanza kuwaza mbali!. Tanzania tulipopata uhuru ile miaka ya 60, kuna nchi tulipata nazo uhuru pamoja, zikiwemo nchi zinaitwa Tiger, ikiziangalia zilikuwa na nani ukilinganisha na sisi, tuna nini, nchi hizo zilikuwa hazina kitu, na sisi tulikuwa tuna kila kitu, lakini leo ukiziangalia zilipo na sisi tulipo, lazima utakubaliana na mimi, sisi tuna matatizo mahali!.

Sasa nikilinganisha zile sensa nyingine na hii sensa ya leo, kiukweli kabisa wa dhati ya moyo wangu, kuna tatizo mahali!. Hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko mjumbe wake wa nyumba 10, hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko serikali yake ya mtaa, nyumba yangu ni hatua chache kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wangu, haiwezekani leo ni siku ya 6 makarani wa sensa hawanifikia, wakati inawachukua nusu siku tuu kwa watu wa serikali ya mtaa wangu kuwafikia wakazi wote wa mtaa wangu, kwa nini hawa makarani wa sensa hawakuwa ni wajumbe wetu wa nyumba 10 na maofisa wetu wa serikali za mtaa?!.

Kama Tanzania sasa tuna vitambulisho vya taifa, vyenye biometric data, na tuna serikali mtandao, nini faida ya vitambulisho vya taifa vyenye biometric data, na serikali mtandao, kama tunahesabina kijima hivi?!.

Nimemsikia Kamishna wa Sensa kitaifa, Mama Anna Makinda, akisema tungekuwa ni nchi za wenzetu, tungejihesabu na kutuma data, mbona kuna sisi Watanzania wengi tuu tuna simu janja, tuna vitambulisho vya taifa, nchi yetu ina serikali mtandao, si wenye uwezo wa kujihesabu na kutuma data tungetuma, na karani angepita tuu kuhakiki kwa dakika chache, zile sensa za kuhesabiwa ki analojia tumehesabiwa kwa siku moja, leo tunahesabiana kidigitali, tunasubiri siku 6 tuhesabiwe, hapa sio kuna tatizo?!.

Mbona kwenye E Passport tumeweza, E Visa tunaweza, E registrations tumeweza, TRA tunafanya E-Filing, tunashindwa vipi kwenye kitu kidogo kama kujihesabu tuu?.

Pamoja na matatizo yote, kwenye mazuri pia tupongeze, naipongeza Televisheni ya Taifa kutulea matangazo live mubashara ya sensa, tukashuhudia ile siku ya kwanza ya sensa ya viongozi, wakihesabiwa, na mpaka leo wananchi tukihesabiwa. Hongera sana Dr. Rioba na timu yako kwa kazi nzuri.

Kuna uwezekana Dr. Albina Chuwa ame over stay pale NBS, maana sijui huu ni mwaka wa ngapi pale, wenzetu wazungu wana msemo hata uwe mzuri vipi, miaka 10 ni mwisho, na ndio maana hata vipindi vya uongozi mwisho ni miaka 10, wakuu wa taasisi za umma mwisho ni miaka 10, vipi hapo NBS?.

La mwisho, mfumo wa kidigitali unarahisisha sana kazi, tukijenga mifumo imara, hatuhitaji hii duplicity ya Vizazi na Vifo, RITA, Vitambulisho vya Taifa NIDA, Idara ta Takwimu NBS, Immigration, vunja haya makitu yote, centralize all the data katika mfumo mmoja, hata ukusanyaji wa kodi, hakuna tena kushikana mashati!, kila kitu ni streamlined pamoja!.

Nasubiria Kuhesabiwa!.

