Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Issue sio kujitawala ni mapato yao wana ya kutosha mfano kagera uchumi unategemea kilimo cha ndizi hasa sasa mikungu mingapi uuze upate pesa ya kujenga barabara? Kilomita moja tu pesa zaidi ya shilingi bilioini moja hapo mikungu mingapi?

Chadema hii sera itaumiza mikoa mingi mno kuwarudisha chini kwenye umaskini wa kufa mtu

Issue sio maamuzi bali ni kwa pesa ipi uliyonayo ya kwako ya source ya eneo lako?

Hiyo ya kuuza ndizi?
 
Vipi unafikiri sera ya nchi katika Afrika Mashariki inaua uafrika mashariki,

Je sera ya nchi Afrika, inaua uafrika,

Je sera ya vijiji inaua uzalendo kikata?

Je, sera ya mikoa nayo inaua utaifa?

Je sera ya kuwa na wilaya, inaua uazlendo kimkoa?

Tumia akili, acha propaganda.
 
Eritrea ilijitenga kutoka Ethiopia sijui kama unakumbuka hilo na sasa ni mwanachama wa AU. Pia kuna Simaliland na Putland zimejimegua toka Somalia huku hiyo AU ikiangalia. Morocco iliivamia Sahara Magharibi kinyume na mkataba wa OAU wakati huo ambao ulikuwa na clause inasema nchi za Africa haziruhusiwi kubadili mipaka iliyowekwa na wakoloni kwa kutumia nguvu. Ndugu yangu ukipenda masuala haya take time kusoma.
 
Hawa wanaokuja na sera za majimbo ndio hao wanaowakejeli watu wa Dodoma kuwa ni maskini mpaka wanakula wadudu.

Ndio hao wanaosema uwanja wa ndege Chato hautakuwa na faida baada ya rais kuondoka ikulu.

Halafu wanataka majimbo hayo yasiyokuwa na chochote yajitegemee!!.

Ni sera ambayo imejificha kwenye moyo wa uchoyo. Watanzania tunategemeana na tumekuzwa katika misingi ya kutegemeana hatuwezi kukwepa kuwa kitu kimoja.
 
Kwako utaifa ni wananchi kuwa mafukara na ombaomba wa magufuli?

Huo ndio utaifa kwa mujibu wa ilani ya CCM?
Mafukara na ombaomba wapo nchi hii kabla wazazi wetu hawajazaliwa na tutakufa tutawaacha, hakuna mfumo wa maisha utakaomaliza umaskini wa binadamu.
 
Wewe ulitaka tulinganishe na nini??? Endeleeni kupiga kelele tunajua kisu cha Lissu kimegusa mfupa. Ndo mwisho wenu kutapanya hela za kodi za watanzania mtakavyo
Lissu mwepesi tu kwa wenye kuielewa dunia. Kwenu labda ndio anaonekana superstar.
 
Nimeanza kufuatilia haya mambo ya siasa kabla hujazaliwa.
Nimekuuliza wale wanajeshi wa Tanzania waliokwenda Kongo walienda kwa mandate ipi ya UN au AU? Pili nani alitoa vifaa na kugharimia uwepi wao kule Kongo ni AU au UN?

OAU na sasa AU haijawahi kutatua mgogoro wowote zaidi ya maneno matupu. Kila mgogoro wa bara hili uluowahi kutatuliwa ni UN ndio walihusika tena kwa kusaidiwa na nchi za magharibi.
 
tanzania hii hakuna mkoa ambao ni masikini wa rasilimali
kila mkoa una rasilimali ambazo kama zikitumika ipasavyo basi kila maendeleo yatakuja katika mkoa husika
 
Mfano mzuri wa maendeleo katika majimbo ni kama hivi; ichukue Rwanda au Burundi irudi Tanzania then baada ya miaka 10 iangalie maendeleo yake, Rwanda au Burundi zingekuwa upande wa Tz toka uhuru zingekuwa zinafanana na Kagera au Singida, je kwa sasa Rwanda na Burundi kimaendeleo unaweza kuzilinganisha na hiyo mikoa niliyoitaja?
 
Mitanzania tu kulipa kodi hamtaki hayo maendeleo hao mnaowasadiki/kuwapenda waume zenu hao wagombea urais wote/chama chochote ndo watawaltea pesa mifukoni? Fanyeni kaz kwa bidii mtaji ikowa jamii yako unatusua....mnapenda bata kuliko kazi
 
Kazi ya AU na UN ni kulinda territory za nchi wanachama, kesi ya eritrea ni kwamba AU na UN zilisimama na Eritrea ili liwe taifa make Ethiopia ni mvamizi alilazimisha muungano, hata zanzibar ikitaka kuvunja muungano, AU na UN hawatakuwa na pingamizi coz since day one tanganyika na zanzibar zilikuwa separated territories. Kuhusu kesi ya somalia nadhani kila mtu na ulimwengu unatambua somalia ni failed states kila jimbo linaibuka na kujitangazia uhuru, lkn pamoja na hayo somalilanda na puntland AU na UN haizitambui hizi nchi
 

..kwa majibu haya, ungekuwa karibu yangu ningekununulia kinywaji baridi, nusu kuku, na chipsi.
 
Sidhani kama kila jimbo litakuwa na askari wake watakufafanulia lakini
 
Objectives za AU na UN almost the same, AU for Africa na UN for world, so if UN is for world manake AU ipo ndani ya UN, wachama wa AU ni wachama wa UN so suala la kongo UN iliamua kulisimamia AU ingiwezaje kujitenga na UN?
 
Hufahamu historia vizuri, unakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kuwa msuluhishi wa huo mgogoro ikashindikana? Eritrea walifanikiwa kimapambano wakateka eneo lao lote na wakajitangazia uhuru.. OAU ililazimika kuitambua Eritrea; Ethiopia hawakuivamia Eritrea ila Eritrea ikiwa sehemu ya Ethiopia iliwahi kutawaliwa na Italy hivyo walivyoondoka ndipo Mfalme Haileselassie akunganisha. Ni kama case ya Caameroun ile iliyotawaliwa na wafaransa na ile iliyotawaliwa na waingereza lakini zote ziliunganishwa kuwa nchi moja wakati wa uhuru.
 
Hivi mfumo wa Majimbo wa Kanisa Katoliki, Lutherani (kule unaitwa Dayosisi), Moravian, SDA, TAG nk. nao huwa unaua uzalendo wa kiimani miongoni mwa wakristo?

..hata benki kuu imegawanywa kikanda/kimajimbo.

..tra nao wamegawanywa kikanda/kimajimbo.

..wakati wa muingereza kulikuwa na majimbo, lakini Watanganyika tulikuwa wazalendo, na tulikuwa na umoja, tukaweza kudai uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…