Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

Anayehitaji kumpima mtumishi (tuseme afisa utumishi) ndo anatakiwa aje na kifaa chake cha kupimia achukue vipimo aendelee na utaratibu wake, kumlazimisha mtumishi kujaza taarifa ili ziweze kutumika kumpima ni unyanyasaji maana unampunguzia muda na ufanisi wa kufanya majukumu yake ya kila siku awe anahangaika namna ya kujaza taarifa za kumpima.

Kwa maana nyingine hilo zoezi lao linamwongezea mzigo mtumishi ambaye bado anahangaika na mshahara kiduchu na kikokotoo kausha damu.​
 
Pia mfumo ume assume sote tuna fanya routine works...Kusema ukweli Hawa utumishi sijui kwanini hawataki kuelewa Webber alishafanya hizi tafiti nakuona ukimfanya binadamu kama Robbots uzalishaji unapungua
 
Huu mfumo hatari sana, hapa bila Mwenye nchi kuingilia itabidi watumishi wawe watumwa kwenye huo mfumo kwa sababu zifuatazo:-


Kwanza, ni mfumo unaogitaji mtumishi anunue bundle kwa pesa yake. Experience ni kwamba kuna watumishi wana magroup ya WhatsApp wanayopeana taarifa za kazi, lakini kuna exception ya baadhi yao na wanawapigia kufikisha ujumbe... Wakiamini wanaishi maeneo magumu kimtandao, kiuchumi n.k. sio kila mara mtumishi atakuwa na kifurushi cha internet... Hali ni ngumu sana vijijini, hiyo 500 ni pesa ndefu sana. Mf watu mnasikiaga mtoto kachomwa moto kwa ajili ya kitu cha thamani ndogo, mana yake hali ni tete kuipata hiyo thamani mzazi anaumia.

Pili uelewa kuhusu matumizi ya huo mfumo. In short hao wakuu na wasaidizi wao wengi wamefanya kazi ngumu sana ya kuwaunganisha watumishi wasiokuwa na uelewa kwenye mfumo, tena wakiwaambia wasafiri waende makao makuu wa taasisi especially halmashauri na manispaa, au taasisi nyingine watumishi walio mbali walilazimika kutumia gharama kufanyiwa mchakato wa kuunganishwa. Kumbuka watoa mafunzo kutoka Ofisi za Utumishi walitoa mafunzo kwa makundi makubwa ya watumishi na wengi hawakueleweka hata na wale walio Head quarter's. Kilichotokea zoezi lilivyoanza watu walijiongeza na usumbufu mwingi sana. Na ili kuokoa jahazi waliamua kuact na kuwasaidia wale wasio na uelewa.

Hali ilivyo sasa ni kwamba majority hawaelewi mfumo, na hawajui ndio umeanza kutumika ama wasubiri maagizo namna ya kutuma hizo taarifa. Na waliopata mwanga kidogo wanatuma taarifa bila kujua ndio inavyotakiwa ama la. Na kuna wengine wanajua ndio mambo ya mfumo yamekamilika. Na kuna wengi sana vijijini hawana hata simu janja na hawazihitani kwa sababu hawajui kuzitumia sijui kitatokea nini. Endapo watalazimika kutuma taarifa watakuwa wanasaidiwa bila kujua kinachoendelea humo panapo PEPMIS
 
Reactions: Ame
Mfumo ni mzuri ila utekelezaji wake ungezingatia variation zilizopo, na pia ungetoa majibu sahihi Kwa watu specific. lakini kutengeneza one fit all solutions kwenye hizi variations ni kuleta utendaji wa ki robbot ambao utashindwa kuleta tija na badala yake watu kutimiza wajibu
 
Haya mambo ya vikisomwa kwa pamoja, blabla, mara circular ndivyo vikanifanya nione govt kuna ulafa mwingi ambako sistahili kuwepo huko. Ni sehemu ya kufanyia kazi vilaza na wanaotaka pesa mtelezo tu tena zenye dhambi kabisa. Kanuni nyingi kwelikweli, lakini kila report ya CAG imejaa wizi tu.😩
 
Vipi kuhusu Mifumo mingine waliyo nayo haifanyi kazi?
Hawatumii simu za mkononi kuingia whatsapp?
Na kufanya matumizi mengine?
Kutumia simu yake ya mkononi kuingia whatsapp ni swala binafsi maana anatumia muda na gharama zake, vipi unataka kumbebesha mzigo kwenye jambo ambalo halina msaada kwake zaidi ya kumwongezea usumbufu na gharama.​
 
Kutumia simu yake ya mkononi kuingia whatsapp ni swala binafsi maana anatumia muda na gharama zake, vipi unataka kumbebesha mzigo kwenye jambo ambalo halina msaada kwake zaidi ya kumwongezea usumbufu na gharama.​
Kuna maswala huwa yanafurahisha sana Mtu mwenye Akili Timamu akiyaongea..
Pia inanipa mashaka na Nianze kuhoji vitu vingi kuhusu Yeye..

Taarifa na Report ya kazi Unazofanya kutimiza wajibu wa kati yako ikiwa pamoja na kuithamini kazi inayokupatia Kupato cha kununua simu na kuweka bando unalotumia..

Unaita Swala binafsi kwahyo kazi yako sio swala binafsi..
Me naona ngoja mifano itoke ndo akili zitawarudia watumishi wachache wenye akili hizi..

Ambao wenyewe wanaona Ofisi walizonazo sio Jukumu lao ila ni jukumu la watu fulani
 
Kwa hiyo mtumishi atumie mshahara kiduchu kununua smart phone ili ajaze taarifa kwenye mfumo? maafisa utumishi kwenye vituo vya kazi kwa nini wasiwatembelee watumishi na kuwapima, yaani mtumishi afanye kazi zake halafu afanye na majukumu ya afisa utumishi.​
 
Mtumishi kafanya majukumu yapi ya Afisa utumishi?

