Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Kwanza niwapashe nyinyi wafuasi wa Lissu kuwa mnaposhabikia mambo anayosema Lissu vile vile mtumie akili ku analyse mambo badala ya kutukana na kumuona Lissu kama ndiye Mungu.

Sera ya majimbo kama ukitokea muujiza Lissu ashinde (sababu haiwezekani kushinda) basi lazima nchi isambaratike.

Ingawa mnatolea mifano Marekani na Ujerumani na Kenya kama mifano ya majimbo ambayo imedumu lakini nchi hizo mbili za wazungu zina uchumi mzuri na wanacnhi wake wameelimika na wanajua kuchambua mambo hivyo hawaburuzwi na wanasiasa. Kwa Kenya bado kipindi ni kifupi kuweza kuwajaji.

Mifumo ya majimbo kwa hao wenzetu kwanza ilijadiliwa ikakubalika na kuingizwa kwenye katiba hivyo chama chochote kikiingia madarakani kinafuata mfumo huo. Hapa kwetu ni sera ya CHADEMA sio muafaka wa nchi, na kwa kuwa hakuna chama kitakachodumu daima madarakani, baada ya muda CHADEMA wakiondolewa madarakani chama kingine kinaweza kubadilisha huo mfumo kwa sababu hauna ridhaa ya nchi hivyo kama nchi tutakuwa tunayumba kila chama kipya kinapoingia madarakani.

Pili Mtambue huo mfumo umewahi kusambaratisha nchi nyingi vilevile nitazitaja:

Yugoslavia: Hii ilikuwa majimbo (federal system) wakati wa utawala wa Rais Tito majimbo (republics) sita yaliitwa Serbia, Croatia, Slovenia, Mecedonia, Montenegro, Bosnia and Herzegovina; na pia mikoa ya Kosovo na Vojvodina iliyokuwa ndani ya Serbia. Baada tu ya kifo cha huyo rais licha ya kuwa aliweka utaratibu wa urais wa mzunguko kwa kila jimbo kupokezana urais wa Yugoslavia hatimaye zilisambaratika tena kwa kupigana vita vikali.

Soviet Union: Hii wengi wanaifahamu kama Urusi. Ilikuwa na Jamhuri 15. Baada ya mageuzi ya kuleta uhuru wa kusema aliofanya Gorbachev hatimaye zilisambaratika. Russia Federataion ambayo ndiyo Urusi ya sasa nayo nusura isambaratike.baadae kama insingetumika nguvu kubwa kuzima muelekeo wa kujitenga uliokuwa umeanza kushika kasi. Ilianza Chechnya ikajitenga, baadae ikaisaidia Inguetshia nayo ikiajitangazia uhuru ndipo Putin akatumia nguvu kuizuia Inguetshia na pia kubadili uamuzi wa kuiruhusu Chechnya ijitenge lakini kwa kumwaga damu.

Ethiopia: Hii nchi inatumia mfumo wa majimbo (federal system). Baada ya vita vya kumng;oa Mengistu vilivyoongozwa na Tigray, walianzisha mfumo huo wa majimbo, Baada ya serikali kuanza kuongozwa na huyu Waziri Mkuu wa sasa Mr Abiy Ahmed, ambaye ni kutoka kabila la Oromo, watigray wengi ambao walikuwa wamedominate serikali walipoteza ushawishi wao. Sasa wameanza chokochoko za kuchallenge mamlaka ya Addis ababa. Hivi karibuni waliamua kuitisha uchaguzi wa jimbo lao kinyume cha katazo la serikali ya Shirikisho kwa sababu uchaguzi ni mamlaka ya serikali kuu sio ya jimbo. Kutokana na chokochoko hiyo ya uasi Waziri Mkuu alikuwa anashinikizwa apeleke jeshi ili kudhibiti Tigray lakini yeye bado anasita. Hivyo kuna wasiwasi kuwa Ethiopia nayo inaenda kusambaratika kutokana na yanayoendelea sasa nchini humo. Jimbo la Oromo nalo haliko nyuma katika vuguvugu hilo. Kwa kifupi majimbo ya Ethiopia yana manung;uniko mengi na kuiona kama hawanufaiki vile walipaswa kunufaika.