Wasalaam

Paskali.
Sensa ya mchongo... Data za mchongo!
Wanatamani kuhesabu kila mtu ili wapate tozo lakini pia wanawaogopa WB na "dona kantrez"
Japo wangehesabu wote tungegonga milioni 80+. Kwa sensa hii sidhani ka tutafika hata 70+
 
Zoezi ni gumu na Kwa manpower waliyoiweka , ili likamilike Kwa usahihi inahtaji walau 2 weeks, sasa mtu tuu anaropoka kwenye media , kila karani afikie Kaya 100, Jana kuna karani kafika Kwa mganga wa kienyeji hyo ni Kaya moja , ina watu 50 na wengi ni wamama ambao maswali Yao yanaongezeka kaanza sa sita mchana kamaliza sa 11 jioni , kajikuta sku nzima kahoji Kaya 5 tuu,

Karani mwingine anafumania gap la wapangaji ambao ni Kaya ya mtu mmoja au wawili , unajikuta ndani ya masaa matatu kahoji Kaya 10 , .....hili zoezi linaenda pamoja na accuracy pamoja na efficiency , ukiwaforce Sana makarani wanakuwa wanaskip baadh ya maswali ili wakuridhishe kuwa zoez limekamilika ..

Hawa viongozi wengi wa NBS hasa hawa mama zero kabisa , zoezi nyeti wanaleta matamko ya kisiasa,.......
Kwa mganga[emoji16]
 
Mwaka 2012 na miaka yote ya nyuma kuhesabiwa ilikuwa siku moja tu siku zingine zilikuwa ni maandalizi ya kutoa ripoti. Tena miaka ya nyuma watu waliendelea na kazi zao kama kawaida siyo kama mwaka huu ilitangazwa kabisa kuwa siku ya mapumziko. Tukubali tu kuna tatizo ili siku za mbele turekebishe.
2012 mlihesabiwa siku Moja?
 
Mi nimehisabiwa pamoja na familia yangu, nikamuuliza Mtu wa Sensa Kama kweli umetuhisabu Mimi mpaka Sasa ni no ngapi!? Lakini kashindwa kunitajia no yangu Kama kweli nimehisabiwa!!?? Huu si utapeli!? Mbona Nyumba zetu zote zimehisabiwa na zikapewa no zake kwa kila Mjengo!? Mbona sisi watu hatupewi no zetu Kama kweli tumehisabiwa!!?? Au kuna kitu nyuma ya pazia!? Ni Nani anatafutwa!!??
Usimlaumu karani Kwa kushindwa kujua we ni mtu wa ngapi.Kile kishkwambi kimetengenezewa program,karani ana uwezo wa kujua kuwa kahesabia kaya ngapi,maana kinampa summary ya kaya ila summary ya idadi ya watu imekuwa locked hawezi ona
 
Subiri utahesabiwa. Serikali imeshaziagiza mamlaka za wilaya kutengeneza namba za simu zitakazotumika kutoa taarifa kama hujahesabiwa. Kwahyo ndg yangu Pascal Mayalla kuwa na subra utapata namba ya simu utatoa taarifa km hujahesabiwa

Lkn Siamini kama ni kweli sensa ya mwaka 2012 ilifanyika siku moja.
 
Dah ni kweli kabisa. Umenikumbusha kuhusu mabozi. Mabalozi wa nyumba kumi wote wanawajua watu wao na tena mpaka umri etc. unajua sensa ya safari hii eti mtu anaulizwa una umri gani bila kuthibitisha anatajiwa any age. Nadhani hii sensa ni bonge la failure pamoja na kutumia kiasi kikubwa cha hela. Ninaamini angekuwa Dkt Magufuli angehoji vitu vingi na mabalozi wangeweza kurahisisha zoezi na tena sensa ingefanyika siku moja then hao mawakala wangefanya kazi ya data entry kwa hizo siku zingine.
Hii sensa ukiiangalia Kwa juu juu unaweza ona kama Serikali imefeli,ila kama taarifa zitakusanywa vizuri hii ni miongoni mwa sensa bora kabisa
 