Kwahyo mtumishi huyo hana Smartphone?
Pilot ya Mfumo imefanyika Kupitia mifumo mingi kabla ya hiyo na kupitia GPS za eMap kipindi wanafanya kuweka Raman za kielectronic za ukaguzi wa Shule na Vituo vya kutolea huduma ya Afya..

Hakuna sehemu yenyew changamoto wa kimfumo iliyoonekana..

Watumishi wamekuwa wakitumia FFARS (Ambao upo ndani ndani mpaka kwa watendaji wa vijiji), PlanRep ,DHIS2, mfumo wa taarifa za shule "SIS", ..Gothomis, Na mifumo mingine mingi..

Kabla ya mfumo wa PEPMIS kuingizwa kwenye watumishi portal ess..

Watumishi Portal.ilikuwa hewani kuanzia mwezi April mwaka jana 2023 na ulionekana kutumia Cache report na Ip adress na Ping Report kuwepo kila kijiji na kila kata mpaka kufikia mwaka 2023 mwezi November Asilimia 94 ya watumishi walikuwa wamejiunga..

Sasa sijui malalamiko yako ni yapi..
Ungeniambia ili.nipate kuyajua
 
Watumishi wao wanalia mishahara duni huku gharama za maisha zikiongezeka na kile kikotoo cha kustaafu ni cha kinyonyaji, haya ya mfumo hayana maana kwao.
 
Watumishi wao wanalia mishahara duni huku gharama za maisha zikiongezeka na kile kikotoo cha kustaafu ni cha kinyonyaji, haya ya mfumo hayana maana kwao.
Ya mfumo hayana maana?
Tutakupimaje kama kweli kazi ulizopatiwa na serkali unazifanya kweli?
Tutajuaje kama wananchi wanapata kweli Huduma?
Zaman tulijipima kutumia mifumo.Ya karatasi Yaani OPRAS ila kwa sasa Tuko kidigital Ni PEPMIS..
Sioni tofauti ya OPRAS na PEPMIS..

Labda kama wewe ni mwajiriwa mpya
 
Lipeni kwanza mishahara ambayo TUCTA wanapendekeza ikiwemo ile nyongeza ya 23%, posho na likizo kwa wakati, rudisheni kikokotoo kilichokuwepo, halafu mje na mifumo.
 
afadhali wakatwe mishahara
 
Vipi kuhusu Mifumo mingine waliyo nayo haifanyi kazi?
Hawatumii simu za mkononi kuingia whatsapp?
Na kufanya matumizi mengine?
Umefanya tafiti ukajua wanao ingia whatsapp ni asilimia ngapi ya watumishi wote nchi hii? Maana jibu lako linaonesha kabisa huna tafiti ila unaongea kwa mihemko tuu, nina ushahidi kuna watumishi wanaingia whatsapp siku wakija mjini kufata mshahara tuu na wengine wengi hawana hata hiyo smartphone.
 
Mkuu!
utafiti umefanyika Na kabla ya kupubllish Mfumo ni kimoja ya Vitu vilivyotiliwa mkazo sana..
Kabla ya kuuweka Mfumo ilifanyika mifumo mingine kama pilot na ilifanikuwa wa 97% Mpaka vijijini nimetoka kidogo Ufafanuzi wake soma Comment no #92...

Hakuna Utafiti umeanza kufanywa kwa muda mrefu kama Huu wa watumishi Portal watumishi Portal Kabla ilianza kutumika Miaka ya nyuma sana Tangu kipindi cha Magufuli..

Baadae mwaka 2019 mwishoni Ukaenda kurekebishwa na baadae Wizara ukaona kuuboresha mfumo huu kwa kufanya Tafiti na mwaka 2020 mlitangaziwa (Kama utakuwa na kumbukumbu) kwamba Mifumo ya Uhamiaji na Oprass Itawekwa Online..

Mwaka 2022 ikafanyiwa pilot kwa baadhi ya maeneo ikiwemo mkoa wa Tanga,Lindi ,Mwanza na Simiyu na Pilot ilionyesha ufaulu kwa 98%..

Baadae mwaka 2023 mwezi wa April kuliachiwa Module kadhaa ikiwemo module ya uhamisho (Tansfer), lengo lilikuwa ni kufanya Ping Location kutoka maeneo mbalimbali Na nakuhakikishia walimu wengi hao unaowataja walionekana kutoka pande zote kwa 84% Ya maeneo mengi ya Tanzania..

Ndo ikaongezwa Module nyingine ya Salary slip,eLoan nazo pia Kwenye eLoan ilionekana Imesajili location kwa 97.7% za Tanzania nzima..

Na Baadae Ikawa lunched Program nyingine kwa ajili ya kuangalia ufanisi wa network nayo pia kwa asilimia kadhaa ikaonyesha iko sawa...

Hiyo yote kabla ya kuwekwa kwa PEPMIS...
Hakuna mtumishi alilalamika kuwa kuna tatizo la mtandao na blah blah nyingi na walikuwa wakitumia vizuri tu mfumo..
Na hata Walipowekewa baadhi yao huo mfumo bado cookie zilisoma kuwa bado asilimia hazijashuka..

Ila tu walipoambiwa Waweke mipango kazi na Kazi zao na viongozi wao wawapime kwa kazi zao kila siku na Hakutakuwa na OPRAS ndo malalamiko yameanza..

Nataka nikuhakikishie kwamba majaribio ya Mfumo huu yalianza mwaka 2018 kipindi haiitwi Ess ilikuwa inaitwa watumishi Portal na ilikuwa inaandikwa Watumishiportal.utumishi.go.tz....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…