Serikali iboreshe sheria ya Ndoa za Kikristu ili ziruhusu talaka kuepusha mauaji na fumanizi

Serikali iboreshe sheria ya Ndoa za Kikristu ili ziruhusu talaka kuepusha mauaji na fumanizi

Mtoa mada!

Sio kwamba serikali haiwezi kuvunja ndoa za kikristo, inaweza kufanya hivyo. Kumbuka madhehebu mengi ya kikristo yanatumia cheti cha serikali wakati wa kufunga ndoa.

Hivyo, mahakama zina uwezo na zimekuwa zikitenganisha ndoa nyingi tu za kikristo kwa kuruhusu wenza wapeane talaka.

Shida inakuja kuwa makanisa mengi ya kikristo hasa haya mainstream, hata kama ndoa ikitenganishwa na mahakama wao bado wanaendelea kuchukulia kuwa hiyo ndoa bado ipo.

Matokeo yake ni kwamba wahusika wote wawili mtatengwa na hamtaruhusiwa kufunga tena ndoa ndani ya kanisa husika.
Duh
 
Serikali ilitazame hili kwa jicho la dharula!

ndoa nyingi sana zimekuwa chanzo kikuu cha mauaji!

Ukipitia mafaili na report za kipolisi asilimia kubwa ya mauaji ya kimapenzi ni ndoa za kikristo!

Swali: Kwanini za Kikristo ndiyo zinaongoza!
Jibu: Ni kwasababu serikali haikutoa utaratibu rahisi wa kuachana (Talaka) kwenye ndoa za kikristo!

Hivyo imewafanya wakristo wanaofight divorce kuishi maisha hatarishi zaidi kutokana kwa wenza wao, mbali na migogoro mikubwa ya kupigana na kufumaniana pengine wengine hadi wanaletewa magonjwa kama ukimwi kwa kukosa namna ya kupata talaka

Mfano
Kuna scenario ya mama mmoja ambaye ameishi na Mme wake na kupata watoto watatu kwa kuvumilia, lakini uvumilivu umefika mwisho baada ya mmewake amekuwa ni wa kumpiga, matusi na kumdhalilisha, Mama huyo kariporti Mara kadhaa polisi lakini hajui afanyeje ili apate talaka kisheria!(divorce)

Pamoja na kipigo na masimango, malalamiko mengine ya yule mama ni mmewe kuwa na vimada wengi hadi na mabinti wa kazi ambayo yote kayavumilia lakini hili la kupigwa mme wake anaporudi kalewa limemshinda.

Hivyo kwa mateso ya mama yule, ni dhahiri yupo hatarini kufanya au kufanyiwa mauaji mda wowote!

Lakini kungekuwa na utaratibu mwepesi wa talaka wangeachana kwa Amani! Lakini hajui afanyeje!

Wahanga wa ndoa za kikristo ni wengi sana! Wanandoa wengi wa kikristo wametengana hadi makazi lakini huwa wanafuatiliana ili kufumaniana! (FUMANIZI kwa mgongo wa cheti cha ndoa)

Ndoa zenye migogoro mkewe/mme wanaotengana makazi miezi sita, au mwaka au miaka miwili kila mtu yuko kivyake, lakini kwasababu wanamiliki vyeti vya ndoa hufuatiliana kufumaniana kwasababu HAKUNA TALAKA! (Ili kuprove wrong kwa jamii mmoja amchafue mwenzake)

wahanga wakubwa zaidi wa hili ni wanawake kwasababu ya ushahidi wa tumbo wanapopata wenza wapya na pengine kupata mimba huko!

Nitoe rai kwa serikali Ione umhimu wa kuboresha sheria za ndoa za kikristo kupeana talaka isiwe jambo gumu la kutoana uhai kama kesi za ardhi!

Serikali itambue haina dini, hivyo itengue na mambo ya iman yabaki kiimani, kama vyeti vya ndoa inatoa serikali basi iruhusu pia kutoa talaka kuliko ilivyo ngumu sasa.