Kiukweli kupitia hii sensa ilipaswa kuwatoa viongozi wote wa NBS na wanasiasa wanaohusika na hii taasisi. Inatia aibu.
Huku mtaani kwangu amekuja karani wa sense kila vipengere 2 anapiga simu juuliza namna ya kuendeleza, nikamtupia jicho la kiufundi nikagundua kuwa bado mwanafunzi wa kishkwambi chake. Wameingiza wadogo zao ujuzi ziro pont. Ni sawa na huko nyuma uandikishaji wa vitambulisho vya utaifa, mtu ana degree ya computer lakini kanyimwa nafasi harafu unakuta mtu na dadaake wamepita wote hata form 4 hawajafika, ukidodosa kumbe wana ukaribu na mtendaji aliekuwa anachuja maombi. Sasa unajiuliza nchi hii tatizo katiba mbovu au urafi wa rushwa!!
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Leo ni Siku ya Sita ya Zoezi la Sensa, Ambao Hatujahesabiwa, Tutahesabiwa Kweli?.

Ama kweli, mkamia maji, hayanywi!, Waswahili walisema, jambo ukilipania saana, haliwi!, inawezekana hii sense, mimi niliipania sana!. Kwa wiki tatu mfulululizo kabla ya sensa, safu yangu hii ya kwa Maslahi ya Taifa, ilijikita kwenye kuhamasisha zoezi la sensa, sasa siku ya sense yenyewe imefika, mimi siku hesabiwa!, leo ni siku ya 6 ya zoezi la sense, bado sijahesabiwa!, kuuliza kama tutahesabiwa kweli ni genuine concern!.

Kuna ka mtindo kamezuka, ukihoji jambo lolote ambalo wewe kwa mtazamo wako unaona haliendi vizuri au haliendeshwi vema, utanyoonyeshewa kidole kuhusu uzalendo wako!. Hii sensa, hatukuanza nayo leo, tena tumeihamasisha kikamilifu.

Sensa nilianza nayo hapa Sensa: Je, kuna ubaya kuwauliza watanzania their hopes & expectations of their government? Niko tayari kuhesabiwa, wewe je? kisha nikaja hapa Agost 23, tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa ili kuiwezesha Serikali kujipanga kimipango mkakati ya SMART, kutuletea maendeleo. halafu hapa Natoa wito Agosti 23 tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa na hapa Sensa: Leo ni leo, Kazi ni Moja tu!, Kuhesabiwa! na hapa Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Nimeshiriki sensa 4, ya mwaka 1978, ya mwaka 1988, ya mwaka 2002 na ya mwaka 2012, sense ya mwaka huu, 2022, ndio sensa yangu ya kwanza, kutohesabiwa siku ya kwanza ya sensa yenyewe!, na mpaka leo naandika hapa, leo ni siku ya 6 tangu zoezi la sensa lianze na bado kaya yangu, au mtaa wangu, haujafikiwa!.

Siku ya sensa niliianza vizuri kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais wa JMT, amenitumia ujumbe mfupi wa maandishi, SMS kuhusu Sensa!, na nikapandisha bandiko humu Just Imagine Umepokea SMS hii "Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha ...."- Ungemjibu nini?
"Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha kushiriki Sensa tarehe 23 Agosti,2022. Nakusihi utoe taarifa sahihi".

Mimi niliupata ujumbe huu, vipi wewe mwenzagu, pia uliupata?. Umejisikiaje kupokea SMS ya Rais wa JMT kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu?.

Nani mwenye kumbukumbu yoyote ya Rais wa JMT kuwahi kutuma SMS yoyote kuhusu jambo lolote at person level "
Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha..."

Si lengo la makala hii kuingilia kazi ya makarani wa sensa, lakini kwa vile sense zote zilizopita, ulikuwa unahesabiwa siku ya kwanza, hivyo ile siku ya kwanza ya sensa, unakuwa umeipania sana, kila ukisikia mlango kugongwa, siku siku zote ni kumtuma dada kufugua geti, lakini siku hiyo ni baba mwenyewe unakwenda kufungua geti ili uwapokee mwenyewe makarani wa sensa, hivyo kusikia tuu geti linagongwa, lao baba mbio kwenda kufugua geti kukaribisha makarani wa sense!.

