Serikali haioni hivi vichwa vilivyopo JamiiForums?

Serikali haioni hivi vichwa vilivyopo JamiiForums?

Paschal Mayalla:
1. Ni msomi mwenye taaluma ya Sheria na uandishi wa habari

2. Ni Mwandishi wa Habari mwenye uzoefu wa miaka mingi

3. Ni mtu jasiri anayejiamini

4. Ni kada wa Chama Tawala asiye mwoga kukisemea pale inapobidi

5. Alishawahi kugombea nafasi ya ubunge EALA lakini kura hazikutosha

6. Anafaa kuwa Msemaji wa Serikali, Mwandishi wa Rais, Mbunge, Waziri, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa TBC, Mkurugenzi wa Manispaa au Jiji na nafasi zinginezo zinazofana na hizo.
Kuna masharti na vigezo hana, yuko 65+yrs.
 
Mshana Jr:
Japo ni mwana CHADEMA, lakini linapokuja suala la maslahi ya Taifa, masuala ya vyama huwekwa pembeni. Serikali isione aibu kumtumia kwa sababu tu ya itikadi zake za kisiasa. Mbona ilimchukus Profesa Kitila Mkumbo alipokuwa bado ni mwanachama wa ACT WAZALENDO, Anna, n.k. japo waliishia kuhamia CCM?

1. Ni mtu mwelewa mwenye exposure kubwa

2. Uandishi wake unaonesha kuwa ni msomi anayejitambua na mwenye uelewa wa mambo mengi

3. Ni Mtanganyika Mzalendo

4. Ni mtu anayesimamia kile anachokiamini. Akiamua kukosoa hufanya hivyo bila aibu. Kwa ufupi si mnafiki, ni mtu jasiri

5. Anaweza kuteuliwa kushika nafasi zisizo za kisiasa kama Ukatibu Tawala wa Mkoa, Ukurugenzi wa Masharika ya Umma, Mjumbe wa Bodi, ubalozi, n.k.
Umri umeenda, kuteuliwa 60+yrs labda uwe mstaafu serikalini cheo kikubwa mf CDF, Wakurugenzi nk. Mshana Jr ni mtaalamu mstaafu sijui alifika nyota ngapi kule kilingeni.
 
Tutawapata vipi wakati nyie na Wanawake wenu mnafunga PM.
Ngoja tuendelee kuwatumia Uvccm na wale wanaunga juhudi
Wekeni majina yenu wazi ili mjulikane vizuri na hoja zenu; hiyo ndio marketing na branding yako!!
Mfano si huyo Mubyazi wenu hapo JF ; mawazo na misimamo yake inajulikana sio ya kichawa na ndio maana anapata uteuzi!! Sasa nyie wakina Mayalla Njaa leo uko ccm kesho unaponda ccm , huwezi pata uteuzi kwasababu ni opportunist, kwa lugha nyepesi MNAFIKI !
 
Wekeni majina yenu wazi ili mjulikane vizuri na hoja zenu; hiyo ndio marketing na branding yako!!
Mfano si huyo Mubyazi wenu hapo JF ; mawazo na misimi yake siyo ya kichawa anapata uteuzi!! Sasa nyie wakina Mayalla Njaa leo uko ccm kesho unaponda ccm , huwezi pata uteuzi kwasababu ni opportunist, kwa lugha nyepesi MNAFIKI !
🤣🤣🤣🤣
 
nipo huko siku nyingi sana,
na kwa miswada makini sana hii ya uchaguzi na tume ya uchaguzi tunajadili hapa mjengoni,
najiskia kuomba tena ridhaa kwa wananchi kwa awamu nyingine tena 2025-2030...
Joannah baba mtumishi kumbe yuko mjengoni na bado sadaka zetu anazitaka 😂😂😂
 
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba wewe ni mmoja wa hao unaowapigia debe ila umekuja kwa ID nyngine.
Hapana mkuu! Mimi siyo Mshana Jr wala Paschal Mayalla.

Humu kuna wataalam wa maandishi. Waliifuatilia uandishi wangu na hao magwiji watagundua ni kama mawingu na ardhi. Hakuna mfanano hata kidogo, naamini.

Na kwa nini Watanzania wengi wako suspicious? Ina maana watu hawaamini kuwa kuna Watanzania wanaoweza kuvisifisia vipawa vya wenzao?
 
Back
Top Bottom