Ilivyo sasa inahitaji watalaam sana kufuatilia talaka kwa Wakristo hususani kwa wanandoa wasiona uwezo/ueleewa na sheria.
Ndio zote za kidini iwe kikristu, Islamic, Buddha, Indian etc zinakuwa guided na Sheria za dini husika.

Ukitaka ndoa isiyo na maadili na miongozo ya dini ni kwa mkuu wa wilaya tu.

However ndoa zote cheti unapata Cha dini ulipofungia na unapewa Cha serikali ambacho ndio cheti Cha ndoa na vyote vinafanana kinachotofautisha ni details za cheti unazojaza mfano aina ya dhehebu ndoa ya wake wangapi nk.

Sasa kwenye divorce kuna miongozo ya kila dini husika ambapo ndio inatumika kama mabaraza ya usuluhishi. Hivyo kama ndoa ni ya kikristu watasuluhisha na hawatawaachanisha Ila wanaposhindwa kusuluhisha wao huandaa muhtasari tu maaana alichounganisha Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kutenganisha not even a church can do that.

So, ukiona wameshindwa kusuluhisha uke muhtasari huwa kama ushahidi mahakamani tena huu utaratibu umewekwa baada ya mvutano mkubwa zamani haikuwa hivi ilikuwa hakuna kuachana kabisa

Hata ukienda Mahakamani ilikuwa hamuachani kirahisi Ila baada ya mabadiliko kwenye sheria ya kanisa na mabadiliko ya kijamii na muda ndipo wakaona ni vema kanisa litoe kama muhtasari wa usuluhishi Ila sio kuachanisha, mambo ya kuachana yakaachiwa mahakamani maana watu wanaweza kupatania mahakamani pia huwa inatokea sana.
 
Mtoa mada!

Sio kwamba serikali haiwezi kuvunja ndoa za kikristo, inaweza kufanya hivyo. Kumbuka madhehebu mengi ya kikristo yanatumia cheti cha serikali wakati wa kufunga ndoa.

Hivyo, mahakama zina uwezo na zimekuwa zikitenganisha ndoa nyingi tu za kikristo kwa kuruhusu wenza wapeane talaka.

Shida inakuja kuwa makanisa mengi ya kikristo hasa haya mainstream, hata kama ndoa ikitenganishwa na mahakama wao bado wanaendelea kuchukulia kuwa hiyo ndoa bado ipo.

Matokeo yake ni kwamba wahusika wote wawili mtatengwa na hamtaruhusiwa kufunga tena ndoa ndani ya kanisa husika.
That's Canon law na ndio maana watu wanapaswa kujua ndoa sio kitu Cha fashion tu kama ambavyo imekuwa siku hizi.

Kama uliapa kwa Mungu kwamba kifo ndio kieatenganishe Ile ni nadhiri ambayo sio ya kumchezea Mungu.

Ndio maana wanaijua hukimbilia kubadili dhehebu na kuoa kwa kanisa jingine especially haya ya kilokole wao wanapokea kila mtu kwa kutumia mistari hiyohiyo ya biblia 😃😃😃😃 hata ukifa wakikutenga walokole wanakuzika tu hakina noma 😃😃
 
Alichounganisha MUNGU mwanadamu hawezi tengua. MUNGU anachukia kuachana. Ukitaka ndoa zakuachana baadae nenda kwingine na serikalini. Kwa wakristo talaka no !!!
Ukiwa na ushahidi kuwa mkeo au mumeo anazini huko nje ya ndoa; ndoa inavunjika
 
Talaka inatolewa mahakamani endapo utathibitisha kuwa ndoa imevunjika na haiwezi kurekebishika pia sababu nyingine ya kupewa talaka ni ukatili iwe ni matusi au kipigo.
Sasa huu mchakato wote wa nn ??? Na mahakama zenyewe nazoooo!! ????
 
Kuomba talaka kwenye ndoa za Kikristo mbona ni simple, uwe na ushahidi.

Halafu talaka ya kikristo unapata nguvu zaidi juu ya uasherati.