Tatu, Hoja za kiuchumi: kuna watu humu eti wanatolea mfano kuwa Dar es salaam wana bandari hivyo watachukua mapato ya bandari, majimbo ya mipakani yatachukua mapato ya mpaka hivyo hakuna jimbo litakalokosa mapato. Kitu ambacho hamuelewi ni kuwa katika mfumo wa shirikisho mapato ya ushuru wa forodha (customs) yaani bandari na mipakani yanakusanywa na serikali kuu sio serikali za majimbo. Hivyo baadhi ya majimbo hayatakuwa na rasilimali za kutosha.

Nne, ongezeko la gharama za serikali: Mfumo wa majimbo ukiruhusiwa maana yake kwa Tanzania kutakuwa na serikali nne hivyo gharama za kuziendesha zitakuwa kubwa sana na italazimika kuwa na kodi kubwa ili kupata fedha za kuendesha serkali hizo. Kwanza serikali ya mtaa (Jiji/Manispaa/ Wilaya) na baraza lake la madiwani, pili serikali ya jimbo na bunge lake, tatu serikali kuu ya Tanganyika na bunge lake, nne Serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzubar na bunge lake. Sijui kama mashabiki wa LIssu wanayaoa haya na athari yake kwao. Huu utakuwa mzigo mzito sana kubebwa na watanzania na wengi humu watajuta kama mfumo huo ukianzishwa.

Tano, Ubaguzi na kujitenga zaidi: Baadhi ya Halmashauri ndani ya majimbo ambazo ni tajiri zinaweza zikadaai zipate mgao mkubwa au wote wa rasilimali zinazotoka ndani ya maeneo yao, mfano Geita wanaweza kudai wanufaike wao zaidi na dhahabu yao kuliko Jimbo zima la kanda ya ziwa kunufaika na mapato ya dhahabu inayotoka Geita. Jambo hilo litapelekea kusambaratisha jimbo na nchi. Aidha hata ajira zinaweza kutolewa kiubaguzi kwa kuajiri watu wanaotoka katika majimbo husika tu. Pia Majimbo yanaweza kutunga sheria za kibaguzi mfano kupiga marufuku pombe na baa; mapenzi ya watu waliokubaliana kwa hiyari nk.

Mwalimu wa idielogy wa Mao Tsetung aliwahi kusema kuwa ninanukuu: A country is not like a machine which you can take it apart and then assemble it again”
 
Tatizo la mfumo uliopo ni hili tunalo liona leo anaingia kiongozi mbinafsi anachota fedha zote toka hapo kwenye hadhina kuu na kwenda kujenga kwao kila kitu, chini ya utawala wa majimbo hilo halingewezekana, eti hapa nilijenga barabara hii kwa sababu mlinichagulia furani, hizo habari zitakuwa mwisho, kupiga simu kwenye kampeni na kuamrisha ujenze wa barabara sehemu fulani itakuwa mwisho.
 
Tatizo ulifeli darasa la.7
 
Mie napigia mstari TU maana yote ulichoandika hapa ni madini!
 
Kenya enzi ya KANU ilikuwa nchi ya kijinga kwelikweli ila baada ya mabadiliko ya katiba Kenya unaiona sasa ilipo? Yani khaya mazimwi yoooteee yameondoka sisi tumebaki na hili la CCM tumeling'ang'ania.
Uko wapi wewe?Kenya wanashida saana na sera ya majimbo. Mpaka hivi sasa kila kitu kimedorora hata wanataka Rais avunje Bunge! Mgawanyo wa fedha KAA LA MOTO. Amka usishabikie sumu itakayoua utaifa.
 


Hapa ndio kwenye "SHIDA" pale ambapo raisi wa nchi anaitenga baadhi ya mikoa kwenye Mipango ya Maendeleo, anadiriki kusema sasa kaskazini Maendeleo basi! Tuachie na mikoa mingine!

Pale ambapo raisi anasema "siwezi kuwaletea Maendeleo watu ambapo wamechagua upinzani"

Wakati watu hao na mikoa hiyo inayotengwa kimaendeleo inalipa kodi tena nyingi tu kwenye mapato ya serikali, alafu fedha zao zinaenda kujenga mikoa na maeneo mingine huku wao wakiona kabisa wametengwa kimaendeleo kwasababu tu yakisiasa au chuki za kikanda! Wakati hela zao unakusanya kila siku!

*Kwanini wasinung'unike na kulalamika?!

