1. Hakuna safari ya kikazi ya Rais ya nje isiyo na tija, kama hufuatilii ni uvivu wako lakini mara kwa mara zinatolewa press conference na DPC Zuhuru kuhusu ziara hizo na faida zake. Dunia ya Sasa inahitaji mazungumzo lakini anapokwenda nje kuzungumza ina tija zaidi kuliko kuwakilishwa bila hivyo tusingesikua Rais wa Marekana anazuru katika nchi za Afrika.
2. Hoja ya pili ni mpaka pale nchi itakapokuwa na wawekezaji wengi na wenye uwezo wa ndani wa kuwekeza kwenye miradi mikubwa. Kwa mfano uwekezaji kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere pekee unagharimi Zaidi ya Dola za kimarekani billion 7 ambazo ni sawa na Trillion 16 za kitanzania. Kwa wawekezaji waliopo ni nani ambaye ana hiko kiwango Cha pesa kutukamilishia ujenzi huo? Hata matajiri 10 wakubwa wakawekeza Kila kitu Chao Bado hawawezi kufanya mradi kama huo. Ingefaa kweli miradi ijengwe na wazawa ili malipo yafanyike Kwa shilingi lakini tuseme kweli tutachelewa Zaidi.
Hoja ya Tatu, Serikali inakopa ili kuharakisha maendeleo na zaidi mikopo hiyo ni Ile yenye riba nafuu sana au isiyo na riba kabisa. Pia, tunakopa ili tuwe na akiba kubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya manunuzi ya nje, bidhaa na Teknolojia. Ingefaa utupe na ufafanuzi, Serikali itumie njia Gani kugharamia Kwa haraka miradi mikubwa kama Tukiachana na mikopo.
Hoja ya nne, umemtaja Makamu wa Rais Dkt.Mpango kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia wizara ya fedha na wizara ya mipango na uwekezaji Kwa uwezo wake wa kitaaluma kwenye masuala ya uchumi na fedha na ndio maana ukataka wizara hizo ziwe chini yake lakini umesahau jambo Moja kubwa ambalo litahitaji majibu baadaye, je asipokuwepo Dkt Mpango katika ofisi ya Makamu wa Rais na akawepo mtaalamu wa Sanaa ofisi ya Makamu wa Rais, je Bado itahitajika wizara hizo chini ya ofisi ya Makamu wa Rais?
Hoja ya Tano, siamini kama unaendesha asasi yoyote ya kufanya tathmini ya uchumi mpaka uje na hoja ya kwamba tunakwenda kutumbukia kwenye mdororo wa kiuchumi. Ni vema hoja yako hii ingejikitika kwenye takwimu halisi Zaidi ya blabla Kwa sababu uchumi ni namba na namba hazidanganyi.