Kufika getini na kufungua geti… la haula!, kumbe ni mama wa mboga!, nusu ubamize mlango na kutaka kumfurusha mama wa watu kuwa leo hatununui mboga!, mama wa mboga, anamuulizia dada kama leo tunachukua!, kumbe dada kamsikia na kuja getini, tunachukua, pesa utapitia baadae!, dada wa mboga nae kasema, leo nimepita mapema zaidi, ili nimalize mapema na mimi niende kwangu kusubiri kuhesabiwa, hivyo naomba pesa kabisa, maana leo nikipita nimepita sirudi tena njia hii!. Uzuri wa waleta bidhaa wa nyumbani siku huna wataacha na kesho yake watapitia. Hivyo dada akamwambia tunachukua utapitia kesho!, na siku hiyo ndio baba unashuhudia mboga zikinunuliwa, kisa ni kuwasubiri makarani wa sense!.

Kwa vile sensa zote za nyuma, umezoea kuhesabiwa siku ya kwanza ya sensa, sijui kama ilikuwa ni bahati tuu, lakini kaya nyingine zilikuwa zinahesabiwa kwa siku 7, sijui!, lakini sensa hii leo siku ya 6, nina haki ya kujiuliza kama leo au kesho nitafikiwa kweli?.

Hivyo nikaanza kuwaza mbali!. Tanzania tulipopata uhuru ile miaka ya 60, kuna nchi tulipata nazo uhuru pamoja, zikiwemo nchi zinaitwa Tiger, ikiziangalia zilikuwa na nani ukilinganisha na sisi, tuna nini, nchi hizo zilikuwa hazina kitu, na sisi tulikuwa tuna kila kitu, lakini leo ukiziangalia zilipo na sisi tulipo, lazima utakubaliana na mimi, sisi tuna matatizo mahali!.

Sasa nikilinganisha zile sensa nyingine na hii sensa ya leo, kiukweli kabisa wa dhati ya moyo wangu, kuna tatizo mahali!. Hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko mjumbe wake wa nyumba 10, hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko serikali yake ya mtaa, nyumba yangu ni hatua chache kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wangu, haiwezekani leo ni siku ya 6 makarani wa sensa hawanifikia, wakati inawachukua nusu siku tuu kwa watu wa serikali ya mtaa wangu kuwafikia wakazi wote wa mtaa wangu, kwa nini hawa makarani wa sensa hawakuwa ni wajumbe wetu wa nyumba 10 na maofisa wetu wa serikali za mtaa?!.

Kama Tanzania sasa tuna vitambulisho vya taifa, vyenye biometric data, na tuna serikali mtandao, nini faida ya vitambulisho vya taifa vyenye biometric data, na serikali mtandao, kama tunahesabina kijima hivi?!.

Nimemsikia Kamishna wa Sensa kitaifa, Mama Anna Makinda, akisema tungekuwa ni nchi za wenzetu, tungejihesabu na kutuma data, mbona kuna sisi Watanzania wengi tuu tuna simu janja, tuna vitambulisho vya taifa, nchi yetu ina serikali mtandao, si wenye uwezo wa kujihesabu na kutuma data tungetuma, na karani angepita tuu kuhakiki kwa dakika chache, zile sensa za kuhesabiwa ki analojia tumehesabiwa kwa siku moja, leo tunahesabiana kidigitali, tunasubiri siku 6 tuhesabiwe, hapa sio kuna tatizo?!.

Mbona kwenye E Passport tumeweza, E Visa tunaweza, E registrations tumeweza, TRA tunafanya E-Filing, tunashindwa vipi kwenye kitu kidogo kama kujihesabu tuu?.