*kwanini wasifikirie labda utawala wa majimbo utawaletea haueni kwenye kutengwa kimaendelo?!

*kwanini wasifikirie hata "kujitenga" kama kodi wanalipa lakini kwasababu tu za chuki za kikanda na kisiasa unawanyima maendelo?!

*wanashangaa unasema "MAENDELEO HAYANA CHAMA!" huku unasema "SIWEZI KUWALETEA MAENDELEO WAKATI MMECHAGUA UPINZANI!"

kwani kuchagua upinzani ni dhambi?! Au ni kosa la UHAINI?! mbona basi katiba yetu imeruhusu upinzani hapa nchini?! Kwanini uwatenge watu, majimbo yao ya uchaguzi, au mikoa yao eti kwasababu tu wamechangua upinzani?!

NANI ANALETA UTENGANO NA FIKRA ZA KUJITENGA KWENYE HALI HII?!

Tanzania tumejengwa kwenye umoja, amani na mshikamano! Lakini utawala kutenga kanda Fulani au majimbo yaliyochagua wapinzani ndio mwanzo wakuleta utengano na chuki za kikanda!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Wewe unachukia lakini raia wanashangilia! Magu kwa kweli atasababisha magonjwa ya moyo kwa jamaa zetu! Maendeleo hayana chama! Mungu azidi kumuinua, kumbariki, kumlinda na kumuongoza jembe letu rais Magufuli na serikali yetu yote! Mungu azidi ibariki Tanzania!
 

Ni Dhahiri kwamba CDM hawana jipya zaidi ya kutaka kugawanywa nchi na kurahisisha kuvunja Muungano wa nchi na hivyo kurahisisha utengano.
Kuleta mfumo wa Majimbo ni jambo ambalo halikubaliki kwa namna yoyote.
 
Labda utuambie. Sie atuijui??? Nyie mnajua dhambi gani yake????

Alafu kumbe na nyie ni miungu??? Mnajuaje dhambi za watu???
Sio lazima uwe Mungu ili ujue dhambi ya mtu. Mbaya sana kuifanyia ukuadi mbaya nchi ambayo wazazi wako wote wawili walizaliwa.
 
Usione vyaelea. Unajua imewagharimu kiasi gani kufika hapo walipo?.

Acha propaganda mkuu. Hakuna kilicho kizuri bila kujitoa sadaka. Hata sisi tungekuwa tumepigania uhuru - tungeona maana ya uhuru. Wengi wetu hatujui uhuru maana yake nini. Mfungwa anaweza kueleza zaidi uhuru ni nini kuliko watu wengi sana humu nchini!!

Kama walipitia hayo na wako hivi? Sisi yatusa kupitia nini?? Au tukae hivi tulivo?
 
Ujinga unao wewe mkuu, hakuna anayemwomba Magufuli kufanya kila kitu kwani wapo wabunge wenye kuwakilisha maoni ya mtu wa chini kabisa.

Wapo madiwani wenye kazi ya kumwakilisha mtu wa kawaida.
Tatizo letu ni unyonge wa kifikra na kuwa negative katika kila jambo.
 
Uko wapi wewe?Kenya wanashida saana na sera ya majimbo. Mpaka hivi sasa kila kitu kimedorora hata wanataka Rais avunje Bunge! Mgawanyo wa fedha KAA LA MOTO. Amka usishabikie sumu itakayoua utaifa.
Yaani Kuna watu wapo usingizini Tena wa pono wanahitaji gongwa tosi zao kwa nyundo ya kuvunjia Mawe! Unashabikia majimbo, seriously!? Hizi akili za kukopi na kupesti hizi taaabu kweli kweli! Wasamehe bure!
 
Wapenda teuzi kama bashite utawala wa majimbo mnaona kama kaa la mawe
 
Hivi kuna sera mbaya kama ya mtoto wa kambo- Ukichagua Upinzani sipeleki maendeleo' na kweli sehemu za wapinzani hakuna kitu kinaenda. Mbona sio deal leo iweje sera ya majimbo yenye ugatuzi wa madaraka iwe shida?
Nani anaua mshikamano, kati ya hizo sera mbili?
 
Polee sana!

Nianzie hapa?? Kwani Chadema wamesema wapi kuwa wataanzisha huu mfumo wa majimbo bila kushirikisha wananchi???

Kwani hii katiba tunayoitumia sasa ni wapi na lini iliindinishwa na wananchi????? Mbona tunaitumia hadi leo????

