DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kushughulikia wachawi kama ni wachawi kweli binafsi sinaneno.

Tena awashughulikie hasa. Lakini kuchomoa watu Hela ndio naona si Sawa .

Halafu atakuwa na pepo la utambuzi anajua mwenye Hela na asokuwa nayo.
 
Huyu jamaa kama hatumii nguvu za giza basi atakua mchawi. Si kwa nyomi lile analoingiza. Ajabu yuko machokoloni lakini anajaza uwanja full haus.


Ni kweli.
Maana anaweza kutambua mwenye Hela na asokuwa nazo.
Yaani ukifika pale kwanza wale wakongo wenzio ni wa jeuri jeuri tu.
Very aggressive utasema hauko mazingira ya kanisani.

Wanataka waogopwe.
Ukishanidai Hela maana yake nakuwa mteja wako , kama ni mteja Kwanini unifokee, Kwanini unidumie kama hisani?!

Kuna jamaa aliwazingua kinoma!
 
Kuna masai alienda kuombewa ndugu wakachanga watu wenyewe wamechoka maskini ya Mungu!

Wakatoa Hela kwenda kumuona akasema wakaongeze Hela na hapo Hela ya awali walishampa,

Huduma hawa kupata akawaambia wakalete Hela nyingine waje amponye,

Masai wakasema Hawana akawafokea tokeni nje kama hamna Hela .

Huruma imagine Hela ya awali imeenda bure bila huduma yoyote na kufukuzwa .
 


Nazani ndio maana anadharau sababu watu wanaendelea kupigwa na hawastuki na vyombo vya doła vyenye dhamana ambavyo tuna ani viko kazini 24/7 lakini havistukii wananchi kuibiwa kwa njia ya ulaghai?
 
Hakuna utapeli hapo ,umejipeleka mwenyewe ukishindwa acha
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Siyo kila anayejiita nabii na anahubiri jina la Yesu ni mkristo. Ukristo una principles zake. Ndiyo maana Yesu alisema siku ya mwisho kuna watu atawakataa lakini watamjibu walifanya miujiza kwa jina lake lakini ajibu SIWAJUI. Miujiza SI KIGEZO CHA UKRISTO au kwamba mtu ameitwa/ametumwa na MUNGU
Sawa. Hayo ndiyo Yesu aliyoyaita KIZAZI CHA ZINAA. Kizazi cha kutafuta miujiza. No matter who performs the miracles in no matter who's power basi wataifuata hiyo miujiza huko. Hata kama inatendeka kwa nguvu za shetani comouflaged in the name of Jesus, poteleambali. A really bad generation!
 
Huduma zote za kinabii ,kichungaji ,kikanisa kiutume na kiroho nikilainishi cha serikali ili kuwatiisha chini ya mamlaka ,serikali haiwezi chukua hatua mpaka nabii aanze kuua kondooo ,kiunafki serikali itamshika shika kufunika kombe mwanaharamu apite.
 
wacha afanye mambo ata kama ni uongo,mtaani tunaumizana sana,wakati mwingine mikwala ni muhimu sana!!!
 
Wewe umeona kosa kwake, ila Serikali haijaona kosa kwake, usidhani kwamba hayo uyasemayo Serikali haijui, inajua, kama kuna uvunjifu wa sheria ama la, na ipo makini kuliko unavyofikiri na kama kuna kosa itachukua hatua dhidi yake, muhimu utoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama uhitajikapo kama kweli una nia njema.
 
Wewe ni suguye ,Mwamposa au malisa au Musa naona amewazidi ,jamaa anaouwezo Mkubwa sana yule sio level zenu

Nitajie nabii ambapo kuniona ni bure


USSR
 
Hakuna alicho andika cha kweli kwani wananyang'anywa watu wanapona wewe unaleta siasa


USSR
 
Wajinga ndio waliwao

Lakini hii inaonesha wazi jinsi watu walivyo na shida pamoja na kukosa tumaini, lakini ukiwaambia mwende katika makanisa ambayo yanafuata misingi ya Kristo wanatafuta shortcut

Waache wale jeuri yao
Hayo makanisa mafuata misingi ya Kristo yatoe solution basi kwa matatizo yao basi

Wao ndio tatizo la kusababisha waumini wazurure

Sidhani kama kanisa lina majibu na matatizo yao hawawezi zurura kutafuta solution hata kwenye imani potofu watatulia

Mwenye shida hana dini atasaka ufumbuzi kokote atakapoona kuna msaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…