Pamoja na matatizo yote, kwenye mazuri pia tupongeze, naipongeza Televisheni ya Taifa kutulea matangazo live mubashara ya sensa, tukashuhudia ile siku ya kwanza ya sensa ya viongozi, wakihesabiwa, na mpaka leo wananchi tukihesabiwa. Hongera sana Dr. Rioba na timu yako kwa kazi nzuri.

Kuna uwezekana Dr. Albina Chuwa ame over stay pale NBS, maana sijui huu ni mwaka wa ngapi pale, wenzetu wazungu wana msemo hata uwe mzuri vipi, miaka 10 ni mwisho, na ndio maana hata vipindi vya uongozi mwisho ni miaka 10, wakuu wa taasisi za umma mwisho ni miaka 10, vipi hapo NBS?.

La mwisho, mfumo wa kidigitali unarahisisha sana kazi, tukijenga mifumo imara, hatuhitaji hii duplicity ya Vizazi na Vifo, RITA, Vitambulisho vya Taifa NIDA, Idara ta Takwimu NBS, Immigration, vunja haya makitu yote, centralize all the data katika mfumo mmoja, hata ukusanyaji wa kodi, hakuna tena kushikana mashati!, kila kitu ni streamlined pamoja!.

Nasubiria Kuhesabiwa!.

Wasalaam

Paskali.
Hunalolote unajifalagua tu, kwani mapambio veepe !!!???

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wakikupa uteuzi nageuka kuwa mavi nipo nimekaa pale [emoji117][emoji117][emoji117]
 
Kuna uwezekana Dr. Albina Chuwa ame over stay pale NBS, maana sijui huu ni mwaka wa ngapi pale, wenzetu wazungu wana msemo hata uwe mzuri vipi, miaka 10 ni mwisho, na ndio maana hata vipindi vya uongozi mwisho ni miaka 10, wakuu wa taasisi za umma mwisho ni miaka 10, vipi hapo NBS?.
Upo sahihi kabisa ila hili haliwezi kuathiri ufanisi wa zoezi husika labda unahitaji tu kuona akili mpya kwenye utendaji hapo Nbs.

kwa nini hawa makarani wa sensa hawakuwa ni wajumbe wetu wa nyumba 10 na maofisa wetu wa serikali za mtaa?!.
Swali zuri sana hili maana ingeepusha mkanganyiko wa makarani kutojua vizuri mitaa waliyotengewa kupita au hata kupotea kabisa.

mwisho, mfumo wa kidigitali unarahisisha sana kazi, tukijenga mifumo imara, hatuhitaji hii duplicity ya Vizazi na Vifo, RITA, Vitambulisho vya Taifa NIDA, Idara ta Takwimu NBS, Immigration, vunja haya makitu yote, centralize all the data katika mfumo mmoja, hata ukusanyaji wa kodi, hakuna tena kushikana mashati!, kila kitu ni streamlined pamoja!.
Upo sahihi kabisa naunga mkono hii hoja.
Ila bado asilimia kubwa ya Watz hawana access na huu mfumo wa kidigitali hivyo hiyo sensa unayoiita ya kijima bado ni muhimu itumike.

Maadam sensa itahusisha watu na makazi sio kila kitu kitafanyika kidigitali kwa huku kwetu labda ushauri hii ya kijima ingeenda sambamba na hiyo ya kidigitali ili kufikia kila mtu.
 
Kuna uwezekana Dr. Albina Chuwa ame over stay pale NBS, maana sijui huu ni mwaka wa ngapi pale, wenzetu wazungu wana msemo hata uwe mzuri vipi, miaka 10 ni mwisho, na ndio maana hata vipindi vya uongozi mwisho ni miaka 10, wakuu wa taasisi za umma mwisho ni miaka 10, vipi hapo NBS?.
Sikujua kama ulilenga huku. Hata hivyo, huyo Dada Dr Albina alipewa uhuru wa kufanya maandalizi ya sensa hii kwa Uhuru alioutaka?