Tatu kwa nini hautaki sisi kutumia mifano ya nchi zilizofanikiwa kwenye Sera ya majimbo alafu unataka kutulazimisha tuamini mifano ya nchi ambazo hazijafanikiwa??

Nne unasema mapato ya forodha kukusanywa na serikali kuu , Wapi imeandikwa kuwa lazima mapato ya forodha yakusanywe na serikali kuu???? Ni msahafu upi umeandika hayo????

Kwani ni lazima mfumo wa mundo wa serikali uwe kama unavyopendekeza wewe??? Kwani sasa hakuna wakuu wa mikoa??? Hakuna wakuu wa wilaya??? Hakuna Madas??? Hakuna Maras????
Huu nao sio mzigo????

Unasema majimbo hayatakuwa na rasilimali za kutosha??? Labda nikuulize kivipi???? Na labda nikuulize unajua muundo wa majimbo yetu utakuwaje????

Unasema ubaguzi na kujitenga zaidi, Mbona kwenye mfumo huu magufuli ndo kajitenga zaidi??? Alivyosema kule kilwa hawezi kujenga stendi sio ubaguzi???? Alivyosema bunda hawezi kupeleka maendeleo kwa wapinzani sio ubaguzi???
Nitolee mfano wa ubaguzi wowote waliofanyiana watanzania alafu nitakujibu kwa mifano mingi zaidi ya ubaguzi alioufanya magufuli???
 
Huo utaifa upo? Katika kipindi hiki cha Jiwe kuna utengano mkubwa sana miongoni mwa watanzania! Kwake yeye ukichagua upinzani basi hilo jimbo halitapata maendeleo kamwe! Ni mfumo wa majimbo pekee utakaoondoa aina hii ya usultani!
 
Mtu unazunguka kuonyesha ujinga wako wote kuunga mkono juhudi muda ukifika upate uteuzi kumbe ukweli unaufahamu na unauweka mwisho. Namba 6 katika orodha yako ya mabaya, ndiyo maana halisi ya Utawala wa Majimbo yakiwa ni maeneo ya uzalisha kwa maendeleo yao yakisimamiwa na Serikali yao waliyoiweka madarakani wao wenyewe na kuitupilia mbali wakati wowote kama dhaifu. Mapato yote yatakayotokana na juhudi zao za uzalishaji yatatumika kutekeleza miradi ya maendeleo inayobuniwa kutokana na kipaumbele cha wananchi kwa faida ya wote. Kizuri chochote kina gharama lakini afadhali kugharamia kizuri kitakachodumu kuliko kugharamia kitu hafifu ambacho kina kila dalili ya kufa baada ya muda mfupi ikalazimu kupata kingine mbadala mara kwa Mara. Marekani ilianza na Majimbo 13 sasa Ina Majimbo 50 miaka 330 toka ipate Uhuru kutoka kwa Mwingereza hiyohiyo kama sisi hawajateteleka mpaka wanaongoza dunia kwa mengi. Serikali Kuu ya Marekani miaka ya karibuni iliamua kuanza kuchimba mafuta yaliyogunduliwa Jimbo la pembezoni la Alaska na kuyaleta Majimbo ya kusini kwa Bomba mpaka katikati ya nchi badala ya kuagiza toka Uarabuni. Alaska walifurahi sana maana ajira zitapatikana na mapato ya uhakika pia kwa maendeleo lakini Majimbo kadhaa ya kusini yamekataa katakata Bomba kupita kwenye Majimbo yao kwa sababu litachafua mazingira. Tatizo letu ni elimu hatuna sanasana huko CCM wakisikia Majimbo wanahamaki kumbe inaweza kuwa ni Mikoa iliyopo ila isitawaliwe na Serikali Kuu kama ilivyo sasa ambapo wafanyakazi muhimu ni makada wa Chama Tawala wanaoteuliwa na Mwenyekiti na wanawajibika kwake siyo kwa wananchi. Mapato ya Mikoa inakusanywa na Serikali Kuu na matumizi yake yanaamuliwa hukohuko bila wazalishaji kuhusishwa wala kuwa na usemi matokeo yake fedha za Umma mara nyingi zinatumika vibaya. Muundo wa sasa unanufaisha viongozi wa Serikali Kuu ndo maana wanaogopa mabadiliko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…