Ikiwa na ushahidi ukianzia kwa viongozi wa dini mlipofungia ndoa. Wakiridhia wakiona hii ngoma ipo at the point of no return wanakupa taa ya kijani nenda mahakamani. Issue labda utoaji wa talaka mahakamani unachukua mda mrefu.

Au unataka iwe kama wale wenzetu unalala ukiamaka asubuhi ghafla unakuta talaka mezani?
Ndugu,hakuna kiongozi yeyote wa dini utakaempelekea hoja kuhusu kuachana kwenye ndoa akakupa go ahead,zaidi atakushauri mvumiliane tu.
 
Mkuu sijajua umetoa wapi hii habari kuwa wakristo hawana talaka.

Talaka inatolewa mahakamani endapo utathibitisha kuwa ndoa imevunjika na haiwezi kurekebishika pia sababu nyingine ya kupewa talaka ni ukatili iwe ni matusi au kipigo.

Mshauri huyo mhanga wa ukatili katika ndoa yake kama anataka talaka aende kufanya petition mahakamani kama hafahamu taratibu atafute wakili naye atamsaidia.

Kitu kinachofanya talaka kuonekana ngumu inatokana na watu kutofahamu utaratibu wa kudai talaka, eti mtu anaenda kudai talaka huko serikali ya mtaa au polisi unategemea nini? Kama hufahamu taratibu mtafute wakili akusaidie.
Umenena vema,,,
 
isome vizuri biblia achana na mambo ya kuhadithiwa hayo.kule walipowaunganisha ndio huko talaka inatolewa.uwe na ushahidi kwa hayo ufanyiwayo.
hata kwa waislam ni jambo zito sana kutoa talaka ndio maana zipo 3
sema siku hz watu wanarahisisha tu.
 
Utakuwa hujui Ukristo ila unajaribu kujadili jambo usilojua.
Pia serkali haiingilii imani za watu na kuwawekea sheria.

Kifupi hujui unasema nini.
 
Utakuwa hujui Ukristo ila unajaribu kujadili jambo usilojua.
Pia serkali haiingilii imani za watu na kuwawekea sheria.

Kifupi hujui unasema nini.
Kama wewe
 
Msidanganyane kwamba talaka kwenye ukristo hazipo,kisichokuwepo ni ndoa nyingine ya kikristo baada ya hiyo kuvunjika,isipokuwa mpaka mmoja wenu atakapofariki.

Hivyo kama mmeshindwa tenganeni tu msije kuuana,ila kuoa na kuolewa litakuwa swala gumu.
 
talaka inatolewa serikalini maana hata ukifunga ndoa kanisani lazima ukaandikishe serikalini so ndo inavunjwa ni vile watu wamajibebdsha ukatoliki hatare
 
Ndugu,hakuna kiongozi yeyote wa dini utakaempelekea hoja kuhusu kuachana kwenye ndoa akakupa go ahead,zaidi atakushauri mvumiliane tu.
Kama hakuna anaetoa go on hizi ndoa za makanisani wanafikiaje hadi kuvunja ndoa bila hati mahakamani?
Screenshot_20210807-223041.jpg
 
talaka inatolewa serikalini maana hata ukifunga ndoa kanisani lazima ukaandikishe serikalini so ndo inavunjwa ni vile watu wamajibebdsha ukatoliki hatare
Hahah
 
Rudi darasani ujifunze sheria za nchi kuhusu imani. Kanisa lina uwezo wa kutatua matatizo ya ndoa, ikibidi hutenganishwa na kutoa nafasi ya kurudiana hali ikiwa shwari.
Unataka inchi nzima tusome sheria?
 
Mkristu aliyefunga ndoa kwa baba Paroko hakuna kuachana ndomaana maandiko yanasema kwa waliyojaaliwa tu sasa kama ujajaliwa unaenda kufunga ndoa kwa baba paroko ya nini
Labda wa edit biblia Kwanza Kama itawezekana.
 
Back
Top Bottom