Mbali na kutatizika na hoja yako hii ya "kumsagia kunguni" Dada wa watu, ninakupongeza kwa kuuliza swali hili digitali siku 7 na analogia siku 1.

Nilichelea kuuliza swali hili maana uhuru wa kuhoji kwa Sasa unakipimo ambacho sijakikamata sawa.
 
Mi nimehisabiwa pamoja na familia yangu, nikamuuliza Mtu wa Sensa Kama kweli umetuhisabu Mimi mpaka Sasa ni no ngapi!? Lakini kashindwa kunitajia no yangu Kama kweli nimehisabiwa!!?? Huu si utapeli!? Mbona Nyumba zetu zote zimehisabiwa na zikapewa no zake kwa kila Mjengo!? Mbona sisi watu hatupewi no zetu Kama kweli tumehisabiwa!!?? Au kuna kitu nyuma ya pazia!? Ni Nani anatafutwa!!??
Anyway najua hauko serious na hoja yako sensa zote nilizo hesabiwa sikuwahi kupewa namba na hakuna kitu kama hicho kitakuja tokea.
 
Kilichotakiwa kufanyika ni kwanza kuangalia nini hasa kinachohitajika kwenye sensa wanataka ku achieve nini? Kama ilikuwa kufanya research wame fail big time kwa sababu njia zote za ukusanyaji taarifa lazima ziwe na sample standard wangeweza kuwa na dodoso refu na fupi.... wakaamua kaya 6 dodoso fupi kaya 4 fupi.

Au kama walitaka nchi nzima kutuhesabu tungeenda kwenye vituo mahususi sio wao kutufuta tena huko angeenda mkuu wa kaya na taarifa za watu wake basi. Au njia bora zaidi wange fanya sensa kwa kanda hii ingesaidia kupunguza gharama ya muda na vifaa yaani vishikwambi vyote vingekuwa mfano nyanda za juu kusini kwa mwezi mzima then vikimaliza kazi vinahamia kwingine ...sensa hata kama itachukua mwaka mzima na wakakusanya taarifa zote muhimu baada ya mwaka isingekuwa tabu sasa hapa sidhani hata kama 25% ya watanzania tumehesabiwa. Sometimes we need to brain storm as much as we can before hatujaanza project zilizo shindwa kabla ya kuanza.
 
Wanabodi,
Makala ya leo ni Swali
Sensa za nyuma tulihesabiwa Ki Analogia na ilichukua Siku 1 tuu, sasa tunahesabiana Kidigitali inachukua Siku 7!, Could There Be Something Wrong Somewhere?!. Leo ni siku ya 6, kuna kaya hazijafikiwa, kesho ni siku ya 7 ambayo ndio ya mwisho, jee kaya zote zilizobakia zitafikiwa?, Je ambazo hawajafikiwa, mpaka kesho, jee watafikiwa, jee watahesabiwa au ikibidi kuongeza siku moja au mbili, tuongeze wote tufikiwe, wote tuhesabiwe?!
View attachment 2336973View attachment 2336974
Leo ni Siku ya Sita ya Zoezi la Sensa, Ambao Hatujahesabiwa, Tutahesabiwa Kweli?.

Ama kweli, mkamia maji, hayanywi!, Waswahili walisema, jambo ukilipania saana, haliwi!, inawezekana hii sense, mimi niliipania sana!. Kwa wiki tatu mfulululizo kabla ya sensa, safu yangu hii ya kwa Maslahi ya Taifa, ilijikita kwenye kuhamasisha zoezi la sensa, sasa siku ya sense yenyewe imefika, mimi siku hesabiwa!, leo ni siku ya 6 ya zoezi la sense, bado sijahesabiwa!, kuuliza kama tutahesabiwa kweli ni genuine concern!.

Kuna ka mtindo kamezuka, ukihoji jambo lolote ambalo wewe kwa mtazamo wako unaona haliendi vizuri au haliendeshwi vema, utanyoonyeshewa kidole kuhusu uzalendo wako!. Hii sensa, hatukuanza nayo leo, tena tumeihamasisha kikamilifu.

Sensa nilianza nayo hapa Sensa: Je, kuna ubaya kuwauliza watanzania their hopes & expectations of their government? Niko tayari kuhesabiwa, wewe je? kisha nikaja hapa Agost 23, tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa ili kuiwezesha Serikali kujipanga kimipango mkakati ya SMART, kutuletea maendeleo. halafu hapa Natoa wito Agosti 23 tujitokeze kwa wingi kuhesabiwa na hapa Sensa: Leo ni leo, Kazi ni Moja tu!, Kuhesabiwa! na hapa Shuhudia Sensa Live Kupitia TBC, Nimeshuhudia Live Rais Samia Akihesabiwa. Let's Share Experiences za Sensa na Zoezi la Kuhesabiwa Toka Maeneo Tofauti

Nimeshiriki sensa 4, ya mwaka 1978, ya mwaka 1988, ya mwaka 2002 na ya mwaka 2012, sense ya mwaka huu, 2022, ndio sensa yangu ya kwanza, kutohesabiwa siku ya kwanza ya sensa yenyewe!, na mpaka leo naandika hapa, leo ni siku ya 6 tangu zoezi la sensa lianze na bado kaya yangu, au mtaa wangu, haujafikiwa!.

Siku ya sensa niliianza vizuri kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais wa JMT, amenitumia ujumbe mfupi wa maandishi, SMS kuhusu Sensa!, na nikapandisha bandiko humu Just Imagine Umepokea SMS hii "Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha ...."- Ungemjibu nini?
"Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha kushiriki Sensa tarehe 23 Agosti,2022. Nakusihi utoe taarifa sahihi".

Mimi niliupata ujumbe huu, vipi wewe mwenzagu, pia uliupata?. Umejisikiaje kupokea SMS ya Rais wa JMT kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu?.

Nani mwenye kumbukumbu yoyote ya Rais wa JMT kuwahi kutuma SMS yoyote kuhusu jambo lolote at person level "
Mimi Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakukaribisha..."

Si lengo la makala hii kuingilia kazi ya makarani wa sensa, lakini kwa vile sense zote zilizopita, ulikuwa unahesabiwa siku ya kwanza, hivyo ile siku ya kwanza ya sensa, unakuwa umeipania sana, kila ukisikia mlango kugongwa, siku siku zote ni kumtuma dada kufugua geti, lakini siku hiyo ni baba mwenyewe unakwenda kufungua geti ili uwapokee mwenyewe makarani wa sensa, hivyo kusikia tuu geti linagongwa, lao baba mbio kwenda kufugua geti kukaribisha makarani wa sense!.

Kufika getini na kufungua geti… la haula!, kumbe ni mama wa mboga!, nusu ubamize mlango na kutaka kumfurusha mama wa watu kuwa leo hatununui mboga!, mama wa mboga, anamuulizia dada kama leo tunachukua!, kumbe dada kamsikia na kuja getini, tunachukua, pesa utapitia baadae!, dada wa mboga nae kasema, leo nimepita mapema zaidi, ili nimalize mapema na mimi niende kwangu kusubiri kuhesabiwa, hivyo naomba pesa kabisa, maana leo nikipita nimepita sirudi tena njia hii!. Uzuri wa waleta bidhaa wa nyumbani siku huna wataacha na kesho yake watapitia. Hivyo dada akamwambia tunachukua utapitia kesho!, na siku hiyo ndio baba unashuhudia mboga zikinunuliwa, kisa ni kuwasubiri makarani wa sense!.

Kwa vile sensa zote za nyuma, umezoea kuhesabiwa siku ya kwanza ya sensa, sijui kama ilikuwa ni bahati tuu, lakini kaya nyingine zilikuwa zinahesabiwa kwa siku 7, sijui!, lakini sensa hii leo siku ya 6, nina haki ya kujiuliza kama leo au kesho nitafikiwa kweli?.

Hivyo nikaanza kuwaza mbali!. Tanzania tulipopata uhuru ile miaka ya 60, kuna nchi tulipata nazo uhuru pamoja, zikiwemo nchi zinaitwa Tiger, ikiziangalia zilikuwa na nani ukilinganisha na sisi, tuna nini, nchi hizo zilikuwa hazina kitu, na sisi tulikuwa tuna kila kitu, lakini leo ukiziangalia zilipo na sisi tulipo, lazima utakubaliana na mimi, sisi tuna matatizo mahali!.

Sasa nikilinganisha zile sensa nyingine na hii sensa ya leo, kiukweli kabisa wa dhati ya moyo wangu, kuna tatizo mahali!. Hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko mjumbe wake wa nyumba 10, hakuna mtu anaujua mtaa wake kuliko serikali yake ya mtaa, nyumba yangu ni hatua chache kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wangu, haiwezekani leo ni siku ya 6 makarani wa sensa hawanifikia, wakati inawachukua nusu siku tuu kwa watu wa serikali ya mtaa wangu kuwafikia wakazi wote wa mtaa wangu, kwa nini hawa makarani wa sensa hawakuwa ni wajumbe wetu wa nyumba 10 na maofisa wetu wa serikali za mtaa?!.

Kama Tanzania sasa tuna vitambulisho vya taifa, vyenye biometric data, na tuna serikali mtandao, nini faida ya vitambulisho vya taifa vyenye biometric data, na serikali mtandao, kama tunahesabina kijima hivi?!.

Nimemsikia Kamishna wa Sensa kitaifa, Mama Anna Makinda, akisema tungekuwa ni nchi za wenzetu, tungejihesabu na kutuma data, mbona kuna sisi Watanzania wengi tuu tuna simu janja, tuna vitambulisho vya taifa, nchi yetu ina serikali mtandao, si wenye uwezo wa kujihesabu na kutuma data tungetuma, na karani angepita tuu kuhakiki kwa dakika chache, zile sensa za kuhesabiwa ki analojia tumehesabiwa kwa siku moja, leo tunahesabiana kidigitali, tunasubiri siku 6 tuhesabiwe, hapa sio kuna tatizo?!.

Mbona kwenye E Passport tumeweza, E Visa tunaweza, E registrations tumeweza, TRA tunafanya E-Filing, tunashindwa vipi kwenye kitu kidogo kama kujihesabu tuu?.

Pamoja na matatizo yote, kwenye mazuri pia tupongeze, naipongeza Televisheni ya Taifa kutulea matangazo live mubashara ya sensa, tukashuhudia ile siku ya kwanza ya sensa ya viongozi, wakihesabiwa, na mpaka leo wananchi tukihesabiwa. Hongera sana Dr. Rioba na timu yako kwa kazi nzuri.

Kuna uwezekana Dr. Albina Chuwa ame over stay pale NBS, maana sijui huu ni mwaka wa ngapi pale, wenzetu wazungu wana msemo hata uwe mzuri vipi, miaka 10 ni mwisho, na ndio maana hata vipindi vya uongozi mwisho ni miaka 10, wakuu wa taasisi za umma mwisho ni miaka 10, vipi hapo NBS?.

La mwisho, mfumo wa kidigitali unarahisisha sana kazi, tukijenga mifumo imara, hatuhitaji hii duplicity ya Vizazi na Vifo, RITA, Vitambulisho vya Taifa NIDA, Idara ta Takwimu NBS, Immigration, vunja haya makitu yote, centralize all the data katika mfumo mmoja, hata ukusanyaji wa kodi, hakuna tena kushikana mashati!, kila kitu ni streamlined pamoja!.

Nasubiria Kuhesabiwa!.

Wasalaam

Paskali.
Eti bajeti halisi ta sensa ni tzs ngapi??
 
Back
Top Bottom